Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,020
- 577
Lazima tutambue hapa kwamba CCM wanatumia strategy ile ya "Adui ya adui yangu ni rafiki yangu". Lakini ajabu kwamba spika amezidiwa mapema hivi, kiasi kwamba hata akiwapo kwenye kiti chake bado wabunge wanapafanya bungeni ni kijiwe cha taarab.
Wabunge kwa ujumla bunge la sasa wamejidhalilisha na kujipotezea heshima yao. Hata kule kuitwa mheshimiwa kwa sasa naiona kama wanajidhalilisha zaidi maana wamethibitisha kwamba hawastahili. bado kidogo tunawazidi majirani zetu Kenya tutaanza kutwangana bungeni kama hoja haitaeleweka kwa maneno ili kuonyesha msisitizo. I am so worried!
Tulishaambiwa sana tupingane lakini pasipo kupigana. Kuzomeana bungeni sikumbukikumewahi kutokea hapo nyuma. Wanaume kwa wanawake waisikika kuzomea na kutema maneno ya kejeli kwa sauti kubwa kiasi kwamba unaweza kujua anayeongea ni nani. Yaani hakukuwa tofauti na wavuta bhangi. Spika akakaa kimya maana hata akisema kitu alionekana sauti yake kuzamishwa na za wazomeaji. Ni aibu isiyo na ufafanuzi labda wanafiki tu wanaweza.
Ina mana wabunge wa sasa hawajui kwamba kuna aina nyingi za mtu kulalamikia kile anachoamini kuonewa na pasipo kupewa uhuru wa kusikilizwa? Kwani Tanzania tuko dunia ya wapi? Majuzi tu tuishaambiwa kwamba kutoka nje sio mojawapo ya makosa bungeni. Kwa hiyo wabunge wa sasa ina maana shule haipandi hata hawafundishiki?
Tuwakumbushe tu kwamba raha zao ni maumivu yetu tuliowatuma huko. Hatukuwatuma kule kujenga vigenge vya kihuni bali wapaze sauti juu ya mambo yanayotukera. Hivi sasa umeme ni shida achilia mbali gharama yake juu. Maisha ni hoi kwa kila mtanzania wa kawaida, hawaoni hayo?
CCM ina maana mko radhi kweli kuiongoza nchi ya watu hohehahe milele? Mnajidanganya, kama mnadhani natania subiri au ulizia dibaji ya Tu nisia na Egypt. Msifanye sherehe kwenye matanga ya mtu masikini, hata maiti zinaweza kuwageuka.
===========
August 2012:
Napendekeza Tanzania tuache kutumia neno "Mheshimiwa" kwa viongozi

Wakati wa utawala wa Mwinyi tulishuhudia kujikweza kwa viongozi wetu na kutaka waitwe "Waheshimiwa", wakibadili neno lililotumiwa kwa miaka mingi kwa viongozi na watanzania kwa ujumla wote kuitana "ndugu".
Ukweli ni kwamba wengi hatujagundua kwamba toka viongozi waanze kuitwa "waheshimiwa" walianza kujiona kama tabaka la aina iliyo juu mbali na mwananchi wa kawaida, wengi wao wakawa mafisadi na kusahau shida za wanachi wa kawaida waliowawakilisha.
Kumbuka neno "ndugu" lilitumika kwa kila mtanzania, hata katika katiba nadhani, tuna misemo kama "binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja".
Tangu lianze kutumika, neno "mheshimiwa", lililopata baraka zote na viongozi wa CCM, lilimekuwa kama neno lilololeta laana kwa CCM na uongozi Tanzania.
Kwa msingi huu basi, napendekeza turudi tena kwenye matumizi ya neno "ndugu" badala ya "mheshimiwa". Na ukweli ni kwamba heshima inayohusiana na "uheshimiwa" ni jambo ambalo mtu analipata kwa matendo yake (you earn respect rather respect by default).
Na pia, japo tunawaita viongozi na wabunge "mheshimiwa" kuna wengi sana hawastahili kabisa kuitwa hivyo. Binafsi niko radhi sana kumwita kiongozi fisadi "ndugu" kuliko "mheshimiwa".