Matumizi ya Kiswahili vyuoni hasa kwa fani za afya bado sana

GIBA KB

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
367
110
Za asubuhi wanajamvi,

Nianze kwa kusema mimi ni daktari nimemaliza degree yangu ya udaktari mwaka 2008 pale Muhimbili na sasa nachukua masters ya pediatrics (Magonjwa ya watoto) Mandela University Arusha.

Serikali imetoa sera mpya ya elimu ambayo imeazimia kiswahili kutumika kama lugha ya kufundishia kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu. Matumizi ya kiswahili kwa chuo kikuu hasa kwa fani za Afya itakuwa ngumu kwa sababu:

1)Hatuna wataalamu waa kutosha wa kuweza kutafsiri vitabu vinavyotumika kwa kiswahili.

2)Fani za udaktari zina maneno mengi magumu ambayo hata kwa kiingereza unaweza ukashindwa kuyaelewa.

3)Kutumia kiswahili kufundishia kutamnyima daktari nafasi ya kupata ajira nzuri tu nje ya nchi.Mfano UN,Unicef,South Africa n.k

4)Hatuna teknolojia tunayoweza kutumia hata km tutajifunza kwa kiswahili.

Hizo ni baadhi tu ila zipo nyingi.Hili suala ni muhimu sana liangaliwe vizuri.Sio kwamba napinga kiswahili kisitumike la hasha!! Napenda ty lakini maandalizi yawepo ya kutosha.
 
GIBA KB

Chief, Nelson Mandela wameanza kutoa MMED ya Pediatrics? Wameanza mwaka gani? And mnatumia hospitali gani as a teaching hospital?
 
Last edited by a moderator:
GIBA KB

Wewe kama ni kweli ni Muhitimu wa Chuo kikuu cha nchi yetu basi nadiriki kusema haukupikwa vizuri labda siyo kosa lako nitajaribu kujibu baadhi ya maswali yako!

- utafsiri wa vitabu, unasema hakuna Wataalamu, sasa hilo nalo ni tatizo? Kwani Biblia alitafsiri nani? Kuna mpaka Biblia ya kiyao na Kimasai kuna kazi ngumu kama hiyo?

Na kwa taarifa yako tu kazi ya kutafsiri Biblia ilifanywa na wazungu na hii ni kutoka Kijerumani (kwa wakati huo) kwenda Kiswahili na hawa Wazungu walikuwa wala kiswahili Siyo Lugha yao sasa jiulize waliwezaje kutafsiri Biblia ktk lugha yao ya Kijerumani kwenda kwenye lugha ngeni ya Kiswahili halafu sisi tushindwe kutafsiri ktk tu Kiingereza kuja kwenye Lugha yetu?

- Udaktari una maneno magumu unamaanisha nini? hata kwa kiingereza unashindwa kuyaelewa kwa maana kiingereza siyo Lugha yako na hapo ndipo tatizo lilipo unalazimisha tu,

na isitoshe mimi Shule ya Msingi nimesoma sayansi ya Viumbe kwa Kiswahili (Biology) mbona mbona tulikuwa tunasema mamalia, protozoa, Mitokondria, seli nyeupe/nyekundu, n.k na mbona tulielewa?

-Unasema kutumia Kiswahili madakatri hawawezi kupata kazi nje na hapo ndipo unapozidi kuonyesho kutokuiva kwako pmj na kudai kwamba umesoma jukumu la Serilaki yoyote ile ni kusomesha watu wake kwa faida ya watu wake hakuna Serikali Duniani inayotumia fedha nyingi kusomesha Watu wake ili wakafanye kazi Umoja wa Mataifa au Nchi nyingine

na ndio maana hasa Nchi zenye watu wenye akili husomesha watu wao kwa lugha ambayo inatumiwa ktk hiyo nchi ili wahitimu waweze kuwahudumia vizuri wananchi ambao ndiyo walipaji kodi!
 
limetumbuka Kwa kweli nimependa jinsi umeshikilia jambo hili. Ni kama uko katika mawazo yangu. Afadhali nyie huko TZ mko 50-50. Huku kwetu watu wengi wana mawazo ya kuwa ni wakoloni.

Yaani umerudia maneno yote amabyo mimi husema kila siku ninapopingana na watu amabo husema eti sijui, bila kutumia English Medium, ati huwezi pata Kazi.

Watu wamesahau kuwa Cuba ndio Nchi moja iliyo na sekta nzuri ya afya na hawatumii kingereza. Natamani watu kama wewe wangejaa huku Kenya ili tuwe na mabadiliko. Hongera sana.

Jambo ambalo sielewi ni Kwanini Tanzania inafanya vigumu kutafsiri maneno? Kwa mfano, Biology ingefaa iwe Bayolojia wala si Biolojia. Mitochondria ingefaa iwe Maitokondria bali so Mitokondria. Kwa maoni yangu.

kuitafsiri njia hii itarahisisha kazi mtu anapotaka kufanya transition kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.
 
limetumbuka Kwa kweli nimependa jinsi umeshikilia jambo hili. Ni kama uko katika mawazo yangu. Afadhali nyie huko TZ mko 50-50. Huku kwetu watu wengi wana mawazo ya kuwa ni wakoloni.

Yaani umerudia maneno yote amabyo mimi husema kila siku ninapopingana na watu amabo husema eti sijui, bila kutumia English Medium,

ati huwezi pata Kazi. Watu wamesahau kuwa Cuba ndio Nchi moja iliyo na sekta nzuri ya afya na hawatumii kingereza. Natamani watu kama wewe wangejaa huku Kenya ili tuwe na mabadiliko. Hongera sana.

Jambo ambalo sielewi ni Kwanini Tanzania inafanya vigumu kutafsiri maneno? Kwa mfano, Biology ingefaa iwe Bayolojia wala si Biolojia. Mitochondria ingefaa iwe Maitokondria bali so Mitokondria.

Kwa maoni yangu. kuitafsiri njia hii itarahisisha kazi mtu anapotaka kufanya transition kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza.

Nitakwambia kitu kimoja kinachotusumbua sisi Waafrika kikubwa kuliko vyote ni kutokujiamini, kujidharau na kujishusha, kwa mfano leo hii Kikwete akisema ya kwamba kuanzia leo TZ tutatumia Kireno (Portuguese) kama Lugha ya kufundishia ungeshangaa watu wengi wangefurahia hilo ingawaje Dunia nzima Kireno huongewa Brazili, Ureno kwenyewe na Angola labda Moz.

Utaona kwa mfano mimi kama Mtz nikienda Ghana leo hii nikasema sijui kiingereza kwa sababu najua Kiswahili Waghana watanicheka, kunidharau na kunikebehi lkn Muangola akienda huko huko Ghana akasema kwamba hajui Kiingereza kwa maana anajua Kireno basi watamuelewa na hata kuanza kumuona kwamba ni mtu wa maana sijui kama unanipata ninachomaanisha, na hapo ndipo tatizo lilipo hapa Afrika kwetu!
 
limetumbuka,

umenifurahisha sana ndugu yangu saaana tu, kati ya michango nilioiona ya maana mwezi huu ni huu wako.

Mimi kwa kukolezea tu niseme hakujawahi kuwa na nchi duniani inayotumia rasilimali zake kusomesha watu wake ili wakafanye kazi nje. Nia ya serekali nikuelimisha watu wake waelewe na watatue matatizo yanayowazunguka.
Hakuna nchi duniani iliyopiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kutumia lugha za kigeni.

Madhumuni ya awali ya elimu yalikuwa sio kuzalisha wafanyakazi, bali ni kuielewa dunia. Lakini bado itakuwa ni nafuu mara mia kuajiri mtu aliesoma kakielewa kitu kuliko aliyekariri kwa kutokuelewa.
 
Last edited by a moderator:
limetumbuka,

Kaka Ahsante sana, natumai Amekuelewa. Hivo hii Lugha inaanza lini?

Watu tumechoshwa kwenye maofisi eti lugha ni English mpaka kwenye Interview utadhan hatuna Lugha yetu bhanaa!!
 
Last edited by a moderator:
limetumbuka

Haha..Mkuu, unanifurahisha sana. Yaani, ni kana kwamba umewajadili hawa watu ukachoka. Huku Kenya, utapata shule zinawafunza watoto lugha ya kifaransa. Watoto wako katika darasa la kwanza, eti wanjifunza Kifaransa.

Ukitoa hoja, na je, tukiwafunza watoto Kikuyu, au kijaluo? Utaona watu wanakuita mjinga. Kuna taifa jina lake Iceland. Liko na watu 320, 000 pekee. Wao wanatumia Icelandic kwanzia Chekechea hadi chuo Kikuu. Lakini hutaona Mbongo au Mkenya akisema kuwa hawezi tibiwa na daktari wa Iceland eti hawajui Kiingereza.

Lakini ukisema ulisomea shule ya upili katika lugha ya kiswahili, amabayo inaongelewa na watu Zaidi ya milioni mia moja, utaona watu wanashuku ustadi wako kwa vitu vyote.

ikiwa mtu atatoka Iceland aanzishe Shule TZ au Kenya na fundishe Icelandic kama lugha ya ziada, wengi watamfurahia. Lakini ebu kuja ufundishe kichaga au Kijaluo na watu watakuona mkabila; mpumbavu na mtu anayetaka kuwarudisha wengine nyuma.

Hivi juzi, nilimuuliza mwalimu wa shule ya chekechea kwa nini asifundishe watoto wa miaka mitatu kwa lugha ya kiswahili. Alicheka sana na kuniambia kuwa tayari, mtoto ashajua kiswahili, ni nini unamfundisha shule.

Nilihuzunishwa sana kwa kuwa nilikuwa nataka maoni yake kuhusu kitabu nilichokuwa nikiandika ambacho ni cha Kiswahili. Watoto wengi huku ukimwambia aandike Kuku, atakuandikia CooCoo au kama ni Kaka, ataandika Caca au Cucu.

Hii ni kwasababu shule hufundisha Kiswahili katika mhula wa mwisho katika shule ya chekechea. Kuna shule zingine ambazo hungoja hadi darasa la kwanza kabla mtoto kujifunza Kiswahili. huu ni umaskini wa kimawazo.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom