matokeo ya shule nabii japhet mungira ya efatha sec school s.4197 wamefeli wote kasoro wa2

swala ni kwamba weng hamfahamu kuhusu Efatha shule hiyo tumeinunua mwaka jana shutuma hizo apewe aliye tuuzia alaf kitu kingine kuweni na nidhamu juu ya hich chombo cha Efatha na Mtume Mwingira matokeo ya hiyo shule ni mwakan ndo mtaongea

Hata kama mmeinunua, inamaana mlishindwa kutia bidii ili walimu wafundishe watoto ipasavyo kama mlivyotia bidii kudai ada za watoto mpaka wengine kutishiwa kufukuzwa shule!Kwa nini mliangalia sana input kwa maana ya income kuliko output kwa maana ya mafunzo stadi!...Afu kufaulu kwa wanafunzi ndo kunauza jina la shule na hivyo kuendelea kupata wanafunzi wengi na income kuongezeka. Sasa kaka unasema tusubili mwakani huoni kwamba matokeo haya tayari yasharudisha nyuma jina la shule na kuna uwezekano wazazi wakaamisha watoto wao (labda kwa wale amabao ni washirika wa EFATA ndo wanawezakuwabakisha) na ama msipate wanafunzi mliokuwa mmekusudia kuwapata wa kidato cha kwanza na wale wanao hamia!
 
Mbona hii haiendani na mwenendo wa Efatha?

Huyu mwingira mwenyewe ana elimu gani? Je, ana historia ya kufaulu? Unafikiri kama unaweza KUKEMEA MAPEPO HATA MTIHANI UNAFAULU?. EFATHA ina utaalamu gani wa kuendesha shule?
 
Du,
Mtume alisahau kuwaombea na kuwapa upako wa kufaulu mtihani wanafunzi wake.
Namshauri apitie upya sifa na uwezo wa Walimu wake.
 
Wengi wanashangaa, wanamponda Mwingira kama kwamba sylabus iliyotunga mtihani ni yake Mwingira. Hiyo ndo elimu ya Bongo! Pamoja na shule kuwa ya Efata chumba cha mtihani wanatakiwa kujibu maswali, sio kuomba na kusifu! Matatizo ya walimu ni kilio cha kila shule! Ukistaajabu ya Musa utaona ya Filauni Angalia hii. KIBUTA SEC. DIV 1 - 0, DIV 2 - 0, DIV 3 - 0, DIV 4 - 6, FAILED 80!
 
swala ni kwamba weng hamfahamu kuhusu Efatha shule hiyo tumeinunua mwaka jana shutuma hizo apewe aliye tuuzia alaf kitu kingine kuweni na nidhamu juu ya hich chombo cha Efatha na Mtume Mwingira matokeo ya hiyo shule ni mwakan ndo mtaongea

Mkuu mliiinunua mwaka jana tusubiri matokeo ya mwakani? kwenye mtihani wa form three au four? au mna mpango wa kuiba mtihani?Nisaidie kwa hilo mkuu
 
huyu ndiye nabii mchungaji josephat mungira wa kanisa efatha la mwenge matokeo ya shule yake ni
division one-o,division two-2,division 3-2,divison 1v--121 na zero--157

Naomba mtoa mada akafanye uchunguzi upya kuhusu taarifa hii kwa sababu hii si shule ya josephat mungira, ila tu inaitwa Efatha secondary school kwa sababu chanzo chake ni sehemu ambayo mwanzo lilikuwa jengo la kusali watu wa efatha ministry mkoani Iringa na si shule ya dini kama mnavyodhani. Mimi nimefundisha pale mwaka 2010 ni wanafunzi waliokuwa mtaani kwa muda mrefu hivyo wakaamua kwenda kusoma, wengine ni wakumbwa kuliko hata walimu wao. Ni kama reseaters ndio wanaosoma pale...............
 
Hii si shule ya Mtume na Nabii Josephat Elias Mwingira. Shule ya Mtume na nabii ipo Kibaha siyo Iringa na inajulikana kwa jina la Efatha Seminary wala si Efatha Sekondari
 
Back
Top Bottom