Matokeo yametoka

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
Ni ya kidato cha Nne,matokeo yametoka,
Jamani njoo muone,mwenzenu nimeumbuka,
Busara ionekane,tushone palotatuka,
Matokeo yametoka,wakubwa wameumbuka.



Sifuri zimeniganda,ya siri yamefichuka,
Majukwaa nilipanda,mikakati sikuweka,
Sikujifunga makanda,umma uliponitaka,
Porojo mlikalia,mikakati ni sifuri.

Kila upande sifuri,mijini na vijijini,
Jamani hali si shwari,naona soni jamani,
Wezangu wamenawiri,ya kwao nayatamani,
Tafuta waliofeli,kama nawakwao wamo.

Niliona wachochezi, walio sema ukweli,
Mwanangu ana machozi,miaka mnne chali,
Hana tena mkombozi,ziro zina mkabili,
Maarifa hajapata,na cheti hatokipata.

Wa kwao wapo Savvana,na wani za kutakata,
Walimu wanapishana,si kule kwa katakata,
Maabara za kufana,kufaulu si matata,
Kwetu mwalimu mmoja,mshahara wa mashaka.

Kwa wapenda sifa,majina mkajiita,
Kumbe mwaua taifa,elimu gani mwa leta,
Taifa la zidi kufa,kama kura mmepata,
Mifano na kupatia,uone nimeumbuka,

Nchimbi kule musoma,257 walifanya,
164 sifuri mesimama,nani atayewaponya,
Mbona hamna huruma,tafuteni lakufanya,
Nawaomba wa baraza,muwapatie nakala.

Jakaya kule Manyara,130 walifanya,
Masifuri yameng'ara,76 kama nyanya,
Hizi data zinakera,nami ninazitawanya,
Kama elimu majina,hawa wangekuwa mbali
 
Kwa Isidori Shirima,86 walifanya,
72 wamepata sifuri,wametawanywa,
Nasema kwa lengo jema,mawazo yakiwa chanya,
Takwimu sijazipika,tafuta utazipata
 
Safi sana. Ushairi ni lugha ya moyoni. Ina hisia nyingi kwa sababu inatumia tamathali nyingi za usemi. Mimi napenda sana kwani huniamsha sana ari kutoka moyoni. Keep on.
 
Ni Jukwaa la siasa au miye nimepotea jukwaa?

Mi nadhani ni sawa, kwani wakati hawa jamaa wakifanya kampeni huwa wanaahidi Elimu, afya, uchumi bora etc....kwa hiyo baada ya uchaguzi inatakiwa watekeleze. And that's when this issue comin' in!
 
Mwache maskini aendelee kuwa maskini. Dar ya wenye pesa na wasomi imechagua CHADEMA (Kawe na Ubungo), maskini wameng'ang'ana na CCM. Sifuri kwa watoto wao sawa.
 
Back
Top Bottom