Matumizi ya gas ya kupikia na mkaa

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
1,083
1,135
Habarini wakuu.
Siku zote nimekuwa nikitumia nishati ya mkaa ktk kupikia nyumbani kwangu.lkn kuna watu wamenishauri kuwa gas(oryx) ni gharama nafuu kuliko mkaa.je ni kweli jamani naombeni ushauri kabla ya maamuzi.ahsanteni
 
Gas ni safi (nyumba yako haichafuki)
Unatumia unapohitaji (si kama mkaa, ukishawasha hata kama ni kuchemsha chai tu basi moto hupote bure)
Unaokoa mazingira (imagine hilo gunia moja la mkaa ni sawa na miti mingapi? Na kwa mwezi unatumia magunia mangapi? Kwa mwaka je, unatumia eka ngapi za msitu?)
 
sikia nikuambie, jiko la mkaa utanunua sh.30elf, gunia la mkaa sh.45elf na unaanza kupika hadi gunia liishe ni miezi 2. lakini Gas, jiko na mtungi wake pamoja na gesi yenyewe utanunua kwa sh.laki 2 na kila ges ikiisha utajaza sh.58elf kwa mtungi wa kilo 16, utatumia mwezi 1 na nusu. hebu fuatilia uone.
 
Usidanganye watu! Takwimu zako si sahihi kabisa. Kwa mtumiaji wa gunia moja la mkaa kwa miezi 2, mtungi wa gas wa kilo 15 (sio 16) nina hakika atatumia miezi 4 hadi mitano. Ukweli ni kuwa gharama ya kuanzia (initial cost) ni kubwa; deposit ya mtungi na kununua jiko lenyewe, lakini gas ni nafuu mno. Mimi nina familia kubwa (watu wazima 5), tunachemsha maji ya kunywa, tunapika mara tatu kila siku, tunakaanga samaki very often: matumizi ya mtungi wa gas ni 40 days. Sembuse mtumiaji wa gunia moja la mkaa kwa miezi 2. Kama huamini invest kwenye gas utakuja kukiri hapa!
 
Haya maelezo hayana ukweli wowote jamani,gas is the best hebu jaribu utafurahia na wala hutarudia tema kutumia mkaa kamwe.
 
Ahsanteni wakuu,naenda kununua gas kesho ili nijaribu.lakini sielewi nitapata wapi jiko(2plets) imara kwa bei nafuu.
 
Habarini wakuu.
Siku zote nimekuwa nikitumia nishati ya mkaa ktk kupikia nyumbani kwangu.lkn kuna watu wamenishauri kuwa gas(oryx) ni gharama nafuu kuliko mkaa.je ni kweli jamani naombeni ushauri kabla ya maamuzi.ahsanteni
Unaishi wapi mkuu? Kipi kinapatikana kwa urahisi maeneo unayoishi?

Generally, kwa kulinganisha gharama zilizo wazi, ni kweli gas inaweza kuonekana kuwa na gharama kuliko mkaa. Lakini ukiangalia na gharama zinlizojificha- vitu kama usafi na muda pengine gas ni option nzuri zaidi (inachukua si chini ya dakika 15 kuandaa jiko la mkaa na kuanza kupika wakati gesi, ni suala la sekunde kadhaa tu).
 
sikia nikuambie, jiko la mkaa utanunua sh.30elf, gunia la mkaa sh.45elf na unaanza kupika hadi gunia liishe ni miezi 2. lakini Gas, jiko na mtungi wake pamoja na gesi yenyewe utanunua kwa sh.laki 2 na kila ges ikiisha utajaza sh.58elf kwa mtungi wa kilo 16, utatumia mwezi 1 na nusu. hebu fuatilia uone.

Uwii unanichanganya,kilo 15 gas kwa mwezi na nusu,yani kwangu ni 3weeks only,nikiwa likizo mimi ndio unakaa mwezi mzima.Yani sijui hata nifanyeje,nishasema mpaka,familia yangu ndogo tu,2kids,dada,mimi na mr.Kwa kifupi pia anaetumia anapaswa kuwa makini mmno,vinginevyo utaona bora mkaa,kurudi shida maana ushazoea fasta fasta.
 
Usidanganye watu! Takwimu zako si sahihi kabisa. Kwa mtumiaji wa gunia moja la mkaa kwa miezi 2, mtungi wa gas wa kilo 15 (sio 16) nina hakika atatumia miezi 4 hadi mitano. Ukweli ni kuwa gharama ya kuanzia (initial cost) ni kubwa; deposit ya mtungi na kununua jiko lenyewe, lakini gas ni nafuu mno. Mimi nina familia kubwa (watu wazima 5), tunachemsha maji ya kunywa, tunapika mara tatu kila siku, tunakaanga samaki very often: matumizi ya mtungi wa gas ni 40 days. Sembuse mtumiaji wa gunia moja la mkaa kwa miezi 2. Kama huamini invest kwenye gas utakuja kukiri hapa!

Jamani mbona mnanitisha,au inategemea na aina ya jiko,hebu niambie jiko lako ni aina gani?umezidi kunidatisha,mimi hata maji ya kunywa nachemshia kwenye umeme,lakini ni 3week tu gas imeisha.Au mtungi haujai,kulaleki nitaanza kuja na mtungi posta upimwe kabisa,siiti tena.Nielewesheni jamani nijue how to save it.
 
Mkuu hapo nami nimestuka. Kwa uzoefu wangu mtungi wa 15kg (gas) huwa natumia kwa wastani wa siku 60. Familia ya 4 people. Maharage tu ndo yanachemshiwa kwenye umeme.
 
Habarini wakuu.
Siku zote nimekuwa nikitumia nishati ya mkaa ktk kupikia nyumbani kwangu.lkn kuna watu wamenishauri kuwa gas(oryx) ni gharama nafuu kuliko mkaa.je ni kweli jamani naombeni ushauri kabla ya maamuzi.ahsanteni
Tumia gas ni nzuri na utakua umelisaidia taifa katika
Harakati zake za kutunza misitu na mazingira kiujumla.
 
gas nunua petrol station na dealers wakubwa wakubwa wewe. hivi viduka vya mtaani wanachakachukua kwa kupunguza baadhi ya mitungi na jaza iliyo empty. chezea wabongo wewe au hujasikia jamaa alivyolipukiwa mwenge akiwa anadjust mitungi ya gesi
 
Mkuu hapo nami nimestuka. Kwa uzoefu wangu mtungi wa 15kg (gas) huwa natumia kwa wastani wa siku 60. Familia ya 4 people. Maharage tu ndo yanachemshiwa kwenye umeme.

Sasa ni nini,maana hata mi maharage nachemshia kwenye umeme na pressure cooker,why 3 weeks jamani?mi ni mdada lakini sio mkuu,maana mkuu nahisi umemaanisha mkaka,au!
 
Gas ni safi (nyumba yako haichafuki)
Unatumia unapohitaji (si kama mkaa, ukishawasha hata kama ni kuchemsha chai tu basi moto hupote bure)
Unaokoa mazingira (imagine hilo gunia moja la mkaa ni sawa na miti mingapi? Na kwa mwezi unatumia magunia mangapi? Kwa mwaka je, unatumia eka ngapi za msitu?)
none sense yani una mawazo mepesi namna hii wewe,is that all about the difference
 
Mm nadhani suluhisho ni kuainisha gas kg kadhaa inatumika kwa muda fulani ukiiwasha bila kuzima?
 
Mi mkaa kwangu nishapiga marafuku kama mwaka wa 5 sasa sinunui mkaa, natumia gesi na umeme na jiko la umeme linatumika kwa ajili ya vitu vigumu kama maharage, maji ya kunywa, kuoga n.k. na umeme nalipa elfu9700/= kwa mwezi. Na gesi natumia elf 54 kwa mwezi na siku 10
 
Back
Top Bottom