Dk Jakaya Mrisho Kikwete ametangazwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuibuka na jumla ya kura 5,276,827 sawa na asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa. Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA ametangazwa mshindi wa pili kwa kupata kura 2,276,827 sawa na asilimia 26.3 na Profesa Ibrahim Haruna Lipumba wa CUF amekuwa mshindi wa tatu kwa kura 695,667 sawa na asilmia 8.06.