Matumizi GMO Kwa hapa Tanzania

ssl

Senior Member
Apr 20, 2013
138
101
Je, Muda wa kutumia mimea ambayo vinasaba vyake vimebireshwa nchini Tanzania umefika?

Karibu tujadiri hii kitu kitaalam maana nimeona kuna mijadala inaibuka juu ya matumizi ya GMO hapa kwetu.
 
gmo ndio nini?

vinasaba vinabadilishwaje, ili iwe nn?

nani anayebadilisha vinasaba, kashawahi badilisha hapo awali na kuthibitisha tija?

kuna madhara/ mabadiliko kwenye mfumo wa uzalishaji na ecolojia inayozunguka mmea kwa kutumia gmo?

ecosystem inayozunguka mmea inaweza kubadilishwa namna gani kwa kuingizwa kwa hizo gmo?

kuna uwezekano wowote wa hivyo vinasaba vilivyo badilishwa vikasababisha kuanzisha reaction itakayo fanya watumiaji wadudu/binadamu kubadilika vinasaba vyao?

samahani mkuu jazia skeleton ili tuweze kuchangia hoja!
 
gmo ndio nini?

vinasaba vinabadilishwaje, ili iwe nn?

nani anayebadilisha vinasaba, kashawahi badilisha hapo awali na kuthibitisha tija?

kuna madhara/ mabadiliko kwenye mfumo wa uzalishaji na ecolojia inayozunguka mmea kwa kutumia gmo?

ecosystem inayozunguka mmea inaweza kubadilishwa namna gani kwa kuingizwa kwa hizo gmo?

kuna uwezekano wowote wa hivyo vinasaba vilivyo badilishwa vikasababisha kuanzisha reaction itakayo fanya watumiaji wadudu/binadamu kubadilika vinasaba vyao?

samahani mkuu jazia skeleton ili tuweze kuchangia hoja!

Maswali Magumu ila yanatoa mwelekeo sahihi kwenye hii mada. Sina uelewa sana wa GMO.

Japo neno GMO linasimama badala ya maneno Genetic Modified Organisms. Ni technologia inayoruhusu kuingizwa kwa sifa moja au zaidi kwenye mmea au unyama ambayo awali hakuwa nayo. kitu kikubwa ivyo vinasaba ni muhimu vilandane.

Wenye uelewa zaidi waje wasaidie maana inaweza kuwa technolojia nzuri kwa ukuaji wa uchumi wa taifa letu.
 
imefika na kuna madhara mskubwa sn kwa consumer....tuna advantage ya organic fruits tu but kwenye mboga labda tule matembele na mchicha ila majangA..ni ngumu
 
Wazalishaji wa hii GMO ni nani Haswa. na je Tanzania wapo?
 
GMO usage katika nchi yetu syo stage ya kujivunia maana hakuna kipya kilicho onekana kwenye nchi za wenzetu zaid ya cancer na magonjwa ya ajabu
Siyo kila kitu wanachotumia wenzetu n bora kwetu
 
Effect mojawapo ya GMO ni kupoteza the wild type of the organism, iwe mmea au mnyama. Nakumbuka zamani kijijini kulikuwa na mbegu za mahindi ambayo ilikuwa yanalimwa na wakati wa mavuno tulikuwa tunachagua mahindi mazuri yanawekwa kwaajili ya mbegu za msimu unaofuata. Ila kwa mahindi ya kisasa ambayo ni GMO huwezi kufanya hvyo, unanunua unapanda, na kuivuna huwez kuyatunza kwa mbegu ya msimu unaofuata, ni lazima ukanunue tena kwa wauzaji. Tumeshapoteza yale mahindi ya asili. Watakuwa nayo kwenye maabara zao tu
Wanakuja na sifa kwamba GMO zinaongeza yield na kusaidia kuzuia njaa. Ila hakuna kizuri kisicho na mapungufu/madhara. Huo ni mfano mmoja tu ipo zaidi
 
Very Interesting. Africa kuna nchi wanatumia na wameugua kansa? Japo mimi najua kansa ilikuwepo tokea zamani. Kama ni kweli inamadhara kwa nini izo nchi ziruhusu watu wake waendelee kufa???
 
Sina uhakika sana,ila hii kitu GMO ishaingia na inatumika zenyewe ni mbegu ambazo haziliwi na wadudu,zinahimili ukame pia zina zaa sana,sasa sijajua kwa waliozitumia......ila nakumbuka humu ndani kuna mada iliwahi kujadili hii kitu ya GMO kindani zaidi inabidi kuitafuta!
 
Mods. kama huo uzi upo uunganisha ili watu wengi tujue kwa undani kuhusi hizi taarifa. Hakuna dhambi mbaya kama kutisha watu na usichokijua. binafsi napata maswali kuhusiana na hii kitu kwa jamii yangu. huwa sina jibu zaidi ya kuwaambia ni technolojia twaweza kubali au kuikataa. japo siamini kama inasababisha kansa
 
Back
Top Bottom