Matokeo ya tafiti yadhibitiwe - Serikali

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,465
1,170
Serikali yaagiza matokeo ya tafiti yadhibitiwe
Thursday, 30 September 2010 19:26
James Magai


Source: Mwananchi

KUKIWA na tuhuma za kuzuiwa kutangaza matokeo ya tafiti za kisiasa, serikali imesema inajipanga kuweka mkakati wa kuhakikisha Chama cha Wanatakwimu (TAST) kinadhibiti matokeo ya tafiti zinazofanywa na taasisi zisizo za kiserikali au watu binafsi ili kuhakikisha kuwa ni sahihi.

Katika siku za karibuni matokeo ya tafiti zilizofanywa na taasisi binafsi kuhusu hali ya kisiasa zilipingwa na baadhi ya wanasiasa ambao baadhi wanadai vigezo vilivyotumiki havikidhi utashi wa kisayansi kutokana na kuhusisha watu wachache na hivyo kutoa picha tofauti na hali halisi.

Pia Chadema ilidai hivi karibuni kuwa taasisi ya Synovate ilitishwa na chama tawala na kuamua kutotoa matokeo ya utafiti wake kuhusu mgombea wa urais anayekubalika zaidi kwa sasa. Synovate imekana kufanya utafiti kama huo.

Jana, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Takwimu ya Taifa(NBS), Dk Albina Chuwa alitangaza mkakati wa kudhiti taarifa za matokeo ya tafiti zinazohusu umma wakati akizungumza na wandishi wa habari kwenye mkutano wa TAST jijini Dar es Salaam. Dk Chuwa alikuwa akiunga mkono kauli ya mgeni rasmi katika mkutano huo, Omar Mzee, ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi aliyezungumzia udhaifu wa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa katika tafiti nyingi zinazofanywa na taasisi zisizo za kiserikali.

Alisema mkutano huo wa jana wa chama hicho ambacho alisema kilikuwa kimeanza kulegalega ni chachu ya kuboresha matumizi ya takwimu katika tafiti. “Kufufuliwa kwa chama hiki kutaboresha matumizi ya takwimu katika tafiti. Sasa tutahakikisha kuwa maadili ya matumizi ya takwimu katika tafiti yanafuatwa," alisdema.

Tutahakikisha kuwa takwimu za tafiti kwa ajili ya matumizi ya umma zinathibitishwa na ili kujiridhisha kama ziko sahihi,” alisisitiza Chuwa. Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri Mzee alikiagiza chama hicho kusimamia na kuhakikisha kuwa takwimu zinazotolewa katika tafiti mbalimbali ni sahihi na zinakidhi maadili ya matumizi ya takwimu.

Naibu waziri huyo, ambaye pia kitaaluma ni mtakwimu, alisema tafiti nyingi zinazofanyika nchini zinafanyika kiholela pasipo mpangilio, jambo ambalo halikidhi matwakwa ya tafiti. Alisema leo hii kuna tafiti ambazo zinafanyika kwa kuhusisha watu 10 lakini zinajumuisha watu 200,000 kama vile ndio msimamo wao wote, jambo ambalo si sahihi. “Kwa nini tunaacha tafiti hizi zisizo na mpangilio. Tusiayaache haya.



Sisi ndio tunapaswa kuwaelekeza nini cha kufanya ili kuhakikisha kuwa takwimu zinazotolewa ni sahihi. Huwezi kutumia sampuli ya watu 10 kwa matokeo ya wilaya nzima,” alisema naibu waziri huyo. Kutokana na tatizo hilo, Mzee alisema kila mtu anaweza kufanya utafiti kwa matumizi yake binafsi, lakini tafiti zinazofanywa kwa ajili ya matumizi ya taifa lazima takwimu zake ziwe zimepitiwa na kuthibitishwa na Idara ya Takwimu ya Taifa.

Pia Mzee alikitaka chama hicho kuziunganisha sekta za umma na sekta binafsi katika matumizi ya takwimu kwa kuwa ndio watumiaj wakubwa wa takwimu. “Ninyi ni wazalishaji na private sector (sekta binafsi) ni consumer (watumiaji).

Sasa mnakutana vipi... mnakutana? Je, ipo forum (jukwaa) ya kuwakutanisha," alihoji. "Bila kuwa na forum ni matatizo. Angalieni namna ya kukutana nao ili nao wawaeleze maoni yao. Muandae vikao vya mara kwa mara na watumiaji ili nao watuambie maoni yao vinginevyo tutazalisha tu bila watumiaji.”

My Take:

Juzi juzi tu walikuwa wanasifia Synovate iliposema JK na CCM wanakubalika (Kama mnamkumbuka Makamba) now the tide is againts them tafiti zidhibitiwe. Serikali na CCM wanaishi karne ya ngapi????

Utahakiki vipi kwamba takwimu ni za kweli? Si inabidi ukafanye tena research as such in maana ni serikali tu ndiyo inaruhusiwa kufanya credible research in Tanzania. What a joke???????

Hiyo nchi itaacha lini uendawazimu????? And someone tells me JK atashinda kwa kishindo na hakuna mpinzani wa kumkaribia. Sasa matukio haya yanamaanisha nini?????
 
Hivi REDET imeishia wapi? Mbona wao hawajatoa matokeo ya uchunguzi wao wa maoni? Hata Majira katika uchunguzi wao wanaonyesha Slaa akiongoza.
 
Piga ua REDET haiwezi kutoa matokeo ya uchunguzi. mnataka mkandala apoteze u-VC? labda itoe uchunguzi wa magazeti yapi sanasomwa na kununuliwa sana siyo nani anakubalika katika wagombea urais
 
ccm wanachakachua hata utafiti ambao upo wazi....................ccm acheni kuwatesa watz na pesa za epa mlizokwapua kwa kuwafanya washindwe kufanya kazi zao sawasawa...........na nyie watendaji husika mnashindwaje kuwa professional?
 
ccm wanachakachua hata utafiti ambao upo wazi....................ccm acheni kuwatesa watz na pesa za epa mlizokwapua kwa kuwafanya washindwe kufanya kazi zao sawasawa...........na nyie watendaji husika mnashindwaje kuwa professional?

Mijitu ya kuja imejua hilo neno "kuchakachua" basi kila mtu anataka aonekane anajua kulitumia. Shida kweri kweri :tonguez:
 
Hivi kumbe Tz kuna chama cha takwimu? ha ha ha ha, siku zote wako wapi.Hii inachekesha sana, hawa watu wanatakiwa wawe wanatupa data za mara kwa mara kwa mfano rate of unemployment in the country, confidency of the people over their govt, satisfaction of how things are going in the country etc. Sasa wanasubiri uchaguzi ndo wanaanza uchakachuaji what a shame?
 
Mtenda anapoTENDWA

Kwani serikali ilikuwa wapi wakati REDET ilipokuwa inatoa tafiti mfululizo kuhusu kukubalika kwa muungwana na CCM? Au kwa kuwa matokeo ya tafiti hizo yalikuwa in favour of the current administration?

Nasikia Mukandara anajiandaa kupata nafasi serikali, katibu mkuu? mbunge wa kuteuliwa? au Waziri? may be not kwa kuwa REDET haijasaidia kitu sasa.
 
Kwani serikali ilikuwa wapi wakati REDET ilipokuwa inatoa tafiti mfululizo kuhusu kukubalika kwa muungwana na CCM? Au kwa kuwa matokeo ya tafiti hizo yalikuwa in favour of the current administration?

Nasikia Mukandara anajiandaa kupata nafasi serikali, katibu mkuu? mbunge wa kuteuliwa? au Waziri? may be not kwa kuwa REDET haijasaidia kitu sasa.

Kwa kweli inashangaza!!!!!!!!!!!!
 
Aibu ya CCM ya Kikwete.

Siku hizi kumbe watu wanaweza kukutana hata kunywa kahawa na kula kashata wakaanza kutoa vitisho?
 
Back
Top Bottom