Matumizi ya iPad Bungeni: Nahodha amuiga Zitto?

Mzalendo

Senior Member
Mar 10, 2006
181
32
Waziri wa mambo ya ndani anasoma budget yake kama mhe zitto kupitia ipad mjengoni now!!
 
Waziri wa mambo ya ndani naye hajapitwa na teknolojia,anatumia ipad kuwasilisha hotuba ya wizara yake.
 
Kumbe hata wazanzibar wapo hahahahah safi sana!
Sijui ataongelea polisi kuua raia kwa risasi za moto??
 
Waziri wa mambo ya ndani anasoma budget yake kama mhe zitto kupitia ipad mjengoni now!!
kadesa huyo. ]
majuzi nimekutana na mbunge mwingine wa CCM (Jina kapuni) akiwa pale Samsung mlimani city anauliza nataka ile simu ipo kama laptop. anaulizwa ikoje anasuasua kujibu - mpaka mimi nikamsaidia ni ipad mweshimiwa? akasema ndiyo hiyo hiyo kijana asante kunisaidia. akalipa akasepa, nafikiri sasa hivi atakuwa ameajiri mwalimu wa kumfundisha matumizi.

Mh. Zitto umezua balaa bungeni -- lol
 
Waziri wa mambo ya ndani naye hajapitwa na teknolojia,anatumia ipad kuwasilisha hotuba ya wizara yake.

Tunataka hoja. Na huyu nadhani atabanwa na akina Tundu Lissu manake suala la polisi kuua raia litajitokeza kwa mapana yake!! Atumie ipad ama ipod tunataka hoja na jinsi ya kutoa elimu ya uraia kwa polisi ili wasiue raia hovyo.
 
They area all followers. Wa kwanza ndio anang'ara!

Mkuu wa kwanza ni nani vile? Mzungu au? Tunakuwa wa kwanza kusema ziwa victoria halikuvumbuliwa na Spake kwa kuwa kulikuwa na wasukuma na wakerewe huko ziwani kabla hajaja mzungu!! Leo tunakuwa wa kwanza kusema Zitto ndio wa kwanza!! Mimi nadhani wa kwanza ni mzungu au?
 
Nahodha is one of good leaders, anajifunza, msikivu, na ni kiongozi.

You made TEHAMA FAMILY proud today, big up mambo ya ndani... Big up ict team pale wizarani.
Congrats comrade.
 
They area all followers. Wa kwanza ndio anang'ara!
<br />
<br />

Tangu lini Zitto wa kwanza kutumia I pad ?.Inchi nyengine kifaa hiki mainstream,watoto wanakitumia kucheza games.La muhimu siyo nani katumia Ipad mwanzo bali convinience inayompa mtumiaji hasa for presention purpose.Navigation is second to non.
 
Mkuu wa kwanza ni nani vile? Mzungu au? Tunakuwa wa kwanza kusema ziwa victoria halikuvumbuliwa na Spake kwa kuwa kulikuwa na wasukuma na wakerewe huko ziwani kabla hajaja mzungu!! Leo tunakuwa wa kwanza kusema Zitto ndio wa kwanza!! Mimi nadhani wa kwanza ni mzungu au?

Wa kwanza kwa kutumia ipad kwenye bunge letu la Jamhuri. Pengine kama Zitto hakufungua pazia wote wengekuwa kwenye makaratasi!
 
Maendeleo yanaanza hivyo! Hamkumsikia Lusinde juzi alivyodai kuwa aliyegundua pen baada ya kuona imepitwa na wakati akaanzisha calculator, baadaye computer. Kweli magamba kwa kufananisha visivyofanana.
 
Wakuu huku Arusha Ngeleja katukatili, mtujuze kuhusu bajeti ya Mh. Lema, waziri kivuli mambo ya ndani ya nchi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom