Matokeo ya Nagu yakibatilishwa, Dr. Slaa kugombea?

Putting the horse before the cart...................who knows mahakama itatengua matokeo hayo?.....na harakati za uraisi sasa je? Hivi Dr. Slaa anaishi karatu au Hanang? Hii sasa si itakuwa Dr. Slaa naye kajidhalilisha na kuwa Capertbagger............The how low can Chadema now stoops?............
acha mambo ya ajabu katiba inaruhusu Mtanzania yeyote kushiriki ubunge katika jimbo lolote nchini si lazma awe anaishi hapo! as long as anakubalika
 
dr.+slaa.bmp



chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kina mpango wa kukata kiu ya ‘waliomisi’ uwepo wa dk. Willibrod slaa bungeni kwa kumuingiza kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika wakati wowote.

Chadema, kinajipanga zaidi kumuingiza slaa bungeni kupitia jimbo la hanang ambalo tayari kimekwishawasilisha pingamizi mahakamani kutaka matokeo yaliyomtangaza mary nagu (ccm) mshindi yabatilishwe.

Habari za uhakika zinasema kuwa endapo mahakama itabatilisha uchaguzi wa hanang, slaa atagombea katika uchaguzi mdogo na kuna uhakika wa asilimia mia moja kwamba atashinda.


mkurugenzi wa vijana wa chadema alilikaririwa akisema mjini dodoma hivi karibuni kuwa aliyegombea hanang, rose kamili tayari ni mbunge viti maalum, kwahiyo slaa anaweza kugombea na kushinda.

“nafasi ni kama hizo, kuna uchaguzi mdogo unakuja, slaa akigombea sehemu yoyote atashinda,” alisema mbunge wa ubungo mheshimiwa john mnyika


mimi naona aachane namasuala ya ubunge kwa sasa ashughulikie na masuala ya kujenga chama, tunamsubiri 2015 kwa nguvu mpya na hata wakiiba tena kura bado hazitawatosha hiyo tutakuweka juu zaidi dr. Wa ukweli
 
Ni mpango mzuri lakini unahitaji mkakati wa hali ya juu sana kwa kuwa Dr Slaa akishindwa ubunge umaarufu wake unaweza kushuka. Kesi iko mahakamani hakuna anaejua kama chadema watashinda kwa hali hiyo jimbo la Hanang haliwezi kuzungumzwa kama vile kama liko wazi.

atashinda! wakumbuka mrema pale Temeke?
 
atashinda! wakumbuka mrema pale Temeke?

Lakini baada ya kina Mrema na Cheyo, nilishawahi kusikia kuwa utaratibu huu haupo tena.
Ukigombea urais huuhusiwi kugombea ubunge ktk uchaguzi huo hupo. ofcoz sina hakika sana lakini hiyo kitu nilishawahi kuisikia.
 
hii ni injini mimi naiamini inaenda kuchukua jimbo ,kuhusu kutumikia chama tunao watu wengi wanaoweza kufanya kazi hiyo kama akina wilfred rwakatare wa bukoba mjini akina mpenda zoe wapo vijana wengi cha maana ni kuwapa tu direction msiogope sisi ni wapambanaji mi naamini huyu jamaa hawezi shindwa pale
 
Duu hata kesi yenyewe sijui kama imefunguliwa licha ya kuanza halafu watu wanasema jamaa atashinda!!!!!!!!!!!!
 
Huu ni uwongo.


NAZIDI KUSISITIZA TUTASOMA TAARIFA NYINGI HAPA JF ZISIZORASMI JUU YA CHADEMA NA VIONGOZI WAKE,KWANI TAYARI WAPO WATU WAMEPEWA PESA KUFANYA PROPAGANDA ZA KIUANDISHI.


nyie acheni bwana Slaa hayuko after madaraka,yuko kwa ajili wa kuhakikisha mtanzania anaishi maisha yanayoeleweka,maisha ya uongozi ni hatua,kamaliza hatua ya ubunge hayuko tayari kurudi nyuma.

Tunakumbuka wote alisisitiza atafanya kazi ya kujenga chama,kuhakikisha halmashauri zilizopatikana zinafanya wonders na mwisho kuwasaidia na kuwalea wabunge wake wafikie utimilifu wa maono yao.
 
Rais....Rais....Rais wa Umma....!

Hii ni Mashine...UWONGO MBAYA...!

Nadhani...afadhali abaki kama mteule wa wananchi, akijenge chama, azunguke nchi nzima, taifa zima linamhitaji sana aongee hata kidogo mbele zao ktk mikutano ya hadhara....
 
Kwa maoni yangu asgombee ajikite zaidi katika kukijenga chama bse CCM usiku na mchana wanajipanga kukiangusha CHADEMA
 
afadhali slaa awe mbunge ili aje kula kiapo bungeni kuwa mtiifu kwa rais wa jamhuri na kuilinda katiba!!!!!
hongera slaa kwa kukubali kushiriki kugombea ubunge!!!
 
Jamani tumwachie Mungu aliyemuandaa mtu huyu kwa ajili ya ya wadanganyika, kumfunga nyau wa porini kengere ni kazi, lkn yy ameonyesha yuko tayari kabisa kumfunga hata kwa kupoteza uhai wake,kama si DR leo CDM kingepata wabunge wachache sn, japo wengi wameibiwa kura zao kama wangetangaza kwa haki basi CDM kingekuwa na wa bunge zaidi ya 50 mwaka huu, kama akipewa nafasi ya kurudi mjengoni basi wana wa nchi hii watapata nafasi zaidi ya kumsikia, na km CDM wakimsimamisha tena 2015, itakuwa heri ameongeza umaarufu wake,
Let God do HIS merciful ways to TZs.
 
Nitapenda sana iwe hivyooo......duu bunge litakuwa sio la kusinzia na kupitisha upuuzi tenaa..litakuwa bunge la mijadala...na la haki kwenda mbele.....
 
akigombea na kushinda maana yake hilo jimbo litaendelea kuwa la chadema ata kama 2015 akirudi kwenye urais........hapa ileweke vita ni kutafuta pa kusema huku ukiwa na kinga pamoja na kuongeza ruzuku kwa chama........WATU WANAPENDA CHANGAMOTO ZA SLAA KILA ANAPOONGEA NA SANASANA ANAPOWABANA SERIKALI!kUMSIMAMISHA mbunge mwingine yoyote kupitia chademA MBALI NA ROSE kwa hanang atakosa...NI KIJIJINI KULE...NIMEKAA MIEZI 6.......ILIKUWA CCM NA ROSE MWENYEWE KATOKEA CCM.....KWA MAANA INGINE HATUNA MTU STRONG WA KUMSIMAMISHA......
SLAA AKIRUDI BUNGENI UWEZEKANO NI MKUBWA MNO WA KUWAMWAGA CCM 2015..................
MABOMU YATAKUWA MAKUBWA BILA UWOGA HUKU WAKIMZIMA ZITO WAKATI AKITAKA KUANZA UJINGA WAKE MAANA DOGO NAE SIO WETU TENA .........KAMA HAMJUI ZITO KACHAKACHULIWA NGOJENI MUONE HUKO MBELE MTANIKUBALIA......CCM WANATAFUTA PA KUINGILIA NA NADHAN NI KUPITIA KWA ZITO NA SHIBUDA......ILA WATAZIMWA TU.......CHADEMA KUNA VICHWA PALE JUU NA TUNACHOONA SISI SASA WENYEWE WAMESHAONA ZAMANI
 
Putting the horse before the cart...................who knows mahakama itatengua matokeo hayo?.....na harakati za uraisi sasa je? Hivi Dr. Slaa anaishi karatu au Hanang? Hii sasa si itakuwa Dr. Slaa naye kajidhalilisha na kuwa Capertbagger............The how low can Chadema now stoops?............

Mbunge Mteule wa Babati mjini, ni mkuria aliyekataliwa Tarime (Chambili), hawa Wambulu wamempa ubunge; Wambulu wa Hanang hawezi kushindwa kumpa Dr Slaa kura. However, I must agree that this will be stooping too low for CHADEMA. I dont expect it!
 
Dr.Slaa hana sababu ya kugombea ubunge tena maana atakuwa hana tofauti na MREMA mwenye uchu wa kula posho za ubunge. Dr. sasa ajikite kuijenga chama na hadhi yake itaendelea kuwa kubwa kuliko kuwa mbunge. Maana Mwenyekiti yuko bungeni, naibu jatibu Bungeni sasa nani atajenga chama km wote wakiingia humo mjengoni.

Mie nadhani Dr. achape kazi kuongeza nguvu ya chama hasa vijijini ambako uelewa bado ni ZERO!

sie tuko nyuma yake na tutamsaidia

Nawasilisha
 
Putting the horse before the cart...................who knows mahakama itatengua matokeo hayo?.....na harakati za uraisi sasa je? Hivi Dr. Slaa anaishi karatu au Hanang? Hii sasa si itakuwa Dr. Slaa naye kajidhalilisha na kuwa Capertbagger............The how low can Chadema now stoops?............
Hapana mkuu anahaki kugombea kama matokeo yakitenguliwa na Mahakama,Kumbuka Mrema aligombea Temeke na alishinda, John Memose Cheyo aligombea Magu na akashinda kwa hiyo banafsi sioni tatizo hapo.
 
Nilithani CDM inakabiliwa na changamoto nyingi zaidi kuliko kuongeza mbunge mmoja bungeni....... mwee! niambieni ninani anaweza kuzikabili changamoto hizo zaidi ya Dr. Slaa
 
unategemea ya Mrema 1995 temeke yatokee lwa Dr S. la hasha hana tamaa ya kuingia bungeni alikokaa for 15 years.
 
Lakini baada ya kina Mrema na Cheyo, nilishawahi kusikia kuwa utaratibu huu haupo tena.
Ukigombea urais huuhusiwi kugombea ubunge ktk uchaguzi huo hupo. ofcoz sina hakika sana lakini hiyo kitu nilishawahi kuisikia.

I think you have to take some minutes and look at the constitution, ijapokua ni ngumu sana kuielewa
 
Back
Top Bottom