Matumizi makubwa yasiyo na tija kwa serikali.

LE GAGNANT

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
1,241
251
Serikali ya TZ ina matumizi mengi ambayo hayana faida yoyote kwa mwananchi wa kawaida. Mfano: Kuna viongozi lukuki wastaafu wa kisiasa na kijeshi wanaoendelea kulipwa mishahara hadi wafe. Marais na mawaziri wakuu wastaafu bado wanapata marupurupu yote maishani. Jeshini kuanzia cheo cha major general, lieutenant general na general wakistaafu wanaendelea kulipwa mishahara hadi wafe na mashangingi wanabadilishiwa yakichoka, service zote serikalini na marupurupu kibao. Ukichanganya na wabunge wa kuteuliwa, waku wa mikoa na wilaya ambao kazi zao zinafanywa na wakurugenzi, wao ni kutoa matamko tu. Mkulo, ndio maana pesa inaishia kuwalipa wao kwa kuwa wao wana 'lion share'.
 
Jamani wafandhili hawaoni Haya!! Unampa mtu hela ya walipakodi wako ili ichezewe? Duh aibu kwa wafadhili, Maendeleo ya kweli yatakuja tutakapodai uhuru kwa mara ya pili
 
nadhani haya sio matumizi ya anasa wewe unataka mtu akistaffu aje akale njaaa humu uraiani ,mbona mmekuwa wabahili sana kila jambo linalofanywa mnaona ni anasa
 
Anachosema ni kwamba huruma imezidi uwezo; kulipa mstaafu fedha stahili za kumwezesha kumudu maisha yake halina tatizo, hoja ni kwamba hapa katikati viongozi wetu walijipangia wao wenyewe na wapambe zao mishahara minono na marupurupu mengi ya kutukoga sisi wengine, na baada ya hapo walijiwekea utaratibu wa kuendelea kulipwa hivyo hata wanapostaafu. Kwakuwa kila kukicha wastaafu hao wanaongezeka itafika mahali tushindwe kumudu gharama hiyo.
 
Back
Top Bottom