Matumizi fasaha ya maneno ya kiswahili

Babu Swahili

Member
Jan 8, 2009
41
6
Nimepewa taarifa na mjukuu'angu mmoja ya kwamba kuna uharibifu mkubwa sana wa lugha yetu ya kiswahili humu jamvini. Kwa hiyo nimekuja hapa kuwa adhibu wale wote wanaoharibu lugha yetu takatifu.

Nikianzia na hawa hapa:

Sio Mwulize, ni Muulize

...zaidi ya kushukuru sana kwa heshima hii lakini kachelea kusema kuwa ..mimi ni sawa na "kichuguu mbele ya mlima kilimanjaro"....sidhani hata kama nilitegemea kuwa recognised au sembuse kuambiwa ahsante katika wajibu....!...najuwa kuna vichwa humu ndani ni adimu ...mmoja wapo ni wewe steve d na kibunango!!!...MUNGU AWAJAZE TELE!!!

https://www.jamiiforums.com/complai...-phillemon-mikael-kwa-mabandiko-2000-a-4.html

Sio Najuwa, ni Najua

Endeleeni kuchambua mambo mbalimbali, lakini mjue ya kuwa nina macho makali sana ya kunasa kila uchafuzi wa lugha yetu.

Ndimi Babu Mswahili
 
Last edited by a moderator:
Ngabu tatizo la africa ni kupuuzia elimu ya chuo kikuu, tizama nchi zilizopiga hatua kielimu (most educated countries) ndo hizohizo zilizoendelea. Tizama nchi zinazotoa elimu ya chuo kikuu bure (Swiden, Denmark, Norway na Finland) na ndio hizohizo tajiri. Korea ya Kusini elimu ya chuo kikuu ni afordable kwa kila mwananchi pia ndio nchi ya kuigwa kwa kasi ya maendeleo.

https://www.jamiiforums.com/business-economic-forum/22686-afrika-ndiyo-bara-maskini.html

Ni vizuri kuona kuwa umejirekebisha mwenyewe ulipotumia neno la ndio kwenye sentensi nyingine.
 
Wasiliana na hawa jamaa ndo wapo karibu nae sana mara kwa mara wanampigia kujua nini kimejili juu yake watakusaidia au watakupa ushiriano wa hali ya juu sana.

Sio Kimejili, ni Kimejiri

Icho kiuno chake au kakazia na masponchi?
Naona hawa ni moja kati ya watu Mungu aliwaumba siku ya kwanza kabla hajachoka.
Akiwa mkeo headache tuu,kubali kushare!

Ni Hicho
 
Naomba uweke msisitizo kwenye neno ulilotumia "Kumdhuru" Kuhusu public wewe ulisema uchaggani...Ngoja nikupe mfano mmoja rahisi...Unaona wwengi wetu hapa wanadai timu hazikufika uwanjani...Nilipokuwa mtoto mdogo kabisa niliweza kuhudhuria mechi nyingi sana za timu ya chuo cha ushirika cha pale Moshi,kabla hata haipanda daraja la kwanza wakati huo.Nilishangazwa sana timu za Simba ama Yanga zikija pale basi uwanja unagawanyika mara mbili na kusema ukweli inakuwa kama timu ya nyumbani wako ugenini ama uwanja huru.Nilijiukiza ni kivipi watu wanazishabikia timu za nje...Ila ilikuwa tofauti sana timu nyingine zote zikija basi uwanja mzima ni Ushirika. Ni kwanini basi nimetowa mfano huo hapo juu? Si sahihi kusema tu eti Mengi hatapita huko uchaggani,ninaamini kabisa Mengi ana mashabiki almost nchi nzima,na Masha naye ni kiongozi wa kitaifa na kama ni public damage iwe mara ngapi? Uwanjani ni reference ya mahakamani.Siku saba zilikuwa vipi? Ndio maana nikasema ni kwa manufaa ya Lau kama anavyosema MKJJ kuwa ana hekima,yaishise hapo,ndio ilikuwa maana yangu.

Link: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/22689-waziri-masha-ajikanganya-6.html

Mjukuu wangu JMushi1, ni Nimetoa, na sio Nimetowa
 
Last edited:
Nimepewa taarifa na mjukuu'angu mmoja ya kwamba kuna uharibifu mkubwa sana wa lugha yetu ya kiswahili humu jamvini. Kwa hiyo nimekuja hapa kuwa adhibu wale wote wanaoharibu lugha yetu takatifu.

Mzee mwenzangu,
Kwanza,ninafurahi sana kuona kitu hiki kinatendeka hapa jamvini.
Sababu kuu ni kwamba,wengi wetu hujisahau na muda unapozidi kwenda,makosa haya huota mizizi na inakuwa vigumu kujirekebisha.

Pili,naomba msaada kwenye sehemu hizi (kutoka kwenye bandiko lako hapo juu)

Katika sentensi hiyo ya kwanza,ninaweza pia kutumia neno 'kwamba' bila kuweka 'ya' na ikaleta maana sahihi,si ndio?Sasa basi,kuna umuhimu gani kuwepo kwa 'ya'?Je?Kuna makosa yoyote iwapo ikitumika (kama ulivyofanya wewe)?

Kuwaadhibu,labda?
 
Shukrani mzee Suki,

Utumiaji wa ya kwamba au kwamba unaleta maana ile ile. Kwa hiyo, utangulizi wa "ya" kabla ya "kwamba" ni uongezaji wa ladha kwenye sentensi tu.

Mara nyingi tuna unganisha (tunaunganisha) maneno mawili na kuunda neno moja, kwa sababu uandishi wetu umejengwa na jinsi tunavyo ongea (tunavyoongea). Angalia mifano kwenye mabano. Sasa je sahihi ni "kuwa adhibu" au "kuwaadhibu," nafikiri hapo nitaomba msaada wa kuelimishwa hata mimi.
 
Kwa mtazamo wangu,kuunganisha au kutenganisha neno kunategemea sheria za lugha.Kwa mfano,neno ulilolitumia ''tunaunganisha'' hatuwezi kusema ''tuna unganisha'' kwani sheria za mnyambulisho wa neno hili haziruhusu.''Tuna'' ikitumika peke yake lazima ifuatiliwe na nomino.Kwa mfano;tuna watoto au tuna majukumu.
Vinginevyo matumizi mengine ya ''tuna'' yanafuatana na sehemu nyingine za maneno bila kuachanishwa na maneno hayo.Vivyo hivyo katika neno kuwaadhibu na mengineyo mengi.

Pia umegusia uandishi unaotegemea uongeaji wa mwandishi na sijaona kama hili ni tatizo katika muunganisho au mgawanyiko wa neno ingawa ni tatizo kubwa katika maeneo mengine mfano; ''kurikuwa'' badala ya ''kulikuwa'' na haya hujulikana kama makosa ya kimatamshi.
 
Hii ya kuakata maneno ni makosa makubwa.
usahihi wake ni kuunganisha kama ulivyoweka sio ulivyo weka kwenye mabano.
hebu niambie kama unaweza kutumia kama hivi: - mfano tunakwenda kazini haiwi sawa na kusema tuna kwenda kazini. tunakwenda ni neno moja kulikata ni makosa sawa na tunaunganisha ukasema tuna unganisha. neno tuna humaanisha kwamba msemaji akiwa yeye na wenzie kwa pamoja wanacho kitu cha pamoja, na kwa kawaida hufuatiwa na nomino mfano tutumie maneno yaleyale tunaunganisha ukilikata itatakiwa useme tuna unganisho( hapo tuna linamaanisha msemaji pamoja na wenzie wanalo unganisho yaani wanalojambo linalowafanya kuungana pamoja.unganisho limekuwa ni nomino).
 
Nakubaliana nanyi kabisa wajukuu zangu.

Naombeni muungane nami katika harakati hizi za kunyoosha lugha yetu humu jamvini.

Tuendelee....

Kuanzia jana nikiingia kwa mtandao wa Tanzania Daima. Napata "Auto Protect" ikionesha imeact kwa risk, na hiyo risk ni "Trojan.Maliframe!html", action ni kwamba risk imekuwa "Quarantined", kuna options za "clean" ama kudelete. Nikijaribu zote zinakataa.

Naomba msaada kwa anayejua hili tatizo, na jinsi ya kuliondoa.

Link: https://www.jamiiforums.com/technology-science-forum/22506-msaada-wakuu.html

Sio Ikionesha, ni Ikionyesha
 
Last edited:
Nakubaliana nanyi kabisa wajukuu zangu.

Naombeni muungane nami katika harakati hizi za kunyoosha lugha yetu humu jamvini.

Tuendelee....

Sio Ikionesha, ni Ikionyesha

Nadhani neno 'ikionesha' ni sahihi katika muktadha anaokusudia Mfumwa. Linatokana na neno 'ona'. Neno 'ikionyesha' kimantiki linatokana na neno 'onya'. Neno 'onya' lina maana ya kukanya. Katika muktadha wa Mfumwa, akitumia neno 'ikionyesha' haitaleta maana anayokusudia.

Angalia maneno haya pia:
'Maonesho' na si 'Maonyesho'
'Onesha' na si 'Onyesha'
 
Babu Mwanakijiji ni mwalimu wangu wa Kiswahili, na hayo uliyosema ni sawia na yale aliyonifundisha!

Ni 'maonesho' na si 'maonyesho'
 
Nyie wajukuu mbona mwataka niadhiri babu yenu?

Haya sasa, kwenye magazeti ya mzalendo huwa wanaandika "maonesho ya sabasaba" au "maonyesho ya sabasaba?"
 
Babu, wanatakiwa waandike 'maonesho' na siyo 'maonyesho', ni makosa yaliyo ya kawaida na kuzoeleka, ndiyo maana wengi hatuoni kama kufanya hivyo ni makosa.
 
Babu ulivyokazania huo ujukuu!
Ila ''kazana'' hii usiichukulie 'kimwinyimwinyi' maana watu wa lugha mh!

Ha si wajua tena ukishakula chumvi nyingi, kila mtu wamwita mjukuu. Weye ulishasema ni mzee mwenzangu. Kwa hiyo heshima yako nakutumia.
 
Nimepewa taarifa na mjukuu'angu mmoja ya kwamba kuna uharibifu mkubwa sana wa lugha yetu ya kiswahili humu jamvini. Kwa hiyo nimekuja hapa kuwa adhibu wale wote wanaoharibu lugha yetu takatifu.Nikianzia na hawa hapa:
Babu,

Kwa niaba yangu binafsi nakushukuru kwa ujio wako hapa jamvini,nadhani utasiadia sana katika kuboresha hii lugha yetu nzuri ya kiswahili na kwa kufanya hivyo sisi watumiaji tutarekebika katika maandishi yetu sawia na matamshi.

Lakini Babu tatizo langu liko hapo juu,kwenye bandiko lako ulipodai kwamba ''hii lugha yetu takatifu''
Tafadhali rekebisha au ni juze kuhusu hili la utakatifu wa kiswahili.

Ni mimi Mjukuu wako kama sio Kikongwe mwenzio.

SANDA
 
Hapa neno "tukufu" lingefaa zaidi. Labda kama Babu Swahili alikuwa na maana nyingine zaidi ya kuitukuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
 
Babu,

Kwa niaba yangu binafsi nakushukuru kwa ujio wako hapa jamvini,nadhani utasiadia sana katika kuboresha hii lugha yetu nzuri ya kiswahili na kwa kufanya hivyo sisi watumiaji tutarekebika katika maandishi yetu sawia na matamshi.

Lakini Babu tatizo langu liko hapo juu,kwenye bandiko lako ulipodai kwamba ''hii lugha yetu takatifu''
Tafadhali rekebisha au ni juze kuhusu hili la utakatifu wa kiswahili.

Ni mimi Mjukuu wako kama sio Kikongwe mwenzio.
Sanda Matuta,
Wewe binafsi unashukuru na si kwa niaba yako binafsi. Unaposema "kwa niaba" una maana ya kuwakilisha mtu mwingine lakini sio wewe mwenyewe. Huwezi kujiwakilisha kwa sababu ndiwe unayesema au kutenda - bila kuwakilishwa.

....ni juze... - ulikuwa na maana "nijuze", au?
Naomba kuwasilisha.
 
Last edited:
naona sasa wakati umefika kwa kila mmoja wetu kuhakikisha anatumia kiswahili fasaha.tupo pamoja katika hili
 
CUF at work , baada ya yale ya Mbeya sasa wamehamia kwenye makongamano.Hapa tuna amini kwamba Chadema ni wapinzani wa kweli na CUF wamekuwa wakitumika .Ushahidi tosha kabisa .Watanzania si wajinga na wataendelea na kuunga mkono Chadema.Hivi hili Mzee Jasusi Kongamano lilikuwa kwa ajili ya Chadema pekee ama maendeleo ya Waislam na maslahi katika vyama vya siasa ? Nimeshindwa kuelewa ama kwa vile sijasoma habari nzima maana nimepata kicgefu chefu kabla sijaenda mbali ?

Kutokana na utaalam wa mzee mwenzangu Suki, haya maneno yanapaswa kuunganisha na kuwa neno moja. Yaani Tunaamini.

Hivi hili Mzee Jasusi Kongamano lilikuwa kwa ajili ya Chadema pekee ama maendeleo ya Waislam na maslahi katika vyama vya siasa ?

Link: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...slam-nchini-kupinga-oparesheni-sangara-4.html

Swali hili halijakaa sawa...

Kianzio cha Hivi hili kinalenga kwa Mzee Jasusi, Kongamano au Mzee Jasusi Kongamano?

Swali hili lingepaswa kuwekwa hivi:

Mzee Jasusi, hivi hili kongamano lilikuwa kwa ajili........?
 
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom