Matunda haya yanaitwaje kwa kiswahili?

GM7

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
492
24
Halo wana JF, nauliza hivi kwa sababu kuna baadhi ya vitu vingine havijulikani kwa majina ya kiswahili. Mfano:
Matunda haya kwa kiswahili yanaitwaje?

Kwa lugha fulani wanayaita mafyulisi, na lugha nyingine wanayaita mapiniges.
Kwa kiswahili je????????
attachment.php

Attachments

• Image009.jpg
Image009.jpg
48.5 KB · Views: 760
Lol... umenifurahisha sana wewe Msafwa wa huko Mbeya!

Haya matunda yanaitwa Matipisi kwa baadhi ya sehemu, zaidi Arusha au Peaches kwa lugha ya Kiingereza!

Nami pia nayapenda sana, ila naboreka kwa sababu yale matunda manene na matamu sana ya jamii hiyo wanayaita "ya kizungu", wakati ya kawaida kama hayo pichani, yanaitwa ya kiswahili!- maneno mbofumbofu!

Kwa lugha fulani wanayaita mafyulisi, na lugha nyingine wanayaita mapiniges.
Kwa kiswahili je????????
attachment.php

Mbeya ndipo mahali wanapoyaita mafyulisi (Wasafwa).
Kwa Lushoto, matunda hayo yanaitwa MAFYOKSI.

Mbeya ndipo mahali wanapoyaita mafyulisi (Wasafwa).
Kwa Lushoto, matunda hayo yanaitwa MAFYOKSI.

Mkuu,

Umenikumbusha mbali sana maana nilikuwa najaribu kukumbuka jina
maana nimesoma Lushoto so tulikuwa tunayachuma tu mitini yalikuwa yamejaa
tele.

Mkuu,

Umenikumbusha mbali sana maana nilikuwa najaribu kukumbuka jina
maana nimesoma Lushoto so tulikuwa tunayachuma tu mitini yalikuwa yamejaa
tele.

Teh teh teh!
Kumbe na ww umesoma kule 'Usoto"? Hongera sana.
Hali ya hewa ya pale inafanana sana na ya Mbeya na Iringa , ndo sababu matunda haya pamoja na pears, matufaa na mengine ya jamii hiyo yanapatikana kwa wingi sana. Kwa kiingereza matunda hayo pichani yanafahamika kama 'Peaches'

Duh!!! katka kutafuta jina mpaka sasa sijaweza kupata jina lake la
kiswahili zaidi ya mimi kuyafahamu kama mafyulisi kwa jina la watu wa mbeya.

Lol... umenifurahisha sana wewe Msafwa wa huko Mbeya!

Haya matunda yanaitwa Matipisi kwa baadhi ya sehemu, zaidi Arusha au Peaches kwa lugha ya Kiingereza!

Nami pia nayapenda sana, ila naboreka kwa sababu yale matunda manene na matamu sana ya jamii hiyo wanayaita "ya kizungu", wakati ya kawaida kama hayo pichani, yanaitwa ya kiswahili!- maneno mbofumbofu!

Mbala uli?

Kwetu Mbeya yanajulikana kama mafyulisi lakini hapa Iringa nimekumbana na jina la mapinigesi.

Back
Top Bottom