Matuta barabarani: Wakazi watumiao Morogoro road walia

Jamani mngekuwa mmefiwa na ndugu zenu kwa kugongwa na magari wanao ishi kando kando ya barabara hiyo mngalikuwa mnashukuru sana tiba hiyo mbadala ya matuta ili kupunguza mwendo kasi wa magari.....
Binafsi nikiwa kama mwenyeji wa KImara nawapongeza sana TANROAD kwa kufanya hivyo kwani sasa vifo vitapungua....Ilikuwa haipiti wiki mtu hajapoteza maisha kwa ajari kwa kugongwa kutokana na mwendo kasi wa madereva........Jiulize mwenyewe kwanini ajari nyingi zinatokea katika barabara hii???
Naona ni sababu ya mwendo kasi nenda pale Manzese ilikuwa lazima kila siku mtu agongwe licha ya kuwekwa daraja lakini saizi vifo vimepungua baada ya kuweka matuta na uzio ule....
 
Jamani mngekuwa mmefiwa na ndugu zenu kwa kugongwa na magari wanao ishi kando kando ya barabara hiyo mngalikuwa mnashukuru sana tiba hiyo mbadala ya matuta ili kupunguza mwendo kasi wa magari.....
Binafsi nikiwa kama mwenyeji wa KImara nawapongeza sana TANROAD kwa kufanya hivyo kwani sasa vifo vitapungua....Ilikuwa haipiti wiki mtu hajapoteza maisha kwa ajari kwa kugongwa kutokana na mwendo kasi wa madereva........Jiulize mwenyewe kwanini ajari nyingi zinatokea katika barabara hii???
Naona ni sababu ya mwendo kasi nenda pale Manzese ilikuwa lazima kila siku mtu agongwe licha ya kuwekwa daraja lakini saizi vifo vimepungua baada ya kuweka matuta na uzio ule....

unaonaje kuhusu watu watakaoendelea kuumia na kufa kwenye ajali za magari yanayogongana kutokana na msongamano wa matuta.....au yale yanayopinduka usiku wa manane kwa kukosa alama za kuonekana..

why guys dont we come with immediate compromise to suit both pedestrians and motor drivers....[pasengers]
 
Utawala wa rushwa katika jeshi la polisi, pamoja sheria dhaifu ni mojawapo ya mambo yanayosababisha madereva kuendesha magari bila uangalifu.

Jeshi linalo ongozwa kwa maadili ya rushwa, huwa linajipangia taratibu za ajabu katika kukabiliana na uhalifu uliopo barabarani, likipata baraka za viongozi wa kitaifa.

Hatua ya kwanza ni polisi wenyewe kulala barabarani, kwa kuweka matuta kama yanavyojulika kama "sleeping policeman" ukianzia ubungo unaanza kumkanyaka Mwema, Kimara unamkanyaga Kombe n.k.

Kwa sasa kila tuta litapewa na jina la kiongozi wa jeshi la polisi kutoka Dar hadi Morogoro.
 
MANZESEE KUNA DARAJA NA WATU WANAGONGWA, KAWAWA ROAD 'SOKO LA MACHINGA' WANAWEKA DARAJA NA WATU WATAGONGWA VILE VILE.

kwa solution ya kitanzania, kilicho fanyika ni best option, ukitaka kuwahi toka mapema.
 
Heshima mbele wakuu. Jamani hivi:

Tatizo wataalamu wetu nao wanachukulia kila kitu anachosema rais kuwa ni halali. sheria yetu ya barabara hairuhusu kuweka matuta kwenye highway. kwa hiyo hata rais akisema, bado ni ukiukwaji wa sheria tu. nadhani hapa walipaswa kufikiria ushauri wa rais na kufanya kitu ambacho ni convinient kutekeleza aguizo la rais na kuwarahisishia watumiaji wa barabara maisha

Mkuu MN, unajua kwa nini matuta yamekwekwa, sababu wahusika walikuwa hawana alternative solution ya kumwambia Mhe Raisi against matuta.. Hili sio kosa la Raisi ni kosa lao kwa kutokuwa na alternative!! Basi kama hakuna alternative then wangemwambia kitaaluma na sio kuweka kilicho sicho (kama kweli matuta ni mabaya kisais hicho against loss of lives). MM kusema Raisi ana kosa narudia tena na kumuonea Mkuu kwa kosa la wataaluma ambao tunao in plenty!!

kwa maoni yangu ni vitu viwili tu wanachoweza kufanya ni kujenga subway au flayover kama la pale manzese,kila polipo na kituo cha basi.
kisha sehemu zilizobakia za barabara wajenge uzio kuzuia watu kukatisha barabara ovyo.

Mkuu KK, huo ushauri wako ni mzuri kwelikweli lakini ukiangalia Dar - Mlandizi - Chalinze Road (especially Dar - Mlandizi) kuna kijiji karibu throughout the road. Pia ukiangalia kwa ukaribu utaona kuwa kila kwenye vituo (vituo vyote/vingi vimejengwa pacha, to and from adjacently) kuna alama ya kwenda 50kmph na maeneo ya shule as low as 30kmph, lakini madereva pretends nothing exists, solution, weka tuta pinduka au punguza mwendo..... Pia ushauri wako kwa pesa zipi Mkuu, hii ni Bongo tunaongelea na sio ahera!!

unaonaje kuhusu watu watakaoendelea kuumia na kufa kwenye ajali za magari yanayogongana kutokana na msongamano wa matuta.....au yale yanayopinduka usiku wa manane kwa kukosa alama za kuonekana..

why guys dont we come with immediate compromise to suit both pedestrians and motor drivers....[pasengers]

Mkuu PM, magari kugongana kutokana na msongamano wa matuta, Mkuu umesahau sheria za barabarani au ni jazba?? Kuna ile inayosema "Keep a safe following distance" Hilo la magari kupinduka kwa kukosa alama zinazoonekana sio kosa la matuta, ni kosa la maintenance agency (na wizi wa alama za barabarani na kugongwa na madereva husika) kushindwa kumaintain standard signs - sio kosa la matuta kuwepo bali ni alama!!

On your second part ya compromise solution to suit both hapo tunaweza ongea lungha ya aina moja. Ndicho tulichosema kwenye ile thread ulianzisha ya Mh Raisi kuingilia majukumu ya watalaam. Kwenye post yangu ya kwanza in this thread nilikuwekea kwa ukumbusho. Tuliongelea mengi yakiwemo safety audit (kwakuanzia na kutafuta blind/danger spots along our roads etc, kisha tutafte best solution considering all users requirement, costs etc)

MANZESEE KUNA DARAJA NA WATU WANAGONGWA, KAWAWA ROAD 'SOKO LA MACHINGA' WANAWEKA DARAJA NA WATU WATAGONGWA VILE VILE.

kwa solution ya kitanzania, kilicho fanyika ni best option, ukitaka kuwahi toka mapema.

Mkuu watu, asante kwa hilo..... Solution za nchi/sehemu nyingine may not necessarilly be the best to our scenario and mind sets!!!

Mungu Ibariki JF, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu tubariki waTanzania!!!
 
kwa maoni yangu ni vitu viwili tu wanachoweza kufanya ni kujenga subway au flayover kama la pale manzese,kila polipo na kituo cha basi.
kisha sehemu zilizobakia za barabara wajenge uzio kuzuia watu kukatisha barabara ovyo.


Tatizo letu lingine ni utawala wa sheria. Hata pale Manzese wapita njia wengi hawapitii kwenye fly over. Paliwekwa fensi ikavunjwa. Paongezwa na njia nyingine ya zebra pamoja na matuta. Kwa kifupi, viongozi wa Tanzania ni akisi ya watanzania!. Kuna haja pia ya kugeuza mindset. Suala la matuta ubungo hata wengine tulijitumbukiza humo. Kuna kilio cha wananchi wa pande zote mbili, lakini wengi hawatakafari chanzo

JJ
 
Kitu kingine kinachonishangaza kwenye matuta ni kugeuzwa kuwa sehemu ya vituo vya kuombea lifti.. Utakuta wanavijiji wamesimama mita chache sana toka kwenye matuta hayo wakiomba msaada wa usafiri...

Incase inatokea dhalura katika gari linalosimamishwa maisha yao yanaweza kuwepo hatarini. Pamoja na nia nzuri ya kuwekwa kwa matuta hayo, naona bado wananchi wanapenda kuwa karibu na barabara...
 
