Matumizi ya R na L

Jomse

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
275
92
Kumekuwa na matumizi mabaya ya R na L mfano amerara badala ya amelala .Kibaya zaidi hata humu Jf wanayatumia vibaya.Kuna gazeti moja leo limetoa makala yenye upungufu huo.Nini kifanyike?
 
Mkuu hii inatokana na kabila ya watu jamani, hili tatizo ni la kitaifa hasa kikanda ya ziwa huwa tuna shida sana kule kwetu kila kitu huwa ni r rrrrrrr na wenzetu wao ni llllllll na pengine hhhhhhhh kwenye A so nikukubali kuwa ni tatizo na kuanza kulipunguza. Babu yangu alisoma wakati wa mkoloni na alinambia kulikuwa na kipindi (subject) cha kutamka maneno inavyopaswa. siku hizi hakuna!
 
Ni kweli usemayo lakini mimi nimekutana na watu ambo hawana hili tatizo la kikabila au mazoea ya kilugha lakini wanaiga hili tatizo ili waendane na kundi au mkusanyiko walipo.

Hili la kusawazisha matamshi kweli linahitaji juhudi na mpango maalum katika shule zetu. Zamani ndio lilikuwepo somo la matamshi ya sauti,(phonetics) na mtu yeyote anaweza kujifunza na kutamka sauti ambazo hazimo katika lugha yake.

Leo hakuna mwenye hamu wala muda wa kujifunza vitu taratibu na kwa utaratibu...ni utamaduni wa fasta fasta!
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani kiwango cha elimu kimeshuka. Hata kama mtu atakuwa hawezi kutamka herufi fulani kwa sababu ya athari ya lugha yake ya kwanza, inabidi aweze kuandika vizuri. Nadhani jambo hili halikuzingatiwa mashuleni, na sasa jambo hili la kuchanganya herufi, hasa katika uandishi, limekuwa jambo la kawaida.
 
Wanakoseaga tu kwenye Ngeli, na sio kwenye majina. Umewahi kuwasikia wakiita Lostam?
 
R= Rostam,
L= Lowassa,

Am sori kama nimekosea matumizi yake kiuelewa.
 
Wanakoseaga tu kwenye Ngeli, na sio kwenye majina. Umewahi kuwasikia wakiita Lostam?
Kweli wakuu, hili jambo linanikera kulikoni. Bora hata ukutane na mtu hajui kutamka, utaelewa. Ila ikija takita kusoma hua nachanganyikiwa, naanza kujiuliza mwandishi alimaanisha nini. Utakuta mtu kaandika "polini", mngine kaandika "piripiri". Kha!
 
Kibaya zaidi hata watangazaji wa radio na tv... Kuna mdada ATN akisoma magazeti utaboreka
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani kiwango cha elimu kimeshuka. Hata kama mtu atakuwa hawezi kutamka herufi fulani kwa sababu ya athari ya lugha yake ya kwanza, inabidi aweze kuandika vizuri. Nadhani jambo hili halikuzingatiwa mashuleni, na sasa jambo hili la kuchanganya herufi, hasa katika uandishi, limekuwa jambo la kawaida.

U said it all mkuu, nakumbuka pia nimewahi kuraise the same issue! Nakumbuka shule ya msingi tulikuwa tunakomaliwa mpka lugha inanyooka. Sasa unashangaa siku hizi hata magazeti ya serikali yanaboronga kimtindo huo huo. My grandpa would neva pronounce "z" and had "s" in place lakini katika maandishi yake sikuwa kuona ameandika "samani" badal ya "zamani" au "simbabwe" badala ya "Zimbabwe". Worse still mtafaruku huu umeingia hata kwenye kiingereza lugha ambayo maana hubadilika kabisa just for mixing that one lettering. Nakumbuka hum,u humu JF kuliwahi kuwa na tangazo "FLAME FOR SALE" ikimaanisha frame.
 
hana mimi linanikera kweli... sanasana hawa ndugu zetu wazaramu ! ukienda tanga ukimkuta mwanamke wa kidigo / kisegeju kiswahili anachoongea .. hutotaka amalize "ni sawa cha wale kina dada wa bbc kiswahili" kiswahili kitamu chenye ladha masikioni
 
Wanakoseaga tu kwenye Ngeli, na sio kwenye majina. Umewahi kuwasikia wakiita Lostam?

Hata kwenye majina mkuu.Kwenye gazeti aliandika waparestina badala ya wapalestina.Hapo ndipo nilipoona kuna tatizo.
 
Back
Top Bottom