Matumizi ya pikipiki-Serikali mnasubiri wafe wangapi ndio mshtuke?

Bobby

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
2,182
1,890
Jana au juzi nilimsikia Kamanda wa kikosi cha barabarani, Kamanda Mpinga, akisema kwamba moja ya sababu kubwa mpaka sasa idadi ya watu waliobadilisha leseni mpya kuwa chini ni fact iliyowazi kwamba waendesha pikipiki wengi hawana leseni. Nakubaliana naye asilimia 100 kwamba ndugu zetu hawa wengi wao hawapaswi kuwa barabarani na ndio maana wengi wao wanapoteza maisha kila siku.

Kinachonisikitisha na kunishangaza sana sana ni kwamba serikali kumbe inajua chanzo cha tatizo lakini haiko tayari kuchukua hatua kunusuru maisha ya raia wake yanayopotea kila siku. Ndani ya siku chache kabisa nimepoteza watu wangu wa karibu kwa ajali za pikipiki, infact mwingine nimepigiwa simu 5 minutes ago. Serikali mnashindwa nini kupiga marufuku matumizi ya pikipiki kwenye main roads? Barabara tulizonazo hususani Dar hazitoshelezi hata magari yaliyopo sasa ukiongeza pikipiki tena zinazoendeshwa na madereva wasiojua sheria za barabari unatarajia nini zaidi ya vifo na vilema vya maisha? Nionavyo mimi faida za kupiga marufuku ni kubwa kuliko hasara. Serikali chukueni hatua haraka please au mpaka waziri afe kwenye ajali ya pikipiki? Bahati mbaya hili linaweza lisitokee kwani wao wanatumia mashangingi. Au may be mnasubiri taarifa za kiintelijensia kwamba ndugu zetu wanakufa kila siku kwa ajali za pikipiki? Kama ndivyo basi mimi ninawapa bure kabisa, watanzania wengi wanapoteza maisha kwa ajali za pikipiki please chukueni hatua madhubuti na kwa wakati.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom