Balantanda
JF-Expert Member
- Jul 13, 2008
- 12,476
- 4,752
Heshima mbele wakuu,mwaka 2008 ndo huoooo unakaribia kuisha,ni vema tukatumia nafasi hii kujikumbusha baadhi ya matukio ya kusisimua(ndani na nje ya Tanzania) ambayo yalitokea kwa mwaka 2008 na daima yatakuwa yakukumbukwa...
Mimi kwa kuanzia nina matukio takribani matano(05) kama ifuatavyo:-1.Mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Marekani(hasa ndani ya chama cha Democrats) ambao ulimalizika kwa Barack Hussein Obama kuweka historia kwa kuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kuchaguliwa kuwa Rais wa Marekani....2.Kitendo cha baadhi ya watuhumiwa wa ufisadi wa fedha za EPA kufikishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana baada ya muda mfupi....3.Kitendo cha mawaziri wastaafu waandamizi BASIL PESAMBILI MRAMBA,DANIEL YONA na aliyekuwa katibu mkuu GRAY MGONJA kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutumia vibaya madaraka yao na kuliingizia taifa hasara na kuachiwa kwa dhamana....4.Timu yetu ya Taifa ya mpira wa miguu(Taifa Stars) kupata tiketi kushiriki mashindano ya CHAN huko Ivory Coast mwezi February,2009....na tukio la mwisho kwangu kulikumbuka ni kitendo cha EDWARD NGOYAI LOWASSA kujiuzulu kuwa PM baada ya kutuhumiwa kujihusisha na mambo ya Ze Richmond...Ni hayo tu wakuu,tukumbushane mengine basi

Last edited by a moderator: