Matumbawe pwani ya Tanzania hatarini kutoweka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,081
Matumbawe.jpg

Matumbawe



[FONT=ArialMT, sans-serif]Wataalamu wa sayansi ya baharini nchini wanaesema kwamba matumbawe katika mwambao wa Tanzania, hasa kisiwani Zanzibar yanakabiliwa na hatari ya kutoweka kutokana na udongo kutoka nchi kavu kuingia baharini na kuyafikia Mwandishi wetu anaeleza zaidi kutoka Zanzibar. [/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Wanasayansi kutoka Taasisi ya Sayansi za Baharini (IMS) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam chenye makao makuu yake Zanzibar, katika utafiti wao hivi karibuni wamesema tatizo la matumbawe baharini kuwa hatarini kutowekalinatokana na na kukithiri kwa uchafuzi wa mazingira, ikiwemo kwenye eneo za fukwe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mtafiti kutoka taasisi hiyo, Profesa Alfred Muzuka anasema udongo kutoka nchi kavu hivi sasa ni tishio kubwa kwa ustawi wa viumbe matumbawe na katika utafiti imebainika kwamba udongo huo huweza kusafiri kutoka ardhini hadi maeneo ya mbali baharini na kuathiri matumbawe ambayo ndiyo makaazi makubwa ya samaki.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Vumbi linalotoka katika barabara husafirishwa na maji ya mvua na kumwagwa baharini, ambapo matokeo yake ni uharibifu wa matumbawe, ambayo yana umuhimu mkubwa katika kulinda fukwe na viumbe vyengine baharini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Profesa Muzuka alisema kwa mfano katika visiwa vya Bawe na Chumbe hapa Zanzibar, ambavyo viko umbali mkubwa kutoka eneo la nchi kavu vipimo vilivyowekwa vilibainisha kuwepo kwa vumbi linalotokana na udongo kutoka nchi kavu, ikiwemo vumbi lililotolewa barababani..[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mtafiti huyo anasema iwapo hatua za haraka za kukabilina na athari hizo hazitachukuliwa, janga kubwa la kimazingira litatokea na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na ustawi wa jamii, kwa vile matumbawe hivi sasa yanafaida kubwa katika nyanja hizo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Prof. Muzuka anasema kwa kiasi kikubwa udongo au vumbi kutoka nchi kavu husababishwa na shughuli za kibinaadamu, na kutoa mfano hapa Zanzibar shughuli za ujenzi wa mitaro ya maji taka unaofanywa na Baraza la Manispaa Zanzibar, ambayo inaishia baharini ni mfano mmoja wapo wa vyanzo vya uharibifu wa matumbawe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Ukataji miti kiholela, ikiwemo mikoko hivi sasa linaendelea kuikumba Zanzibar na mwambao wa Tanzania Bara ambapo katika baadhi ya maeneo Tanzania Bara, takataka za sumu na mbolea kutoka mashambani hukokotwa na mvua hadi baharini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kwa upande wa Zanzibar, alisema imebainika miti ya mikoko inateketewa sana na baadhi ya watu kukata visiki vyake hung'olewa, hali ambayo husababisha udongo kuchukuliwa na maji hadi baharini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Matokeo ya utafiti katika visiwa vya Chumbe kilichopo kusini magharini mwa kisiwa cha Unguja na kisiwa cha Bawe kilichopo eneo la Magharibi ya bandari ya Zanzibar, umeonesha athari za wazi za vumbi la udongo kuganda kwenye matumbawe hayo na kuathiri viumbe vya baharini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa mujibu wa Profesa Muzuka, utafiti huo umefanywa na kituo hicho cha IMS, chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, na umehusisha maeneo ya ukanda wa Pwani nchini, ikiwemio Zanzibar, Tanga, Dar es Salaam na Mafia, lengo lake ni kugundua tishio la matumbawe kuathirika na kushauri njia muafaka za kudhibiti uharibifu wake.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Taarifa za utafiti huo, ambazo hivi karibuni zitawasilishwa kwa wadau na watunga sera za kuhifadhi mazingira, zitatoa msukumo mkubwa katika uhifadhi wa mazingira ya bahari na ukanda wa pwani, ambapo matumbawe hivi sasa yanakabiliwa na hatari kubwa ya kutoweka, licha ya kuvutia watalii na kukuza uchumi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Prof Muzuka anasema katika utafiti huo, mitego kadhaa ya kuhifadhia udongo iliwekwa katika maeneo ya matumbawe kwenye visiwa ya Chumbe na Bawe katika kipindi cha muda usiopungua miezi 21 na baadaye kupatikana matokeo ambayo yameweza kufanyiwa kazi na kubainika ukubwa wa tatizo hilo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Kiwango kikubwa cha udongo huo kwa matumbawe ya kisiwa cha Bawe anasema hukusanyika katika miezi ya Januari hadi Machi, lakini kwa upande wa matumbawe ya kisiwa cha Chumbe, udongo huo ulibainika kujitokeza kwa kasi katika miezi ya April hadi Septemba.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Hali hiyo kwa mujibu wa Prof. Muzuka inaweza kuwa imechangiwa na mabadiliko ya mwelekeo wa mkondo wa bahari, ambayo hubadilika kila muongo kutokana na mweleko wa pepo kama zile za Kusi na Kaskazi.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Mabadiliko hayo ndiyo chanzo cha mawimbi ya bahari kusababisha udongo huo hadi kwenye maeneo ya matumbawe.[/FONT]

”[FONT=ArialMT, sans-serif]Udongo kutoka ardhini unaathiri sana ukuaji wa matumbawe, hasa kwa baadhi ya aina za matumbawe, ikiwemo matumbawe aina ya milima, ambayo hupatikana zaidi katika kisiwa cha Bawe hapa Unguja”, anasema Profesa Muzuka.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Alieleza kwamba katika kisiwa cha Chumbe, ambacho licha ya athari hizo kujitokeza, hali siyo mabaya kama ilivyo katika kisiwa cha Bawe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Inawezekana hali hiyo inasababishwa na kuwa kisiwa cha Chumbe matumbawe yake mengi ni aina ya madole, ambayo kutokana na maumbile yake yanaonekana kuhimili zaidi athari kama hizo, kuliko yale ya milima ambaayo kwa wingi hupatikana katika kisiwa cha Bawe.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Matumbawe aina ya madole katika kisiwa cha Chumbe bado yanaonesha kuendelea kustawi vizuri na kuzaliana kwa wingi, hali inayoomaanisha yana uwezo mkubwa wa kukabiliana na zahama kama hizo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]"Lakini pia matumbawe katika kisiwa cha Chumbe yanahifadhiwa zaidi kuliko ilivyo katika kisiwa cha Bawe”, alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kisiwa cha Chumbe kimo chini ya hifadhi ambapo ni marufuku kwa shughuli za uvuvi, hali iliyochangia kuwa katika hali nzuri kimazingira na kuwepo ongezeko kubwa la matumbawe pamoja na aina mbali mbali za samaki.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sababu nyengine zinazochangia uharibifu wa matumbawe ni kama vile mabadiliko ya tabia nchi, umwagaji mafuta baharini kutoka kwenye meli pamoja na uvuvi usiojali utunzaji mazingira, kama vile nyavu za kukokota, uvuvi wa kutumia utupa na nyavu za matunduu madogo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, Serikali inakabiliwa na changamoto kubwa ya kutengeza barabara zake, ili ziwe katika kiwango cha lami, ili kuepusha udongo usifike maeneo ya baharini.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Tukumbuke kwamba matumbawe yana umuhimu mkubwa kwa maisha ya binaadamu, ikiwemo kukuza pato la wananchi hasa wanaoishi katika ukanda wa pwani, kwa vile kukosekana kwake pia kunasababisha samaki kupotea.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa maana hiyo wasimamizi wa sera na wananchi wote kuhakikisha matumbawe hayo yanabaki katika hali salama na yanaendelea kuzaa.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Lakini kwa kuwa matumbawe hivi sasa yameanza kutoweka kwa kasi kuna hata jamii ya wakaazi wa pwani kuanzisha utaratibu wa kupandikiza matumbawe, hasa baada ya kubainika kwamba yanastawi vizuri pale yanapopandikizwa kitaalamu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Tunaweza kuondoa tatizo la kupotea kwa matumbawe kwa kiasi kikubwa, iwapo wananchi watapewa utaalamu wa kupandikiza matumbawe, hasa utaratibu wa kutumia nyavu, kwasabau umeonekana hauna matatizo", alisema mtafiti mwengine wa Taaisi ya IMS, Dk. Chrostopher Muhando.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Kwa Zanzibar hivi sasa matumbawe ni kivutio kikubwa cha watalii, hasa kwa vile wastani wa watalii 100,000 hutembelea visiwa hivi kila msimu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Maeneo kama vile kisiwa cha Misali huko Pemba, kimeapata umaarufu mkubwa pamoja na kupokea wageni wengi kutokana na kuwa na matumbawe aina mbali mbali, pamoja na kuwa eneo maarufu la kuzaliwa viumbe kasa.[/FONT]



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom