manenge
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 279
- 17
Mimi nimeshikwa na kigugumizi, mwaka 2005 kagada Agriculture walikwapua sh billioni 40 na uchunguzi usiokuwa rasmi ulibaini zilikwenda kwenye uchaguzi wa CCM. Sio nia yangu kuongelea mambo ya zamani lakini ukwapuaji ule na uchangishaji wa amount inayolingana na ile ya zamani hauna mahusiano? bila shaka yapo.Cha kunishangaza zaidi ni pamoja na sasa kuwa na sheria ya kudhibiti matumizi ya fedha chafu. Endapo mtu atachangia hela chafu watawezaje kuchuja kwamba hizi ni safi na hizi ni safi?Pili matumizi ya bilioni 40 kwenye uchaguzi kwa nchi masikini kama tanzania ambayo wagonjwa wawili huchangia kitanda kimoja na wanafunzi kukaa chini bila madawati inaingia akilini kweli? Kuna haja ya kufikiri upya kwamba tunataka nini na nini kianze