Matukio muhimu ya teknohama nchini 2010

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mwaka 2010 umekuwa wa kipekee kwa namna nyingi kwenye masuala ya teknohama nchini , umekuwa matukio mengi yaliyohusiana na teknohama nchini mengine ya kuharibu nchi na mengine ya kujenga nchi kwa ufupi nitaangalia yale ambayo yamechangia kujenga nchini na masuala mazima ya teknohama nchini .


SHULE ZA MSINGI KUUNGANISHWA NA INTERNET
Kampuni karibu 5 za kimataifa ziliahidi kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuunganisha shule za msingi kwenye mtandao kwa ajili ya masomo yao ya kila siku hapa nchini sijapata taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya mpango huu mpaka sasa hivi lakini naamini mambo yanaendelea kwa kasi kama mfumo wa mawasiliano unavyoendelea kusambazwa kwa kasi katika maeneo kadhaa nchini



WIZI WA FEDHA KWENYE MABENKI
Mwanzoni Mwa mwaka huu kulikuwa na habari kadhaa za watu kutuhumiwa kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao toka benki moja kwenda nyingine haswa nchi za nje ambapo kiasi kikubwa sana cha fedha kilichukuliwa
Pia kulikuwa na wale waliohamisha fedha toka mashirika ya umma kwenda kwenye account zao wenyewe au kampuni hewa haswa ile iliyohusu TTCL na TRA ambayo mpaka sasa bado iko kwenye vyombo vya dola .
Matukio hayo yameonyesha kuna tatizo kubwa kwenye suala zima la ulinzi na usimamizi wa kitknohama kwenye idara za fedha nchini hayo ni matukio yaliyotangazwa na kujulikana tu .
EPOCA
Wadau wengi wa teknohama wamekuwa wakilalamikia kuhusu kuwa na sheria za kiteknohama nchini zinazoendana na hali ya sasa ya mawasiliano nchini na dunia nzima kwa ujumla ย– mwaka huu kulipatikana sheria ya EPOCA ย– Electronic and Postal Communications Act hii ni sheria ya masuala ya mawasiliano na electroniki kwa wale wanaodhani kwenye mawasiliano yetu nchini hakuna sheria zozote mfano mzuri ni huo .
Hii haimaanishi kwamba sasa mawasiliano yako binafsi yatakuwa yanafuatiliwa na kurekodiwa kila unachofanya .


WATAALAMU WA TEKNOHAMA KUKUTANA
Ni siku chache tu zilizopita wadau mbalimbali wa teknohama nchini toka kwenye mashirika ya umma , vyuo , kampuni na sehemu kadhaa walikutana na waziri kujadili masuala mbalimbali ya teknohama nchini na maendeleo yake waziri ameahidi ndani ya miezi 3 ijayo ataandaa rasimu ya kuanzisha bodi ya teknohama nchini .


Kabla ya mkutano huu kulikuwa na ICT ROUND TABLE ingawa sina uhakika kama ICT ROUND TABLE inahusiana na mkutano uliokutanisha wadau na waziri husika .
Lakini baada ya ICT ROUND TABLE kumekuwa na masomo kadhaa yanayotolewa kwa mfumo wa mijadala chuo cha usimamizi wa fedha IFM .


Nyongeza yangu kwenye suala hili ni wakati sasa kwa serikali kupanga mikoa yote nchini kwa kanda za kiteknohama ili kule kwenye maendeleo duni ya teknohama pamoja na jamii za huko kuweze kupelekwa misaada zaidi na jitihada zaidi zifanyike haswa maeneo ya vijijini na maeneo ya kusini mwa Tanzania na kati .


VYOMBO VYA HABARI NA MFUMO WA DIGITALI
Hivi nani asiyependa kuwa na chaneli nyingi za televisheni kwenye luninga yake na tena ziwe zinaonekana bila chenga , kwa kutumia luninga hiyo aweze kutumia huduma zingine za interneti kwa gharama nafuu na kasi zaidi ?
Kwa taarifa zaidi gonga viunganishi hivi hapa
TCRA kuandaa umma kupokea mfumo wa digitali

Mchango wa maktaba mtandao katika sekta ya elimu

Basic Transmission yaruhusiwa kujenga mtandao wa mawasiliano

MATUMIZI YA TEKNOHAMA KWENYE UCHAGUZI
Mwaka huu tulikuwa na uchaguzi mkuu ambapo teknohama ilichukuwa nafasi kubwa sana katika kuhabarisha na kutoa elimu kwa baadhi ya wananchi kuhusu uchaguzi huu na wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi ingawa kulikuwa na matatizo kidogo haswa katika utoaji wa taarifa kwa muda .


Mfano kuna wagombea walienda baadhi ya maeneo kumwaka sera zao lakini hatukuweza kupata taarifa zao kwa muda kutokana na maeneo hayo kutokuwa na mtandao wa mawasiliano ya uhakika , wengine ni kutumia mitandao ya simu na huduma zingine kuchafua wengine na kupotosha umma kuhusu baadhi ya wagombea na sera zao .


Pamoja na matatizo hapo kuna mengi ya kujifunza na naamini kipindi kingine watu watakuwa makini zaidi katika kufanya kazi zao na kusimamia baadhi ya vitu haswa vinavyohusu mawasiliano ili kuepusha yale yaliyotokea kwenye suala zima la mawasiliano ya mwaka huu



MKONGA WA MAWASILIANO
Ujio wa mkonga umefungua milango mingi na nafasi nyingi za biashara na mawasiliano katika eneo zima la afrika mashariki pamoja na upunguzaji wa bei wa huduma za mawasiliano kama za internet , simu na nyingine zinazotumika kati ya eneo hili na mengine duniani , ingawa kumekuwa na changamoto nyingi haswa zinazohusu miundombinu na ulinzi wa miundo mbinu hiyo dhidi ya wahalifu na watu wengine wanaoweza kubomoa kwa ajili ya shuguli zao zingine .


Mfano wiki iliyopita mtandao ulikatika karibu nusu ya jiji la dar kuanzia maeneo ya mwenge ni kutokana na mafundi wa TANROAD kukata waya za mawasiliano walivyokuwa wanachimba barabara , kuna maeneo mengi nchini ambapo waya kama hizi zinapita ambapo kuna takiwa ulinzi na usalama wa kutosha na hata elimu ya kutosha kwa wahandisi wa fani nyingine kama wa barabara na maji ili wasiingiliane .


Hayo ndio maoni yangu kuhusu matukio muhimu ya kiteknohama kwa yaliyotokea nchini mwaka huu wa 2010 ,Naamini tunaweza kutumia matukio haya na mengine ambayo sijayataja katika kujiandaa kwa shuguli mbalimbali kwa siku zijazo .


Taarifa zaidi kuhusu matukio kama hayo na mengine mengi unaweza kutafuta kwenye mitandao mbalimbali na kuuliza kwa wadau mbalimbali .

Yona f maro
www.ictpub.blogspot.com
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom