Matokeo ya Udiwani kata ya Lwezera Geita

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Wakuu,mimi niko kwenye kata ya Lwezera wilayani geita,hali huku siyo nzuri saana,ingawa zoezi la upigaji wa kura limeenda vyema isipokuwa tu jana usiku kuna mmoja wa makamanda alijeruhiwa vibaya sana kwa kukatwa mapanga alikimbizwa hospitalini kweli hali yake ni mbaya sana.

Hali hiyo ilikuja baada ya kudaiwa kwamba kamanda huyo aliongoza mshambulizi dhidi ya wakina mama wawili ambao walikuwa wamevaa sare za CCM jana jioni ambapo walipata kichapo kutoka kwa baadhi ya vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa cdm,wakina mama hao kwa sasa wamelazwa kwenye kituo cha afya cha Nzera.

Ilipofika usiku kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM walimvamia kamanda huyo na kutoa kipigo kikali ikiwa ni pamoja na kumjerugi kwa mapanga.

Baada ya muda mfupi kuanzia sasa nitaanza kuwajuza matokeo kwa sababu ndio wanamaliziamalizia kuhesabu kura.

tuko pamoja makamanda,lakini mwenye matokeo mahali pengine tujuzane.
 
Updates:Matokeo ya vituo 7 kati ya 20 CCM-392,CHADEMA-306,C.U.F-103 hii ni kwa mujibu wa Katibu wa CHADEMA wilaya ya Geita Rogers Luhega(Kamanda)
 
Kamanda msilale hadi kieleweke!MAANA HAWA MAGAMBA TUNAWAJUA SANA KWA UCHAKACHUAJI!
 
Twasubiri mkuu,ila poleni sana kwa maswaibu yaliyompata kama mwenzetu.Vipi huko hakuna polisi kwaajili ya ulinzi wa watu wake?!
 
Back
Top Bottom