Last edited:
Tatizo letu lingine ni utawala wa sheria. Hata pale Manzese wapita njia wengi hawapitii kwenye fly over. Paliwekwa fensi ikavunjwa. Paongezwa na njia nyingine ya zebra pamoja na matuta. Kwa kifupi, viongozi wa Tanzania ni akisi ya watanzania!. Kuna haja pia ya kugeuza mindset. Suala la matuta ubungo hata wengine tulijitumbukiza humo. Kuna kilio cha wananchi wa pande zote mbili, lakini wengi hawatakafari chanzo

JJ

Mkuu JM, asante kwa kuweka hilo... Tatizo ni kwamba pamoja na kwamba viongozi nasi wananchi pia tunatabia ya kutibu symptoms na kuacha chanzo kinaendelea kutuathiri ndilo lilitufikisha hapa. Tukirudi nyuma, je Raisi ailikuwa na haja gani kuamuru matuta yawekwe kama sisi wahusika wa taaluma yenyewe (TANROADS, MoW, PORALG etc) tungekuwa tumeshlifanyia kazi?? Au ndi yale ya kusema "Usifanye mpaka uambiwe fanya na wakuu?".... Inasikitisha sana pale tunapolalamikia uamuzi wa kufanya kile tulichozea bila ya kufumbua macho na kuona ni kwa nini tumefikia hapa tulipo!!!

Mungu Ibariki Tanznia na watu wake!!
 
Kitu kingine kinachonishangaza kwenye matuta ni kugeuzwa kuwa sehemu ya vituo vya kuombea lifti.. Utakuta wanavijiji wamesimama mita chache sana toka kwenye matuta hayo wakiomba msaada wa usafiri...

Incase inatokea dhalura katika gari linalosimamishwa maisha yao yanaweza kuwepo hatarini. Pamoja na nia nzuri ya kuwekwa kwa matuta hayo, naona bado wananchi wanapenda kuwa karibu na barabara...

Mkuu Kibunango, nilishindwa kujizuia kucheka manake ukicheki namna watu wanavyojituma kutumia vyanzo vya magari kupunguza spidi kuomba lifti, na wakati mwingine kufanya biashara atiiii.... Unakumbuka ule usemi ulioanzia kwenye daladala, "Msaada kwenye tuta?"

Yapo mengi tu, pita kwenye mabarabara makubwa hapa nyumbani kwenye maeneo ya miji mida ya jioni utakuta watu wanaleta maji na ndoo zao kisha wanatumia barabara/lami kama jiwe la kujisugulia na maisha yanaenda.... Wacha wale wanaogeuza kingo za barabara kama vijiwe vya kupiga soga.... Ni mengi lakini Mkuu Nyani M alisema, Ndivyo..... (I'm still in denial though, amazing!!)
 
Tatizo la ajali pia linachangiwa na magari mabovu yaliyochooka hasa MALORI. Polisi wanayaona na kuyaachia tu. anagalia jioni barabara ya Sam nujoma kuelekea bandarini (zamani Port access) malori kama sita mpaka kumi yanaharibika kila siku.

Haya malori ni chanzo cha ajali maana usiku mengi hayana reflectors...

Na hata yanayotembea hayana BREKI za kueleweka!
 
Jamani hili la matuta halijakaa vizuri hata kidogo

Ni suala tu la kufuata sheria za usalama barabarani!

utakuta ntu anavuka, kana kwamba yupo kijijini, sehemu yenye taa za kuongozea waenda kwa miguu na magari mtu anavuka taa nyekundu! sembuse kwenye sehemu ambazo hazina taa

na kuna usemi kuwa dar watu hawaogopi magari wanaogopa mvua na hii ndo inatumaliza wengi

kusema kweli mi nimekata 'stadi' kwanye haya haya matuta....

stop over penyewe ambapo ni chinja chinja hapana matuta.....sasa pia kuna wenda wazimu huwa 'wanayaparaza' tu mwendo ni ule ule

hizi solution zingine ni matatizo zaidi kuliko faida!
 
Morani75 & Fundi Mchundo.....nisaidieni yafuatayo.....

1.Hivi barabara zetu zinafanyiwa safety audits?
2.Nini sifa za Highway
 
Suala la kuwa na fly-overs ni au under-pass ni muhimu sana kwenye highway kama Morogoro Road hilo halina ubishi. Matuta ni kama kujaribu kuziba pakacha linalovuja. Sambamba na hatua hizi ujengwe uzio along barabara ili kuwa force watu wapite katika vivuko husika.

Otherwise tutakuwa napoteza watu kila siku hususan walevi kwani ndio asilimia kubwa ya wanaogongwa Morogoro road
 
Morani75 & Fundi Mchundo.....nisaidieni yafuatayo.....

1.Hivi barabara zetu zinafanyiwa safety audits?
2.Nini sifa za Highway

Mkuu Ogah, my two cents are:
1. Safety Audits in Tanzania: Kwa uafahamu wangu kwa kweli hili linatakiwa liwe linafanywa kila mwaka lakini kwa muda huu tumeliweka zaidi kwenye wakati wa design phase especially in upgrading projects (mfano ni kama kwenye kukuza barabara kutoka kwenye kiwango cha changarawe kwenda lami, au pale panapohitajika vitu kama traffic lights/round abouts etc). Hii tatizo lake ni short term and it is project related rather than overall applicability/situation in/through the project husika!
Harakaharaka nafahamu kwamba kwa barabara ambayo ni tofauti na zile zinazotegemewa kujengwa ni ile ya Chalinze-Segera-Tanga ambapo kuna wakati ule miaka ya 2003/4 kama sikosei DANIDA walitoa pesa kwa ajili ya kufanya safety audit iliyopelekea kufanyika kwa safety improvement ya barabara lile. Hii ndio kazi inayoonekana pale Chalinze Mzee (kupanuliwa kwa barabaraba), additional shoulder kwenye maeneo ya vijijini nk. Kwa upande wa TANROADS, RFB, MoW, PORALG, Police Force, kwa kweli sijalisikia (at least naweza kusema sijawahi kuona records husika)

2. Sifa za highway: Mkuu, hili linategemea upande umesimama. lakini kwa definition ya general kama wanavyosema kule kwenye Wikipedia wanasema hivi "A highway is a main road intended for travel by the public between important destinations, such as cities and towns.". from Highway - Wikipedia, the free encyclopedia

Ukweli ni kwamba kwa hapa nyumbani (general understanding) ni kwamba Highway (National Highways) ni zile barakbara kuu zote zinazounganisha makao makuu ya mikoa/nchi jirani (mfano ni TanZam Highway: Dar-CHZ-MG-IRA-MBY-TDM; CHZ-SGR-TAN; SGR-MSA-ARS-NMG; na nyingine nyingi). Hapa kuna viwango tumewekewa nijuavyo mimi kwa experience yangu ya kufanya kazi hapa nyumbani vimo safety standard (aina ya matuta kwenye miji), uzito wa magari yanayoruhusiwa kupita (hii lazima iwe as per SAATC due to regionalization), Upana wa madaraja ya kawaida, clearance ya madaraja ya juu (overbridges), speed limits and signage among other things.
Hapa sasa tusichanganye na vitu kama "Freeways" ambazo kwa hapa kwetu hatunazo!

Mkuu Ogah, nadhani nimejaribu kuweka majibu kama ulivyohitaji to the best of my knowledge. FM naye ataleta maneno, kwako FM!!
 
Matuta ni muhimu kwasasa katika barabara ile... wanaosema kuwa matuta yanarudisha nyuma maendeleo, au yanasababisha foleni ni kwakuwa si wakazi wa maeneo husika. ni watumiaji wa msimu wa barabara ile. kwa wasio fahamu, barabara ya Moro kuanzia Ubungo hadi Mbezi ilikuwa ni machinjio yasiyo na kibali kwa binadamu na mali zao. kila siku ya muumba tulikuwa tukishuhidia watoto, watu wazima na watu wenye magari yanayoingia barabara hiyo wakipata adha kubwa ikiwa ni pamoja na kupoteza maisha.

Mimi binafsi nimeona hili limechelewa mno kushughulikiwa! very long overdue!! inawezekana kweli limefanyika kienyeji sana bila kuweka alama za onyo kwa madereva n.k. kitu ambacho kinaweza kikaboreshwa baada ya muda mchache! Suala la foleni asubuhi katika barabara hii lilikuwepo hata kabla ya matuta kuwepo, hususani maeneo kuanzia kimara baruti hadi Ubungo nyakati za asubuhi; na sasa hali ni hiyohiyo. ila sijawahi kushuhudia ajali mbaya kwa kipindi hiki ukilinganisha na ajali mbaya mbaya mno wakati wa nyuma hasa maeneo ya ubungo maji, na kimara kona. Kuna siku za nyuma, Lori moja lililobeba ng'ombe, lilipata ajali maeneo ya Kimara kona majira ya saa kumi na alfajiri kwa sababu ya mwendo kasi. N'gombe zaidi ya kumi na tano walikufa pamoja na utingo wawili. kesho yake zile nyama za ng'ombe vibudu zilitapakaa katika mabucha ya nyama mjini dar es salaam! Nyama ile ilichanganyika na damu za binadamu waliokufa katika ajali ile.

Tunapowasilisha mada za kupinga mambo mengine ambayo ni suluhisho mbadala....tuangalie upande mwingine wa shilingi! Hata kule shule tuliposoma DS tuliambiwa kila kitu kina Prons and Cons. Matuta haya faida yake ni kubwa zaidi! hasa kwa kuokoa roho za wadanganyika wanaoishi kandokando ya barabara hii.
 
Sio wakati wote suluhisho la tatizo likubalike kwa watu wote.

Ni kweli flyover zingefaa katika barabara ya Morogoro. Lakini kutokana na uhalisia wa mambo, watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwenye barabara hii. Kwa hiyo uwekaji wa matuta kwa sasa(kutokana na hali halisi) ni sawa kabisa mpaka hapo tutakapokuwa na flyovers.

Rais ameagiza uwekaji wa matuta, lakini hakuagiza jinsi ya uwekwaji huo wa matuta. Wahandisi wa barabara ndio walitakiwa kujua ni umbali kiasi gani unafaa kati ya tuta na tuta, kuhakikisha optimal vehicle speed, na kuweka road sign.

Tukumbuke solutions nyingi zinaendana na cultures pia. Kwa sasa nchi yetu sheria hazifatwi; madereva na waenda kwa miguu. Kwenye zebra crossing dereva hapunguzi mwendo na pale ambapo mtu hatakiwi kuvuka, yeye anavuka, thinking kwamba dereva anamuona na hivyo atasimama.

Kwenye barabara hii pia, imekuwa ni tabia kwa magari makubwa kwenda kwa mwendo kasi na huku daladala kuwa "zinachomokea", kitu ambacho kimekuwa chanzo kikubwa cha ajali.

Ukiangalia vituo vya daladala kutoka Mbezi/Kimara kuja Ubungo, ni vichache sana ambavyo bado vina sheds, kwa sababu kila siku zinagongwa.

Sasa inafikia wakati tujiulize, kipi bora, slow speed/foleni au kupoteza ndugu na jamaa zetu ?
 
Suala la kuwa na fly-overs ni au under-pass ni muhimu sana kwenye highway kama Morogoro Road hilo halina ubishi. Matuta ni kama kujaribu kuziba pakacha linalovuja. Sambamba na hatua hizi ujengwe uzio along barabara ili kuwa force watu wapite katika vivuko husika.

Otherwise tutakuwa napoteza watu kila siku hususan walevi kwani ndio asilimia kubwa ya wanaogongwa Morogoro road

masatu wellspoken..flyovers na underpuss...makandarasi tunaomba mnapochora plan za barabara mpya au ambazo hazijakamilika ..zingatieni hili..najua flyover ni ghali lakini sio under pass...

kwa mfano kuna barabara bado Zinajengwa kama mandela rd..kuna ubaya gani kutekeleza hilo hasa maeneo ya mabibo hostel na benjamini mkapa export zone ...haili eneo lina high pedestrian traffic na itaongezeka pale EPZ itakapoanza kazi.....saa ukiwauliza watu wa TANROAD kama walizingatia hilo hapo mabibo,buguruni ,temeke sokota..tazara haya yote ni maeneo chinja chinja kwa pedestrians...utashangaa hawana plan....na barabara ikiisha watakurupuka na shortcut ya matuta......

kuhusu wazo lako la uzio ni zuri lakini wajasiriamali wataiba kwenda kuuza scrapper...si unajua wajasiriamali wasio rasmi wameongezeka wanaiba vifuniko vya sewers hadi mataruma ya treni ...
 
ndugu yangu wa Kimara, hilo unaloliongea kuhusiana na ajali ambazo watu wengi walikuwa wanapoteza maisha yao hapo siku za nyuma si kwamba zitakoma, suala la usalama barabarani ni zaidi ya matuta, matuta yanaharibu barabara pamoja na magari pia husababisha muda mwingi kupotea kwa sababu ya matuta.madereva wa magari wa kwetu hapo Tanzania wanatakiwa wajue kwamba mtembea kwa miguu ni traffic, naye ana haki ya kutumia barabara. madereva wanatakiwa wafuate sheria za barabarani zote.tatizo lililopo nchini kwetu watu hawajali sheria za barabarani. Wanasiasa nao wanatakiwa waendelee na siasa zao kazi za kitaalamu awachie technical personnel, hapo tutayafaidi matunda ya Maengineer wetu wa Tanzania. sasa siasa wao, maengineer wao, wachumi wao hatutafika kwa hilo. kwa sababu uchumi wa nchi ni mdogo na waibaji ni wengi ni vigumu sana kwa nchi kama tanzania kujenga madaraja ya kupita juu na chini kila sehemu. Tunatakiwa tutumie tulichonacho bila kuathiri maisha ya watu na maendeleo ya kiuchumi.
 
^^ Mwakaleli karibu... Barabara ya Uyole hadi Kyela ipo vipi? matuta mengi au hakuna? Pale Kiwira lile soko bado lipo barabarani?
 
Back
Top Bottom