Matumizi ya viungo vya vyakula katika kuboresha lishe na afya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MSAMIATI
Kinywaji cha viungo:

Hiki ni kinywaji chochote ambacho kimetengenezwa kwa kuwekwa
viungo. Kinywaji hiki kinaweza kuwa cha moto au cha baridi. Kinywaji
cha baridi kinapotengenezwa, yatumike maji yaliyochemshwa.

Chai:
Hiki ni kinywaji ambacho hutengenezwa kwa kutumia maji ya moto na
majani ya chai. Wakati mwingine sukari na maziwa huongezwa.

Mara nyingine watu wanapotengeneza vinywaji vya viungo huviita
"chai" hata kama havina majani ya chai. Ukweli ni kwamba chai ni yale
majani ya chai. Katika kijitabu hiki vinywaji vya viungo havikuitwa chai.

BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA
ZAKE

Kitunguu saumu (Garlic)

Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi
mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara

nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye
rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo
na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa.

Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi
kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo

katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni.
Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula,

kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani,
maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi.

Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au
kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu
saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita
kwa siku hasa kama vitatumika vibichi .

Tangawizi (Ginger)
Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa
tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa

kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i
inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa.
Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au
kwenye chakula.

Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula,
kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha,
maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia
uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa
matatizo ya mafua au flu.

Iliki (Cardamom)
Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo
hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa
au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au
katika vinywaji.

Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu,
kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji
wa chakula na huongeza hamu ya kula.

Mdalasini (Cinnamon)

Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome ya
mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa

au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini
h u weza kuongezwa kwe n ye chakula au katika
vinywaji vilivyochemshwa au baridi.

Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu,
vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki
huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo

katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha.
Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na
tangawizi kinaweza kutuliza kikohozi.

Giligilani (Coriander)

Giligilani ni aina ya kiungo ambacho
majani na mbegu zake huwez a

kutumika kama kiungo katika mapishi
ya vyakula mbalimbali kama nyama,
supu au mchuzi.

Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na
kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi
ya bakteria na fangasi.

Kotimiri (Parsley)

Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu
zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula.

Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa
tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha.
Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng' e n yo


tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa.
Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya
ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa
katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.

Karafuu (Cloves)

Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo
hiki huweza kutumika peke yake au kwa

kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki
husaidia kuleta hamu ya kula na kubore sha

uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguza
kichefuchefu, kutapika na kuharisha.
Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye
uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa.
 
Binzari (Turmeric/Yellow Root)

Binzari halisi hutokana na mizizi ya mmea wa binzari
manjano ambao hufanana na ule wa tangawizi. Mizizi ya

binzari huweza kukaushwa, kusagwa na kutengeneza
unga wa binzari ya manjano ambao hutumika kama

kiungo cha chakula. Vilevile binzari mbichi
inaweza kutwangwa na kutumika kwenye

Mapishi mbalimbali. Binzari ikitumiwa katika
chakula, hukifanya kuwa na rangi ya njano.

Binzari inaweza kutumika kwenye mapishi ya wali au
vyakula vingine vya nafaka, pia kwe n ye mchuzi au
maharagwe.

Binzari husaidia katika uyeyushwaji wa chakula na pia husaidia mwili
usiharibiwe na kemikali mbaya.
Ni vizuri kuwa waangalifu tunaponunua binzari ile ya unga kwani
wakati mwingine wauzaji huuza binzari ambayo si binzari halisi.

Binzari hii ambayo si halisi hutengenezwa kwa kutumia aina za
unga wa nafaka ambao huchanganywa na rangi ya manjano na
binzari kidogo.

Limau (Lemon)

Limau linaweza kutumika kama kiungo katika
chakula na vinywaji kama chai au vinywaji vingine.
Limau husaidia kuboresha uyeyushwaji hasa wa
protini na mafuta. Limau pia huweza kutuliza vidonda
vya kooni, kikohozi, homa na kuondoa msongo.
8
Binzari nyembamba (Cumin seeds)

Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu

za
giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga
ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali

mfano; supu, mchuzi, wali, n.k.
Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza
maumivu ya tumbo na hata kuharisha.

Mrehani (Basil)

Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa
kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia

kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji
wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. Kwa
vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika
kwa kusukutua.

“Calendula”


Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuia
kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia

kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory
function). Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizi
mbalimbali katika mfumo wa chakula.
‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inawez a

kutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji
wa chakula tumboni.

Pilipili (Cayenne)

“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii
ijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na
nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi
nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na
kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa
na rangi nyekundu.
9

“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza
ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika
au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji
ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi.

Shamari (Fennel)

Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari
nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na
kupunguza gesi tumboni.

Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye
chakula. Mbegu za shamari zinawez a
kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote
cha moto.
Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.

Nanaa (Mint)

Nanaa ni majani ya mnanaa ambayo hutumiwa kama kiungo.
Nanaa husaidia katika kuzuia hali ya mwako wa moto
tumboni, kupunguza kichefuchefu, kuzuia kutapika na

kuharisha. Pia huweza kupunguza maumivu ya tumbo na
mkakamao wa misuli. Vilevile nanaa husaidia katika
uyeyushwaji wa chakula tumboni.

Nanaa iliyooshwa vizuri kwa maji safi na salama inawez a
kutafunwa. Vilevile inaweza kutumika kutengeneza kinywaji cha
moto au kusukutua wakati mtu anapokuwa na vidonda kinywani
 
Binzari nyembamba (Cumin seeds)
Hizi ni mbegu nyembamba ambazo hufanana na mbegu za
giligilani. Mbegu hizi huweza kusagwa na kutengeneza unga
ambao hutumika kama kiungo katika mapishi mbalimbali
mfano; supu, mchuzi, wali, n.k.
Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza
maumivu ya tumbo na hata kuharisha.

Mrehani (Basil)
Mrehani ni aina ya kiungo ambacho huweza kutumika kwa
kuongezwa katika chakula. Kiungo hiki husaidia
kupunguza kichefuchefu na kusaidia uyeyushwaji
wa chakula na kutuliza maumivu ya kichwa. Kwa
vidonda vya kinywani mrehani unaweza kutumika
kwa kusukutua.

“Calendula”
Vikonyo vya maua ya ‘‘calendula’’ vina kemikali inayozuia
kukua kwa vijidudu kama bakteria katika jeraha, ngozi na pia
kupunguza hali ya mwako wa moto (anti-inflammatory
function). Vilevile “c a l e n d u l a” hupunguza maambukizi
mbalimbali katika mfumo wa chakula.
‘‘ C a l e n d u l a’’ inaweza kutumika kutibu vidonda. Vilevile inawez a
kutumiwa kama kinywaji kilichochemshwa ili kuboresha uyeyushwaji
wa chakula tumboni.

Pilipili (Cayenne)
“Cayenne” ni mchanganyiko wa aina za pilipili za jamii
ijulikanayo kama “capsicum”. Pilipili hizi huwa ndefu na
nyembamba, mara nyingi huwa ni kali na zina rangi
nyekundu. Jamii hii ya pilipili huweza kukaushwa na
kusagwa na hivyo kutengeneza unga laini ambao huwa
na rangi nyekundu.
9
“Cayenne” huweza kuongeza hamu ya kula. Pilipili hii inaweza
ikatumika kwa kuongezwa kwenye chakula wakati wa kupika
au wakati wa kula. Pia huweza kuongezwa katika juisi au maji
ya kunywa. Hata hivyo ni vyema pilipili itumiwe kwa kiasi.

Shamari (Fennel)

Shamari ni kiungo ambacho mbegu zake hufanana na zile za binzari
nyembamba. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na
kupunguza gesi tumboni.
Shamari inaweza kutumika kama kiungo kwenye
chakula. Mbegu za shamari zinawez a
kutumika kuandaa chai au kinywaji chochote
cha moto.
Ni vizuri ikitumiwa kwa kiasi.

“Thyme”
‘‘T h y m e’’ inaweza kuzuia maambukizi yanayosababishwa na
bakteria au fangasi. Vilevile kiungo hiki husaidia kupunguza
kikohozi na kulainisha koo. Zaidi ya hayo “thyme” husaidia
ukuaji wa bakteria wazuri wanaosaidia katika uyeyushwaji wa
chakula tumboni. Inaweza kutumika kama kinywaji cha moto au
kusukutua.



Meti (Methi)


Meti ni majani ya mmea uitwao kwa Kiingereza
“Fenugreek”. Kwa Kiswahili inaitwa (Uwatu) Hii ni aina ya kiungo ambacho
huchochea uvunjaji wa kemikali mwilini yaani
umetaboli. Majani ya meti yanaweza kukaushwa
na kutumika kama kiungo au kutumika yakiwa
mabichi. Vilevile mbegu za “Fenugreek” UWATU huweza
kukaushwa, kusagwa na kutumika katika kutengeneza unga wa viungo
yaani “curry powders”. Meti inaweza kutumika kama kiungo katika
vyakula mbalimbali ikiwa ni pamoja na mboga za majani na vilevile
katika mapishi mbalimbali ya samaki.
 
JINSI YA KUTAYARISHA BAADHI YA
VINYWAJI VYA VIUNGO

Kinywaji cha mdalasini

Mahitaji:
• Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini;
• Kikombe kimoja cha maji safi.
Matayarisho:
• Chemsha maji vizuri, na kisha ongeza unga
wa mdalasini;
• Baada ya hapo unaweza kuongeza asali au sukari
kidogo ili kuongeza ladha;
• Na hapo kinywaji ni tayari; kinaweza kunywewa muda wowote.

Kinywaji cha tangawizi
Mahitaji:

• Kikombe kimoja cha maji;
• Kijiko kimoja cha tangawizi mbichi
iliyopondwa;
• Sukari kidogo.

Matayarisho:
• Osha tangawizi na ponda ponda;
• Changanya tangawizi na kikombe kimoja cha maji safi;
• Chemsha mchanganyiko huo ukiwa umefunikwa;
• Acha kwenye moto mdogo kwa dakika 5 hadi 10;
• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda);
• Kinywaji ni tayari.

Kinywaji cha kitunguu saumu
Mahitaji:

• Tumba 3 hadi 4 za kitunguu saumu
kilichopondwa au kukatwa vipande vidogo
vidogo;
• Kikombe kimoja cha maji safi;
• Asali au sukari kidogo.

Matayarisho:
• Chemsha maji vizuri;
• Ongeza kitunguu saumu kilichopondwa au kukatwa vipande vidogo
vidogo, kwe n ye maji yanayochemka, funika na kisha acha
mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 10;
• Ipua na acha mchanganyiko huo upoe;
• Unaweza kuongeza asali au sukari ili kuongeza ladha;
• Kinywaji ni tayari.

Kinywaji cha tangawizi na mdalasini
Mahitaji:

• Nusu ( ) kijiko cha chai cha tangawizi mbichi
iliyopondwa au kukatwa vipande vidogo vidogo;
• Robo ( ) kijiko cha chai cha unga wa mdalasini;
• Kikombe kimoja cha maji safi.

Matayarisho:

• Chemsha maji kisha ongeza tangawizi, funika na acha
vichemke kwa dakika 10;
12


Baada ya hapo ongeza unga wa mdalasini na acha mchanganyiko
huo uchemke kwa muda wa dakika 5 zaidi;
• Ipua na kisha chuja kinywaji hicho. Sasa kinywaji ni tayari kwa
kutumia;
• Unaweza kuongeza sukari kidogo ili kuongeza ladha.

Kinywaji cha Limau
Mahitaji:

• Limau moja;
• Nusu ( ) kikombe cha maji safi;
• Sukari kidogo.
Matayarisho:
• Osha limau kwa maji safi kisha kamua ili kupata maji ya limau;
• Chemsha maji vizuri;
• Ongeza maji ya limau kwenye maji hayo;
• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda);
• Ni vizuri kunywa kinywaji hiki kingali cha moto.

Kinywaji cha Nanaa (Mint)
Mahitaji:

• Majani ya nanaa;
• Kikombe kimoja cha maji safi;
• Sukari kidogo (kama unapenda).

Matayarisho:

• Osha nanaa vizuri na kisha katakata vipande
vidogo vidogo;
• Weka vipande hivyo kwenye kikombe;
• Chemsha maji vizuri na ongeza maji hayo kwenye kikombe chenye
nanaa;
• Funika vizuri na acha kwa dakika 5.
• Ongeza sukari kidogo (kama unapenda) na sasa kinywaji ni tayari.
Kumbuka kutumia vyombo safi na maji safi na salama
wakati wote.
 
waooh nice..asante MziziMkavu mpangilio ni mzuri na unaeleweka.nashukuru kwani kuna viungo vingine ambavyo sikujua kama vinaweza kutengeneza kinywaji.
 
Eeka mbe! Sasa baba yangu, viungo vingine ndio navisoma leo, je huku Bara viungo hivyo vipo??
 
Back
Top Bottom