Matumizi ya Magari ya umma kwa Shughuli Binafsi ni UFISADI pia

Patriote

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
1,718
1,047
Wakati kukiwapo na waraka wa Serikali unaopiga marufuku magari ya yake kutembea baada ya saa za kazi bila kibali maalumu, magari hayo sasa yanaonekana kwenye baa na kumbi za starehe nyakati za usiku.Uchunguzi uliofanywa wa wiki mbili sasa umebaini kuwa utaratibu huo wa kupewa vibali umekuwa ukikiukwa na maofisa wenye dhamana na magari hayo na wamefikia hatua ya kuyatumia kwa ajili ya kwendea sokoni siku za Jumapili na Jumamosi.

Tatizo hilo ni kubwa zaidi kwa magari yaliyoko chini ya Ofisi ya Makatibu Tawala wa Mikoa na Wilaya, Halmashauri za miji na majiji (SM), mashirika ya umma yanayotumia nambari za SU na yale ya miradi yanayotumia DFP. Uchunguzi huo umebaini kuwa tatizo ni kubwa zaidi katika Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam na Dodoma ambapo magari hayo yanatumika pia kwenda kwenye mashamba binafsi siku Jumamosi na Jumapili.

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alipotafutwa simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa, huku Katibu Mkuu wake, Balozi Hurbet Mrango na Naibu Katibu Mkuu, Dk John Ndunguru nao simu zao zikiita tu bila kupokelewa. Utaratibu unataka maofisa hao kupatiwa "kibali cha kutumia gari la Serikali baada ya saa za kazi" kupitia fomu namba EM 1(B) ambayo hutakiwa kueleza muda gari litakaotumika na jina la ofisa na dereva. Mbali na kuweka sharti la lazima la kuonyesha muda halisi gari hilo litakapoanza kutumika na muda wa kikomo, lakini fomu hiyo inataka ni lazima ionyeshwe gari hilo litapita katika barabara zipi.

Kibali hicho kinatakiwa kitiwe saini na Katibu Mkuu au Mkuu wa Idara kwa magari ya wizara, Katibu tawala wa mkoa au wilaya kwa magari ya ofisi ya mkuu wa mkoa au wilaya na wakurugenzi kwa magari ya halmashauri.

"Lakini hali ilivyo sasa ni kama vile hatuna Serikali yenye viongozi makini kwa sababu kila mmoja anafanya lake, magari yanatumika kwa kazi binafsi za kifamilia lakini kwa gharama ya mafuta ya kodi za wananchi," walisema baadhi ya wafanyakazi wa Serikali ambao hawakutaka kuandika majina yao.

Maoni yangu

Utaratibu mzima wa watumishi wa serikali kutumia magari ya kifahari ya serikali kuwatoa nyumbani na kawaleta ofisinini na kuwarudisha nyumbani baada ya saa za kazi kwa ujumla wake utaratibu wa kibwanyenye. Wenzetu wa nchi zilizoendelea utaratibu huo haupo, ni jukumu la mtumishi kufika kwenye kituo chake cha kazi kwa means zozote zile.

Serikali ingesaidia watumishi wake kwa kuwadhamini wachukue mikopo ya magari via taasisi za kifedha zilizopo. Aidha, Serikali pia ingesaidia watumishi wake wote kwa kutoa flat-rate transport allowance.Kazi kubwa ya serikali ingebaki kuweka efficient public transport system in place kwa ajili ya kusafirisha wananchi wake wote efficiently. Pesa inayotumika kununulia na kuhudumia mashangingi kwa watu wachache huku ikiacha watumishi wengine wanateseka ingeelekezwa kwenye utengenezaji wa miundombinu ya kisasa kwa ajili ya high standard city trains na city buses kwa kuwahudumia watu wengi zaidi.

Utaratibu huu ndio unaotumika nchi za wenzetu na hivyo kuokoa gharama nyingi sana zisizo za msingi kwa serikali. Nchi nyingi za Ulaya watumishi wanafika ofisin kwa magari yao wenyewe, ofisi inakuwa na magari machache sana kwa shughuli za ofisi tu. Mimi nadhani sisi nchi masikini tunafaa kuiga utaratibu huu badala ya kung'ang'ana na utaratibu wa kikabaila ilhali serikali yetu ipo dhohoflihali na ikijikuna inatoka unga. Je wana JF mwalionaje hili???





 
Hili ni tatizo sugu katika utawala nchi hii. Ubinafsishaji wa mali za umma upo kila mahali na kosa letu sisi wananchi kutokuwa wakali katika matumizi wa rasimmali hizi. Leo hii kuna majengo na viwanja mbalimbali vilivyojengwa kwa nguvu ya umma enzi zile za chama-dola kwa minajili ya kuimarisha dola kwa kupitia chama ambayo yametwaliwa na chama tawala. Nidhamu ya matumizi ya rasilimali za umma ni sharti iende sambamba na ungalizi wa rasilimali hizi toka kwa wananchi.
 
yatasemwa mengi tu lakini hali halisi kwa sasa ni mbovu tuuu, kama ule msemo unaishi kwenye nyumba ya vioo na unarusha mawe, hapa ni kwamba msimamizi na msimamiwa wote wanacheza rafu, refa naye anacheza rafu pamoja na linesman wake, mchezo wenyewe unachezewa gizani na washangiliaji wamepewa dark glasses ili wasione, ukifanikiwa kuziona rafu hautaweza kuona refa yupo wapi, inaitwa system au darkness system, warundike kwenye giza then fanya fasta kukicha upo maili sita mbele,
 
Back
Top Bottom