Matokeo ya Uchaguzi Mbeya

Inaonekana Kasheshe & Field Marshall mnawachukia sana CUF?

- Yaaani hoja zingine bwana hata pa-kuanzia kuzijibu ni taabu sana, yaani kutofautiana na mawazo yako mkuu on CUF, basi mimi ninaichukia CUF?
 
Naomba nifanye nukuu kutoka gazeti la NIPASHE, kichwa cha habari na sehemu ndogo ya maelezo.

"Wananchi wasusa uchaguzi Mbeya
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini umeweka historia mpya nchini kufuatia wananchi 82,927 ambao ni sawa na asilimia 65 ya watu 127,780 waliojiandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kukataa kushiriki kupiga kura kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo kwamba hakukuwa na mgombea wa chaguo lao.

Kutokana na msimamo huo, wananchi 44,855 ambao ni sawa na asilimia 35 ndio waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo ambao ulitawaliwa na kasoro kibao na hivyo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luckison Mwanjali, kuibuka mshindi kwa kupata kura 32,867 ambazo ni asilimia 73…………..."

Basi ndugu zangu, kama hali yenyewe ndiyo hiyo,je, Mbunge huyu ni halali?
Licha ya kuwa maelezo mengine toka kwa Bosi wa NEC, anasema, katika orodha ya wapigakura yalikuwemo hata majina ya ndugu waliotutangulia mbele ya haki (marehemu), mimi hili haliniingii kichwani. Sijaridhika kabisa na idadi hiyo; Nionavyo mimi ni kweli kabisa kuwa wananchi wamesusia uchaguzi huo.
Nimeamua kuliweka hadharani tulijadili.
 
Kichekesho zaidi ni kwamba kata anayotoka Mchungaji huyo, ya Utengule Usongwe, pale Mbalizi kwenye kitovu cha Kanisa lililomfikisha hapo alipo, walijiandikisha 25,354 lakini waliojitokeza ni 4117 TU!!!!

Kwa maana nyingine kakataliwa hata kwao. Huyu sio chaguo la wananchi, na ni wazi wananchi walisusisa, hawakutaka kubeba sime kama Tarime bali walitaka kuonyesha mgomo wa kistaarabu wa kuwakata wanafiki wa CCM na CUF.

Nimebahatika kumuona na kumsikiliza mgombea wa chadema aliyenguliwa, hakuwepo wa kupambana naye pale, ni kijana msomi, ana mvuto na uwezo mkubwa wa kushawishi. Lakini mbali ya hayo alishawaonyesha kwamba yeye ni mtoto wao aliyerudi nyumbani kuwatumikia kwani aliwatetea wananchi wa kijiji kimoja cha Isuto huko huko Mbeya Vijijini na kuigaragaraza serikali ambayo ilifikia hatua ya kuweka ndani diwani wao.
 
Naomba nifanye nukuu kutoka gazeti la NIPASHE, kichwa cha habari na sehemu ndogo ya maelezo.

“Wananchi wasusa uchaguzi Mbeya
Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini umeweka historia mpya nchini kufuatia wananchi 82,927 ambao ni sawa na asilimia 65 ya watu 127,780 waliojiandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kukataa kushiriki kupiga kura kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo kwamba hakukuwa na mgombea wa chaguo lao.

Kutokana na msimamo huo, wananchi 44,855 ambao ni sawa na asilimia 35 ndio waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo ambao ulitawaliwa na kasoro kibao na hivyo mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luckison Mwanjali, kuibuka mshindi kwa kupata kura 32,867 ambazo ni asilimia 73…………...”

Basi ndugu zangu, kama hali yenyewe ndiyo hiyo,je, Mbunge huyu ni halali?
Licha ya kuwa maelezo mengine toka kwa Bosi wa NEC, anasema, katika orodha ya wapigakura yalikuwemo hata majina ya ndugu waliotutangulia mbele ya haki (marehemu), mimi hili haliniingii kichwani. Sijaridhika kabisa na idadi hiyo; Nionavyo mimi ni kweli kabisa kuwa wananchi wamesusia uchaguzi huo.
Nimeamua kuliweka hadharani tulijadili.

Kwasababu Dataz ni tamu ukiwa na flexibility ya denominator; Mimi naona jamaa kashinda kwa kupata asilimia 25.7 ya watu waliokuwa na uwezo wa kupiga kura. [32,867/127,780]*100%

KWELI PIGA UA GARAGAZA UONGOZI ULIKUA LAZIMA UPATIKANE
 
2010 atashinda huyo huyo aliyeshinda juzi ... hapo ndipo utakapogundua kwamba uchambuzi uliotolewa hapo juu hauna maana yoyote ...
 
Kwasababu Dataz ni tamu ukiwa na flexibility ya denominator; Mimi naona jamaa kashinda kwa kupata asilimia 25.7 ya watu waliokuwa na uwezo wa kupiga kura. [32,867/127,780]*100%

KWELI PIGA UA GARAGAZA UONGOZI ULIKUA LAZIMA UPATIKANE

Bado Kipima joto cha ITV jana kilitoajibu la swali hili. "watu wengi hawakupiga kura kule mbeya, je watu wanafahamu umuhimu wa kupiga kura"? wengi walijibu NDIYO, Ili kupata maana halisi inahitaji ka-mini research kafanyike huko Mbeya
 
- JF bwana sometimes tunakuwa kama ze comedy, kwani sheria ya uchaguzi inasema nini kuhusu idadi ya wapiga kura?

-Kama wananchi hawaelewi umuhimu wa kupiga kura linaweza vipi kuwa tatizo la aliyeshinda? Unaposusia uchaguzi unayemuumiza ni nani hasa? Haya ni ya ajabu sana!
 
Duh... Hii Kali; sina hakika kuna mtu amezungumzia athari za kisheria kwa mshindi au mpiga kura. Kilichoonyeshwa hapo ni changamoto ya turn up ya wapiga kura.

Tupende tusipende... hicho ni kipima joto kwetu. People decided not to waste their time for whatever reasons na imeathiri uchaguzi kwa ujumla;
 
Kwa maana nyingine kakataliwa hata kwao. Huyu sio chaguo la wananchi, na ni wazi wananchi walisusisa, hawakutaka kubeba sime kama Tarime bali walitaka kuonyesha mgomo wa kistaarabu wa kuwakata wanafiki wa CCM na CUF.

Nimebahatika kumuona na kumsikiliza mgombea wa chadema aliyenguliwa, hakuwepo wa kupambana naye pale, ni kijana msomi, ana mvuto na uwezo mkubwa wa kushawishi. Lakini mbali ya hayo alishawaonyesha kwamba yeye ni mtoto wao aliyerudi nyumbani kuwatumikia kwani aliwatetea wananchi wa kijiji kimoja cha Isuto huko huko Mbeya Vijijini na kuigaragaraza serikali ambayo ilifikia hatua ya kuweka ndani diwani wao.

Hii si mara ya kwanza kwa wananchi kutojitokeza katika chaguzi kwa asilimia ile ile iliyojiandikisha. Mwaka 2000 Zanzibar walirudia uchaguzi wa kumchagua prez, wawakilishi na madiwani, na chama cha CUF kiligoma kushiriki tena uchaguzi huo, hivyo kubakia CCM na vyama vingine. Ni watu wachache sana ambao walikwenda kupiga kura tena.

Sababu zipo nyingi za watu kushindwa kwenda kupiga kura, mojawapo ni ya kuona waanae mtaka hatoshiriki tena na kundi kubwa ni lile ambalo linaona kuwa tayali mgombea wao ameshashinda hivyo hamna haja ya kwenda kupiga kura. Wengine ni kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya haki yao ya kupiga kura.

Sasa mtu unaposema ni kutokana na unafiki wa chama fulani inabidi utizamwe mara mbilimbili, isije ikawa ndio wale walevi wa tende aliosema JK hivi karibuni. Zaidi huyo mgombea wa Chadema uliyempamba naona hana sifa yoyote ile ya kuweza kuwa mwakilishi wa wananchi wa MBY vijijini.. Hii ni kutokana na ukihiyo wake wa sheria.
 
Duh... Hii Kali; sina hakika kuna mtu amezungumzia athari za kisheria kwa mshindi au mpiga kura. Kilichoonyeshwa hapo ni changamoto ya turn up ya wapiga kura.

- Swali langu ni what this has to do na mbunge aliyeshinda? Je hataingia bungeni? Na bungeni anaenda kumuwakilisha nani kama wananchi waligomea uchaguzi? The point ni kwamba wananchi wanaipenda sana Chadema ndio maana wamegoma kupiga kura, good sasa ilikuwaje mbunge aliyekufa akawa wa CCM? Changamoto ya turn up ya wapiga kura inabadili nini kwenye uwakilishwaji wa jimbo na mbunge aliyeshinda?

Tupende tusipende... hicho ni kipima joto kwetu. People decided not to waste their time for whatever reasons na imeathiri uchaguzi kwa ujumla;

- Hiki ni kipima joto chako wewe, lakini sio kwa JF nzima hapana Chadema inaposhinda huwa hatuleti filimbi, tunakubali na kusubiri uchaguzi mwingine ndio hasa kazi za vyama vya siasa, kwanza ni kushinda uchaguzi mengine baadaye, uchaguzi haukuathirika hata kidogo sheria zote zimetimizwa na huu uchaguzi na mbunge amechaguliwa, sasa hizi kelele za mlango zitasadia nini? Mtawaponza bure wananchi wa huko jim,boni ambao hawana kabisa hizi siasa za kutokomaa na ndio zinazowaponza CUF kule Pemba.

- Uchaguzi umeisha mbunge amechaguliwa, sasa tumsaidie aweze kuliwakilisha jimbo kwa makini na kujali waliopiga kura na wasiopiga kura. Hizi siasa za yanga na simba hatuzihitaji Tanzania.
 
Binafsi nawashukuru sana wananchi wa Mbeya kwa kuonyesha hali ya utulivu na amani. CCM imewashinda wananchi wa Mbeya kwa kutumia Jaji wa Baraza la Uchaguzi.

CCM ina kawaida hizo za kutumia vyombo vya taifa kulazimisha ushindi. Wanaweza kufanya hivyo kwani viongozi wao ndio wanawateua wakuu wa vyombo hivyo. Ilitakiwa wateuliwe na kamati huru (za Bunge au za vyama vyote).

Amani ni muhimu. Inatisha tunaposikia watu wanatupia mawe magari ya viongozi. Hata kama CCM ikihujumu haki ya wananchi kuchagua wagombea wa Chadema, ni lazima tuendelee kutumia njia za amani kupinga hilo.

Kuhodhi madaraka kunakofanywa na CCM ndio kitu kinatishia amani ya Tanzania kwa kiasi kikubwa kuliko vitu vingine vyote
 
Wakuu zangu tusijenge sababu zetu wenyewe kujaribu kupotosha Umma..Hatuwezi kabisa kusema wananchi wamegoma kupiga kura ktk uchaguzi mdogo Mbeya vijijini kwa sababu ya mgombea wa Chadema.. Yawezekana kabisa vita kati ya vyama hivi (Upinzani) ndiyo sababu kubwa ya watu kutopiga kura ama sababu kubwa inayojulikana duniani kuwa siku zote Uchaguzi ndogo hutokea asilimia ndogo wa wananchi walioandikisha ktk daftari la wapiga kura..
Hapa canada majuzi tu kulitokea uchaguzi mdogo na asilimi chini ya 60 walijitokeza kupiga kura. Ni hesabu ndogo ktk historia ya nchi hii kltk chaguzi zote sasa sielewi kulikuwepo na mgombea gani ambaye walimtaka hakutokea..Tazma hesabu ya chaguzi zote ndogo utaona kuwa hesabu ya wapiga kura sio sawa na ile ya uchaguzi mkuu..
Chadema wamechemsha Mbeya hilo ni wazi na mimi naamini kabisa tumefanya kmakosa makubwa sana kuanzisha vita ambavyo nina hakika hatuwezi kushinda!..
 
- Mkuu Bob, hapo tupo pamoja sana, uchaguzi ukiisha wastaarabu huanza kazi ya kujenga nyufa za kampeni na kuwa kitu kimoja kwa faida ya jimbo, hizi siasa za uganga njaaa kwamba haki na uchaguzi wa halali inakuwa ni pale tu Chadema wakishinda hatuwezi kuzikubali Tanzania,

- Shitambala is the biggest joke of our political time, Mwanasheria kutojua sheria sasa ataongoza vipi katika kipindi hiki cha kuelekea kujaribu kubadilika na sheria? Tusubiri uchaguzi uajo huu umekwisha na Chadema wawe waaangalifu next time, mwenyekiti anakwenda kwenye uchaguzi wa diwani na kelele nyingi lakini wanashindwa anyways, tatizo la political strategy huko upande wa pili!
 
Prof Baregu (Seasoned Tanzanian Political Scientist) amesema sababu za kidanganyifu zilitumika kumwengua mgombea wa Chadema. Nakubaliana na mawazo yake. Flimsy technicality was used to remove the Chadema candidate.

Tunawasifu wananchi wa Mbeya kwa kuwa watulivu. Wamesema, kwa kupitia kiongozi wao wa kimila, kwamba chaguo lao lilikuwa ni mgombea wa Chadema. Wamenyimwa fursa ya kuwakilishwa na wanayempenda na bado wakatulia. Thanks be to them!
 
- Mbunge mpya wa Mbeya kuapishwa wiki hiii, Tanzania hatuwezi kuwa na viongozi wasiojua sheria za uchaguzi, infact this is a biggest political embarrassment ever, chaguo la wananchi wa Mbeya uchgauzi uliopita alikuwa ni RIP Nyaulawa(CCM), na this time arround another CCM candidate,

- Professor Baregu, kutoka Mlimani waliotuambia Muungwana ni chaguo letu wananchi wote wa Tanzania kwenye polls uchwara wakishinikizwa na na Kingunge, this time tunatakiwa kuamini kwamba he is right anaposema tatizo la Mbeya halikuwa sheria, ile something else maana tumelala sana wananchi wa nji hii,

Uchaguzi umefanyika mgombea wa CCM ameshinda, the rest mjini huwa tunaita kelele za mlango!
 
Mh. Kibunango, hata kama huyo Sambwee ni kihiyo kwa mtazamo wako sawa, lakini wananchi wa Mbeya Vijijini ndivyo wanavyosema kwamba ndiye waliyemtaka na wamethibitisha hilo kwa wengi kutokwenda piga kura.

Viongozi wao wa kimila walisha tamka kupitia kiongozi wao na akaripotiwa na vyombo vya habari, suala si kumlilia huyo mgombea wa chadema, suala hapa wananchi wamenyimwa nafasi ya kumchagua kiongozi wanyemhitaji kutokana na sheria zilizopitwa na wakati zenye na zenye kupunguza ukuaji wa demokrasia ya kweli.

Wananchi wengi wilayani himoo wanaeleza wazi kwamba wanahitaji mabadiliko na wamechoshwa na ccm, na hata huyo Sambwee angegombea kupitia CCM wanasema wasingempaparikia.

Kero yao kubwa ikiwa kupanda kwa bei ya mbolea ambayo wanalazimika kununua hadi 130,000. Ikimbukwe kwamba wananchi wa wilaya hiyo ni wakulima wa mazao ya chakula kwa asilimia 100 hivyo kwao mbolea ni bidhaa muhimu sana kwa wakulima hawa.
 
Matokeo ya Uchaguzi yanaoshenya kwamba wananchi wameupuuzia ule Uchaguzi. Lakini taathira yake ni kwamba,baada ya Chadema kutolewa,na watu kuususia ule Uchaguzi,hili labda ni jambo ambalo lina maana kwamba,katika Uchaguzi ujao,
itafanya wananchi wawe na hamu kubwa zaidi ya kushiriki katika Uchaguzi.
 
- Leo pia nimechukua time kuwauliza wahusika wa huu uchaguzi, kuanzia tume mpaka wa CCM nini kilichojiri na namba ya wananchi kuwa ndogo? Jibu nililopewa ni kwamba:-

- Katika historia ya by-election yoyote duniani haijawahi kutokea turn-out ya zaidi ya 40%, infact UK huwa haizidi hata 20% kwa hiyo huku Mbeya hakuna cha ajabu,

ingawa mkuu wa CCM aliniambia hivi kua "hata sisi tuliposhindwa Tarime, tulijaribu kutafuta kila sababu ya kutokea", akasema "infact hata mimi ningekua upinzani ningesema exactly wanachokisema sasa kuhusu turn-out".

Ahsante Wakuu.
 
Kimsingi kutokuwepo kwa CHADEMA katika uchaguzi huu mdogo wa Mbeya vijijini kwa kiasi fulani kulipunguza idadi ya watu kujitokeza kupiga kura.So ni vizuri(kama nilivyoshauri na wengine walivyoshauri awali) CHADEMA wakawachukulia hatua za kinidhamu wale wote walioshiriki kusababisha uzembe wa kijinga kama huu uliofanyika Mbeya(akiwemo mgombea Mwanasheria SHITAMBALA) ili liwe fundisho na kuwafanya watendaji wote wa chama wawe makini katika uchaguzi mkuu wa mwakani...Pia kwa vile uchaguzi wa Mbeya vijijini tayari umemalizika,ni vizuri tukaachana na yale yote yanayohusiana na uchaguzi huo badala yake vyama vikatumia muda uliobaki kwa ajili ya kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwakani(mikakati ya ushindi) badala ya kusubiri mwaka 2010 ufike na kufanya maandalizi ya zimamoto...Huu ni wakati wa kuanza kuangalia ni nani atagombea na kushinda kihalali(kukubalika kwa wananchi) na si wakati wa kuanza kukusanya hela za kutoa rushwa ili ushinde katika uchaguzi huo mkuu...Huu ni wakati wa vyama vyote vyenye nia ya kushiriki katika uchaguzi huo mkuu kufanyia kazi/kusahihisha makosa yote yaliyopelekea vishindwe katika chaguzi zilizopita...Vilevile huu ni wakati kwa CHADEMA kujiimarisha katika ngazi za mikoa,wilaya,tarafa,kata,vijiji na shina(kama ilivyo katika chama tawala CCM) ili kuleta upinzani na ushindani wenye uwiano tofauti na ilivyo sasa(Hii ni pamoja na kuandaa bajeti ambayo kipaumbele chake kitakuwa ni kuimarisha kama sio kuanzisha matawi ya wilayani na vijijini ambako ndiko wapiga kura wengi wapo) ,Pia ni wakati wa CUF kujiimarisha zaidi Tanzania bara kama ilivyojiimarsha PEMBA,lengo kama nilivyosema hapo awali ni kuwa na upinzani wa kisiasa wenye uwiano hasa bungeni na katika halmashauri za wilaya,miji,manispaa na majiji(maendeleo yatakuja kwa kasi ya ajabu mno)...Aidha ni wakati wa chama tawala CCM kukaa na kujisafisha ili kiwe safi(japo kiasi) kinapoingia katika uchaguzi mkuu wa mwakani,hapa nina maana kwamba CCM kiandae wagombea walio wasafi,wanaokubalika kwa wananchi na si wanaoingia madarakani kwa kutoa rushwa ama wale ambao wanasifika kwa kuwa na sifa maarufu ya UFISADI...Mwisho ni wakati kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC) na pia Bunge kukaa chini na kuifanyia marekebisho sheria ya uchaguzi ili kuepukana na malalamiko ya mara kwa mara ambayo ni matokeo ya mapungufu ya sheria hiyo(kama ilivyotokea katika uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini)
 
-
- Katika historia ya by-election yoyote duniani haijawahi kutokea turn-out ya zaidi ya 40%, infact UK huwa haizidi hata 20% kwa hiyo huku Mbeya hakuna cha ajabu

Mkuu FMES

Hii kauli tata hebu nipe shule kidogo...Mbeya was so obvious wanapiga kura hawakuwa na chaguo, imenikumbusha ile enzi za Jembe na nyundo ama picha na kivuli ama nyumba na something, nadhani wakumbuka hizo changuzi enzi za mwalimu. Kilichotokea Jamhuri ya watu wa Mbeya ni wananchi kutoona umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa mgombea wasiye mpenda.....ndo maana turn out ilikuwa ndogo vile. Tusikimbilie historia kusimulate mambo ya Tz

respect

Ushi
 
Back
Top Bottom