Matuta barabarani: Wakazi watumiao Morogoro road walia

ndugu yangu wa Kimara, hilo unaloliongea kuhusiana na ajali ambazo watu wengi walikuwa wanapoteza maisha yao hapo siku za nyuma si kwamba zitakoma, suala la usalama barabarani ni zaidi ya matuta, matuta yanaharibu barabara pamoja na magari pia husababisha muda mwingi kupotea kwa sababu ya matuta.madereva wa magari wa kwetu hapo Tanzania wanatakiwa wajue kwamba mtembea kwa miguu ni traffic, naye ana haki ya kutumia barabara. madereva wanatakiwa wafuate sheria za barabarani zote.tatizo lililopo nchini kwetu watu hawajali sheria za barabarani. Wanasiasa nao wanatakiwa waendelee na siasa zao kazi za kitaalamu awachie technical personnel, hapo tutayafaidi matunda ya Maengineer wetu wa Tanzania. sasa siasa wao, maengineer wao, wachumi wao hatutafika kwa hilo. kwa sababu uchumi wa nchi ni mdogo na waibaji ni wengi ni vigumu sana kwa nchi kama tanzania kujenga madaraja ya kupita juu na chini kila sehemu. Tunatakiwa tutumie tulichonacho bila kuathiri maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi.

....mwakaleli.......karibu ..hapa tunakata issue mkuu...mwendo wa "kumkoma nyani giladi...".karibu kwenye chama ...chama ambalo mafisadi na mitandao yao wakisikia tu jina JF wanashindwa na kulegea....!!!!

endelea kukata issue kwa uhakika...
 
Baada ya siku kudhaa kutokea malumbano ya hoja kuhusu matuta yaliyo wekwa barabara ya Morogoro road Imethibitika kuwa wakazi wa Kimara mwisho na wengine waishio maeneo mbali mbali kando kando ya barabara hiyo wameyafrahia matuta hayo kwa kuwapunguzia kero katika uvukaji.


Na Christina Gauluhanga, Kimara
WAKALA wa Barabara Tanroad kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa Kinondoni imepongezwa kwa kujenga matuta iliyodumu kwa muda mrefu na kusababisha wananchi kupoteza maisha kila kukicha.

Wakizunguma na gazeti hili baadhi ya wakazi wa Kimara wamesema kuwa, wamefurahishwa na hatua hiyo kwani ilikuwa kero na kusababisha wakazi kuvuka barabara hiyo kwa hofu.

Wamesema kuwa, kitendo cha Tanroad kuweka matuta katika barabara ya Morogoro kimeonyesha ni jinsi gani Serikali inavyowajali wakazi kwani wakazi hao walifikia hatua ya kutaka kuandamana.

"Kwakweli tunashukuru kwa kutatuliwa kero yetu kwani ni ya muda mrefu ambayo wakazi walikuwa wakigongwa mara kwa mara na kufa jambo ambalo lilikuwa kero ya muda mrefu, " amedai mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Deo.

Amesema kuwa, wanafunzi walikuwa wakigongwa mara kwa mara na kufa na wengine kuwa vilema kutokana na magari kwenda mwendokasi.

Hata hivyo mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Juliana amesema kuwa, mbali ya kuwapongeza kwa juhudi hizo pia ni vizuri oparesheni hiyo ikaendelea hadi Mbezi.

"Tunaomba oparesheni hiyo iendelea hadi Mbezi ili kuondokana na kero hii ni kweli Mbezi kuna alama za pundamilia lakini bado tunahitaji zaidi kuwepo kwa matuta, " amesema Juliana.

Amedai kuwa, katika eneo la Mbezi mwisho kumekuwa na mrundikano wa magari na kusababisha wakazi kushindwa kuvuka.


"Kituo cha Mbezi mwisho kuna magari mengi yaendayo maeneo mbalimbali hivyo imekuwa ikiwasababishia wakazi kushindwa kuvuka na kugongwa na magari, " amedai Juliana.
Source Dar leo
 
Baada ya siku kudhaa kutokea malumbano ya hoja kuhusu matuta yaliyo wekwa barabara ya Morogoro road Imethibitika kuwa wakazi wa Kimara mwisho na wengine waishio maeneo mbali mbali kando kando ya barabara hiyo wameyafrahia matuta hayo kwa kuwapunguzia kero katika uvukaji.

Mkuu Fidel na wenzangu wanaJamvi, lile swala la matuta naona limepamba moto kwelikweli.... Magari yanaongezeka, madereva makanjanja tupo wengi, watoto wa shule na maspidi mpaka kila mahali kwenye lami watu wanataka matuta... Haya, hili swala linazidi kutuzidi akili wale wote tuliopo kwenye fani hii ya ujenzi wa mabarabara!!!

Hebu angalia Kunduchi mpaka wameamua kulala kwa barabara, hapo ina maanisha mambo ni mabaya sana.... TANROADS, Jiji etc mpo wapi?? Au bado mpo Kuala Lumpur mnatafiti namna ya kuzuia ajali?? Au privatization of roads itasaidia kupunguza ajali pia??

Walipoomba matuta sehemu nyingine Raisi aliingilia swala lile na kuamuru matuta yawekwe.... Sasa kupeleka Riot Police kupiga mabomu kutawanya watu ndio best solution?? Je wahusika tumeshaanza kuangalia swala hili manake limeanza Kunduchi, kesho hatujui watakuwa wapi na haya mabarabara mapya yanayojengwa kule Sam Nujoma, Port Access, Kilwa, Tegeta etc! Je wale wahandisi wanapofanya design wanaangalia issue ya safety baada ya upanuzi/uboreshaji wa barabara hizo?? Inaelekea we are up for a good ride.... What about wale wa mipango miji?? Je mnatusaidia kuangalia mapungufu yakiwemo ya mushrooming residential areas ambazo zinakuwa divided by major arterial roads (schools, markets etc location in relation to barabara hizi??)

Polisi walaumiwa kwa kupiga mabomu msibani

2008-11-02 12:47:50
Na Godfrey Monyo


Polisi Jijini Dar es Salaam imelaumiwa kwa kitendo cha kupiga mabomu ya machozi katika msiba wa mwanafunzi wa darasa la tatu na kusabisha watu kadhaaa kujeruhiwa.

Tukio hilo lilitokea juzi katika maeneo ya Kunduchi Mtongani baada ya akina mama kuamua kulala barabarani kushinikiza kuwekwa kwa matuta katika barabara hiyo.

Wakina mama hao walilazimika kufanya hivyo kufuatia kugongwa kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtakuja, Omari Said (9) ikiwa ni mfululizo wa matukio kama hayo kwa kipindi kifupi.

Kitendo hicho kilipelekea askari kuwatawanya kwa kutumia mabomu ya machozi ambapo katika kupiga mabomu hayo mengine matatu yalipigwa nyumbani kwa mfiwa.
Akizungumza na Nipashe baba mzazi wa marehemu, Said Majinja, alisema kitendo cha askari kuvamia msiba na kupiga mabomu kimewasikitisha sana na kimewaongezea majonzi.

Alisema mabomu hayo yamemjeruhi shangazi wa marehemu,Allia Said ambaye bomu limempiga mguu wa kulia na kumpasua kiasi cha kupelekwa hospitali.

Majeruhi mwingine Athumani Nyangazeni alipigwa bomu sehemu ya kichwani na kukimbizwa hospitali wakati wengine walikimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala.

Wakazi wa eneo hilo wamelalamikia kitendo cha askari kupiga mabomu katika makazi ya watu huku wakijua wazi kuwa wapo watoto wadogo na watu wazee.

SOURCE: Nipashe
 
Morani75 & Fundi Mchundo.....nisaidieni yafuatayo.....

1.Hivi barabara zetu zinafanyiwa safety audits?
2.Nini sifa za Highway

Ogah,
Swali lako la kwanza sintakujibu maana miye nipo Sikonge na huku hata Tabora mjini kwenyewe barabara za lami unaweza kuzihesabu kwa kwa vidole vya mono mmoja.
kwanza nianze na MATUTA. Mie ni MPINZANI mkubwa sana wa MATUTA kwenye HIGHWAY. Kama mtu wa fani hii NALAANI sana kuweka MATUTA kwenye high way, ila kwenye MIJI yote naweza kusuport kwa kiasi fulani hasa sehemu za makazi ya watu sehemu za speed ya 20-30km/hr. Kama mtu wa fani hii nasema Express Road, Highway roads haziwezi kuwekewa MATUTA.

Sifa kubwa ya HIGHWAY kwa nchi nyingi ni kuwa:-
-Zinakuwa na fance.
-Speed yake inakuwa ni around 120/130km/hr na hawaruhusu binadamu kupita juu ya hizi barabara au Matrekta. Lane zake zina upana wa mita 3,50 hadi 3,75m. Kwa hiyo kama kuna lane 4, inakuwa 7x2. Kuna kistreep cha ndani ambacho kinakuwa na 0.5m na kwa nje sehemu ya kusimama kwa dharura inakuwa na 3.m. Ukichukulia na msitari unaogawanya ambao tuseme uwe na mita 3, highyway utaona inakuwa na kama mita 25 upana. Hapo ukiongeza na yale lile eneo liitwalo la Roads Right, highway inaweza kuwa na upana wa mita 120.
-Alivyosema Morani ni kweli kuwa Highywa inaunganisha miji mikubwa. Sasa ni ukiona hata watu wa Kimara wanatumia hiyo barabara ujuwe hiyo si HIGHWAY. Hiyo sana sana ni National Road tu na kwa maana hiyo Class yake iko chini sana.
-Highyway inatakiwa zipite mbali na miji ili kuzuia hiki kizaazaa cha ajali. Mkipata balaa highway ikapita kwenye kijiji chenu basi kijiji huwa kinakuwa kama kimepata mpaka.Inabidi wahandisi wajenge kitukama VIADUCT (madaraja) ambayo watu, magari, wanyama nk watapita kutoka upande mmoja kwenda mwingine ingawa kisheria ni HIGHWAY siku zote lazime iwe chini na barabara la Low class zinakuwa juu.
-Kitendo cha Wahandisi kupitishia hii waiitayo HIGHWAY kwenye vijiji ni makosa ya hali ya juu. Inabidi ipite msituni tu kama ilivyo Train na sana sana karibu na miji na hapo barabara ndogo zinzwekwa kwenda kwenye hiyo miji.
-Ukishapitisha barabara ndani ya vijiji hiyo haiwi HIGHWAY tena. Inabidi kuweka vitu vingi sana kuzuia speed. Na si MATUTA tu husaidia kupunguza speed. Unaweza weka hata surface course ya mawemawe na hivyo kila asogeaye pale hupunguza speed ingawa si sawa na kujibamiza kwenye tuta.
-Waweke KAMERA zinazopiga picha magari yanayopita kwa speed kali. Hizi zinaweza wekwa kila sehemu palipo na hizi alama za kupunguza speed.
-POLISI wawekwe wengi hasa wa kiraia na kuwe na tuseme gari lenye kamera na kila RAIA akivuka sehemu ya barabara pasipo na alama za kuvuka, akamatwe na hapo alipishwe sh. 10,000 au akafanye kazi za kusafisha mji.
Ila hii sina uhakika nayo maana Kuanzia juu hadi Chini, tanzania ni Curupt. Ila kama juu wangelikuwa makini, YES WE CAN.
 
Morani,
Salama Mkuu wangu? Naona hili swala linarudi tena. Kweli kuna umuhimu wa Traffic Engineer wengi sana pale Tanzania. Haya maswala yanapoingiliwa na watu wengine inakuwa kizaa zaa. Inanikumbusha swala la Parking kwa nchi zilizoendelea. Wengi hutaka kuja na magari yao kazini. Kujenga parking mijin siku zote hai-pay. Solution inakuwa mfano kufanya lane moja wakati wa asubuhi inatumiwa na mabasi tu. Waholanzi wanajenga Tram-lines na kuweka lami kwenye reli kwa hiyo mabasi na Matram yanakwenda kwenye barabara moja. Sasa hii husababisha watu wengi kuacha kutumia magari yao na kutumia Metro, Trams na mabasi. Miji mingine hutumia hata ADA ya kulipa ili uiingie City Center. Kama sikosei London na Berlin wamefanya hivyo na kwa kumbukumbu yangu ni kuwa Berlin wamepiga kabisa marufuku New Comers kuingia na magari yao Kwenye RING A.
Wahandisi wa Ujenzi na hasa BARABARA wakati mwingine inabidi wawe RADICAL na kutoa solution ambazo zinaweza zisipokelewe na wananchi ila zikawa na manufaa baadaye na usalama. Hapa itategemea na ushirikiano wa Serikali na hasa vyombo vya dola. Utaona kuwa asubuhi watu wengi hujaribu kutumia ile lane la BUS ila wakiona POLISI basi huanza kuikimbia. Sasa kama kuna Kamera na Polisi na FAINI kali, kila kitu kitawezekana. Ni UTAMADUNI mpya mbao tutake tusitake lazima tuanze kujifunza. Tukianza kukimbilia solution za shortcut, hatutafika mbali. Itakuwa yale ya Wakuu wa Wilaya Tabora wanasema ngoma ya Chagulaga inasababisha mimba kwa wanafunzi wa secondary ila MADISCO hayasababishi. Watu waanze kuwajibika. Kila mtu na fani yake. Haya mambo ya kubeba watu eti kwa sababu ni Ndugu au rafiki, ndiyo yanayotufikisha hapa. Kama BOSS wa TANROAD anaruhusu UOZO kama huu basi au yeye awajibike au hao wanaodesign hizi barabara (kuchora) ndiyo wawajibike.
Kweli, inabidi TUBADILIKE. Bila ya hivyo WATAKUFA sana hata kama matuta yatawekwa.
 
Phil.

Unachosema ni kweli kabisa. Naona kila mtu amechukua madaraka ya kuweka matuta barabarani ovyo ovyo tu. Si serikali si watu binafsi, Utakuta tuta kubwa limeweka kiasi kwamba gari ndogo ikipitisha tairi la mbele tu, gari inakaa juu ya tuta na kuwa kama mizani vile. Mfano ni matuta ya pale Chalinze. Siku za nyuma, nilienda Morogoro na kwa kweli ilibidi nisimame pale na kupiga picha. Nitajaribu kuziweka hapa. Hii ni kero kubwa mno kwa wenye magari. Tatizo la wanasiana wetu ni kukurupuka na maamuzi ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kujua faida na hasara zitokanazo na maamuzi hayo.
__________________


NA KWA USEMI HUU KUMBUKA KUPIGA PICHA ZILE MAITI ZILIZOKUWA ZINATAPAKAA PALE KIMARA BUCHA ,,KWA SABABU YA KUTOKUWA NA HAYA MATUTA SI KUPIGA PICHA MATUTA TU ,,WEKA NA DAMU ZA WALIOKUFA HUMU UJUE UNACHOONGEA NI PUMBA AU NJEGERE!!!11
 
Nakubaliana na wewe My Tanzania kuwa kabla ya matuta ajali zilikuwa nyingi sana! Hata wakati wa Magufuli aliombwa aweke matuta na akajibu "Ovyo"! Hali hii ikafanya eneo la Ubungo-Kibaha kuwa eneo lenye ajali nyingi kuliko popote TZ. Mimi naishi Kimara Suca, kwa eneo hili, hardly 1 km, ajali zilikuwa ktk average ya 4 kwa wiki hadi washirikina wakadai kuwa "Hapa kuna Jini", kumbe jini mwenyewe ni poor planning of the road. Barabara ya Chalinze-Morogoro ina bumps kila Mahali inavyopasa na ajali zimepungua sio kama zamani. Nani asiyekumbuka ajali za Chalinze-Morogoro, hasa ile ya Mikese iliyoua basi zima kasoro mmoja? . Ndivyo hivyo Morogoro RD Ubungo-Kibaha, ajali zimepungua. Big up JK.
 
Wiki kadhaa baada ya TANROADS kutekeleza amri ya rais aliyoitoa alipokuwa akizindua barabara huko shinyanga ..ya kutaka barabara kama ya morogoro road kuanzia chalinze kuwekewa matuta

TANROADS SHAME ON YOU! KAMA NYIE NI WATAALAM MLIOKWENDA SHULE MTAWEZAJE KUWEKA MATUTA YA AINA HIYO KATIKA BARABARA ZETU? NINA HAKIKA WENGI WENU MMETEMBELEA AU KUSOMA NCHI ZA NJE, MLISHAONA MATUTA KAMA HAYO POPOTE PALE DUNIANI? THIS PROVES THAT YOUR ACADEMIC PERFOMANCE IN SCHOOL WAS BELOW AVARAGE.
 
Wiki kadhaa baada ya TANROADS kutekeleza amri ya rais aliyoitoa alipokuwa akizindua barabara huko shinyanga ..ya kutaka barabara kama ya morogoro road kuanzia chalinze kuwekewa matuta

TANROADS SHAME ON YOU! KAMA NYIE NI WATAALAM MLIOKWENDA SHULE MTAWEZAJE KUWEKA MATUTA YA AINA HIYO KATIKA BARABARA ZETU? NINA HAKIKA WENGI WENU MMETEMBELEA AU KUSOMA NCHI ZA NJE, MLISHAONA MATUTA KAMA HAYO POPOTE PALE DUNIANI? THIS PROVES THAT YOUR ACADEMIC PERFOMANCE IN SCHOOL WAS BELOW AVARAGE.

Paulimasao,
Polepole baba. Duniani kote hakuna field ya Uhandisi iliyo karibu na wana SIASA kama hii ya ujenzi. Nafikiri kutokana na gharama za ujenzi kuwa kubwa, WANASIASA kama walivyo fisi wakiona mfupa, hukimbilia huko ili na wao wafaidi kidogo. Huko unaweza kudanganya wee na kuprove inakuwa ngumu sana. Unaweza kukuta hela ya kuweka matuta ndiyo zinakusanywa hela ya uchaguzi.
Ulisikia AMRI ya Mamvi kuwa lane tatu zitumike kuingiza magari mjini wakati wa asubuhi na jioni iwe kinyume. Sasa Lowassa hajui kuwa msongamano wa barabarani husababishwa kwenye Makutano ya barabara. Unapobadilisha mpangilio wa magari kwenye makutano bila ya kubadilisha PROGRAM ya Traffic lights unakuwa unaongeza tatizo badala ya kupunguza. Badala ya kuwaomba wataalamu wakae na kulishughulikia hilo swala na wafanye maamuzi haraka sana, yeye Lowassa tena mtu aliyesomea USANII bila hata mwanga wa uhandisi wa Ujenzi, anaingilia na kusema "Ulaya wanafanya hivi, na sisi tufanye". Sidhani kama hawa jamaa NA UHANDISI walikubali kufanya hivyo. Kama walifanya kwa mawazo yao, basi sidhani kama kweli kuna Wahandisi wa Ujenzi wa BARABARA. Sanasana ni wahandisi wa Ujenzi IN GENERAL.
Kumbuka kitu kimoja hapa kinaweza kuwa kilifanyika. Tuseme Morani kaamua kuchora HIGHWAY kweli kama wanavyoisema Tanzania. Anaamua kuweka barabara na kuweka WIGO kuzuia watu na wanyama kuingia kwenye Highway. Anaipitisha nje ya miji Mikubwa na midogo ili kuondoa ajali. Hapa inakuwa kama RELI maana watu hawataona kama SERIKALI inafanya kitu. Ukiwawekea watu HIGHWAY mlangoni, watakufurahia siku ya kukata Utepe na kukubeba juu juu ingawa ndiyo kesho yake wanaanza kuzika watoto wao.
WATANZANIA tuanze kupata fundisho kuwa BADALA ya KULALA barabarani kudai MATUTA yawekwe, basi tuwe kama nchi zilizoendelea ambazo wakiona HIGHWAY inajengwa kupitia CITY CENTER yao, huanza kuandamana na KUPINGA VIKALI ujenzi huo. Sisi tunashangilia kama kumchagua Msanii au CCM na mambo yakiwa mabaya tunaanza kulialia. Ehh, si tulimchagua kwa asilia ngapi sijui? Nafikiri VYAMA vya UPINZANI hapa inabidi wawe wanasaidia wananchi kwa kuwapa Mwanga wa mambo kama haya. Wakikataa na mambo yakiharibika wanakuwa wameongeza POINT kwa kusema SISI tulijua na tuliwaambia, nyie mkaifuata CCM na sasa mpo mlipo. Next time mtuamini sisi.
 
