Matokeo ya udiwani kata 23 (Oktoba 2, 2011)

ningependa kujua kama chadema ilikua inatetea au imechukua kata mpya?
 
Mi pia nawajua wagogo na mi pia no mgogo ila hao sasa waishio dom hawaambiliki juu ya CCM panatakuwa nguvu ya ziada pale

Sio kama unavyodhani mkuu. Waliopiga kura ni wale waliojiandikisha mwaka 2005. Dodoma imebadilika sana, vijana wamekua na mawazo mapya, maelfu ya watu wanahamia Dodoma kila kukicha, na uwepo wa UDOM unaifanya DDM kuwa tofauti na Dodoma ya zamani. Nakuhakikishia, daftari la wapiga kura likiboreshwa, hakuna uchaguzi CCM watashinda Dodoma mjini...
 
Aliyekuwa anataka source ni msimamizi wa uchaguzi jimboni Serengeti matokeo ni haya CDM 652, CCM 250, CUF 30.
 
Hicho kiti awali kilikuwa chini ya chama gani? itakuwa afya mkiweza kutuandalia list ya chaguzi zote na matokeo ya udiwani zilizofanyika leo.
 
Asante Mods, kuna nyuzi tofauti kadhaa tayari na matokeo nadhani tukiunganisha itapendeza. Wazo tu
 
Wakuu...wakati tukisubiri dakika tu ili CHADEMA itangazwe rasmi kama washindi wa ubunge IGUNGA tayari mgombea wa udiwani wa chadema kata ya masekelo manispaa ya shinyanga bw.MFUKO ametangazwa mshindi wa kata hiyo iliyoachwa wazi na marehemu shelembi magadula kwa kujinyakulia kura 1501 dhidi ya 587 za mgombea wa CCm bi rashida rajamu..
Kwa matokeo hayo ya zaidi ya 72% chadema imefanikiwa kutetea kiti chake kwa ushindi wa kimbunga..
Kazi kwenu magamba..
Nawasilisha
Mwendo mdundo kitaeleweka tu
 
huu ungese wako ndo unawafanya wa2 waifhkilie vibaya Cdm
Halafu eti mtu baadaye anataka hawa watu waichague CDM wakati tunawaona wajinga na ombaomba. hizi siasa za kijinga zitaiua CHADEMA. mimi mwenyewe ni mgogo jee ni OMBAOMBA?
 
Mungu endelea kutusimamia kwa haya tunayoyaomba kwako,kwani ni kweli kabisa naamini huja lala,hata hay tunayoendelea kutendewa na CCM-Magamba plus mafisadi unayaona na uayajua,kama sisi wanachi tunaangamia kwa kukosa maarifa basi utusaidie na utupe ujasir kila dakika iendayo ndani ya hii dunia ili siku ya siku tujikomboe.
Shukrani kwa wale walipgania haki na kisha wameshinda hizo kata za udiwani,wana FJ kwa mwenye taarifa rasmi za kule Arusha ambako walimteka kamanda wa CDM matokeo yakoje kwa taarifa zilizo rasmi?
Wengine leo hatulali mpaka tujue tumevuna nini katika uchaguzi wa Igunga na kwingineko kwenye uchaguzi wa udiwani,Niliwahi kusema hapa jamnvini kuwa pamoja na Kilango kwenda Masekelo kufanya kampeni asingeweza kusaidia kwani kule tayari wasingekuwa tayari kuirisha kata kwa CCM wakati hata marehemu Shelembi alishinda vyote udiwani na ubunge ila wakachakachua ubunge.
Tunaomba mwenye data atuhabarishe
 
Habari nilizozipata hivi sasa huko Katesh katika kata ya Endasaki CHADEMA imeshinda na watu wako mitaa wanasherekea ushindi huo!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sio kama unavyodhani mkuu. Waliopiga kura ni wale waliojiandikisha mwaka 2005. Dodoma imebadilika sana, vijana wamekua na mawazo mapya, maelfu ya watu wanahamia Dodoma kila kukicha, na uwepo wa UDOM unaifanya DDM kuwa tofauti na Dodoma ya zamani. Nakuhakikishia, daftari la wapiga kura likiboreshwa, hakuna uchaguzi CCM watashinda Dodoma mjini...

Umenisaidia kutoa maelezo mkuu
 
Back
Top Bottom