Phil.

Unachosema ni kweli kabisa. Naona kila mtu amechukua madaraka ya kuweka matuta barabarani ovyo ovyo tu. Si serikali si watu binafsi, Utakuta tuta kubwa limeweka kiasi kwamba gari ndogo ikipitisha tairi la mbele tu, gari inakaa juu ya tuta na kuwa kama mizani vile. Mfano ni matuta ya pale Chalinze. Siku za nyuma, nilienda Morogoro na kwa kweli ilibidi nisimame pale na kupiga picha. Nitajaribu kuziweka hapa. Hii ni kero kubwa mno kwa wenye magari. Tatizo la wanasiana wetu ni kukurupuka na maamuzi ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kujua faida na hasara zitokanazo na maamuzi hayo.

Mama Mia,
Naomba kama ukishapiga picha basi niwekee kwenye EMAIL yangu ili na mimi nione haya matuta ambayo nasikia hata akija Yelena Isinbayeva itabidi mwenye jasho limtoke kuyaruka maana akianguka upande wa pili atakuta hamna godoro la kuangukia. Kama utaweza nitumia kwa EMAIL basi nasema ASANTE IN ADVANCE. Tuma kwenye SIZYAS@yahoo.co.uk
 
Kwa wanaotumia Barabara ya Morogoro pale Mbezi Mwisho, nimeshangaa na kushtushwa mno kwani pale kituoni upande wa kushoto kamaunaelekea Kibaha pamewekwa concrete blocks kubwa hivyo kufanya kituo kile kisitumike tena. Kinachoniumiza kichwa ni jinsi msongamano wa magari ulivyomkubwa pale kituoni Mbezi Mwisho kwani wakati mwingine magari yanayoingia kituo cha daladala upande wa pili na yale yanayoingia njia ya Makabe inakuwa ni vigumu sana kwani lazima wasubiri yale yanayoelekea mjini yapite hivyo foleni inakuwa kubwa sana na usalama unakuwa ni mdogo kwani hata ushushaji wa abiria kwa magari yanayoelekea Kibamba na Kibaha umekuwa ni wa shida sana.

Je walioweka hizo bocks wana maana gani?, Umuhimu wa hicho kituo umekwisha?, Wahusika hawaoni msongamano wa pale kituoni na ufinyu wa barabara yenyewe kuwa ni tatizo ambalo linahitaji kutatuliwa haraka kabla ya maafa ya ajali kutokea?
 
Jambo la kujiuliza je wataalam wa barabara walitoa tahadhari kwa wanasiasa madhara ya kuweka matuta Morogoro Rd? Inawezekana nao hawakuwajibika kisawasawa katika kutoa ushauri kwa wakati muafaka. Wanajenga kumfurahisha mkubwa bila kujali nini kitatokea baadae. Zaidi ya hayo matuta yangepakwa rangi nyeupe maan adha nyingine ni kuwa kama dereva hukuwa mwangalifu unaweza kuleta ajali mara nyingi zaidi kwani hayaonekani vizuri. Ni vyema utafiti wa kina ufanyike kabla ya kukurupuka kufanya madudu.
 
Back
Top Bottom