Matokeo ya Maalim Seif Kumtambua Karume

Karume amekua raisi tokea mwaka 2000. Aka pata nafasi ya kuongoza kipindi cha pili mwaka 2005. Sasa ana kuja kumtambua leo wakati kabakiza chini ya mwaka katika uraisi wake? Na hata asinpo utambua uraisi wake je inge badilisha chochote? There must be something deeper involved here.
 
Mkuu Zitto heshima mbele,

Hapo ndo tunasema hapa kuwa upinzani mlitakiwa kuseize hii opportunity na kumobilise umma tayari kwa 2010.

wakati CCM wakiparurana huko, hapa tulitegemea alternatives kama Chadema muwe mitaani mkiwaeleza watu kinagaubaga ni nini kinaendelea nchi hii na incompetence ya huu utawala uliopo. Maana si wananchi wengi wenye access ya habari/taarifa kama ilivyo hapa JF.

Lakini, ndio kwanza Maalim yupo Ikulu anaweka mambo yake sawa na mh Karume, huku mkuu kama wewe tunayekutegemea bungeni nasikia upo Jordan kwenye mkutano, sijasikia viongozi wengine wa Chadema wanasemaje kwenye hili!

Mi nilidhani hii ni a golden window of opportunity kwa upinzani Tanzania kuonyesha makali yake!

Watu waelezwe nini mkuu? Mambo yote yanayotokea mimi sitegemei kama kuna mtu ambaye atakosa kuyaelewa (unless he/she is dumbly idiot!)... which is the case with most of us..... Tanzanians...
 
Kaizer, umesema kweli mkuu. Tumebakiwa na miezi 7 tu kuvunjwa bunge na kuanza kampeni za uchaguzi mwezi Julai. Hivyo itakuwa vigumu kufanya mikutano ya hadhara kuanzia Mei kutokana na vyama kuwa bize ktk michakato ya kupata wagombea. Kwa upande mwingine Serikali/Polisi watakuwa wazito kutoa vibali vya mikutano kwasababu wanasubiri muda rasmi wa kampeni.

Kwa kuangalia hayo kuna miaezi 4 tu ya kutimiza aliyoyasema Dr. Slaa kwamba Richmond, Kiwira, ticts etc wanazipeleka kwa wananchi baada ya kushindikana bungeni. Hali ya CCM ni mahututi kabisa huu ni wakati wa operation sangara na zinduka.

Swali langu kwa CUF na CHADEMA operation hizo zimeishia wapi? Wito wangu kwenu huu ndiyo wakati wa kuvua sangara, huu ndiyo wakati wa kuzindua. Mnatu-let down sana. https://www.jamiiforums.com/members/kaizer.html
 
Watu waelezwe nini mkuu? Mambo yote yanayotokea mimi sitegemei kama kuna mtu ambaye atakosa kuyaelewa (unless he/she is dumbly idiot!)... which is the case with most of us..... Tanzanians...

Mkuu, nimekupata, mana hasa ni kwamba watu kwa mamilioni hawajui nini hasa kinaendelea, kwa maana wamezoea redio ni moja ya taifa, na magazeti ndo hivyo hayafiki sehemu zote na umasikini uanwafanya wengine waone kama ni anasa. Na hapa ndipo ninapoona potential ya watu kama kina Zitto!
 
Kaizer, umesema kweli mkuu. Tumebakiwa na miezi 7 tu kuvunjwa bunge na kuanza kampeni za uchaguzi mwezi Julai. Hivyo itakuwa vigumu kufanya mikutano ya hadhara kuanzia Mei kutokana na vyama kuwa bize ktk michakato ya kupata wagombea. Kwa upande mwingine Serikali/Polisi watakuwa wazito kutoa vibali vya mikutano kwasababu wanasubiri muda rasmi wa kampeni.

Kwa kuangalia hayo kuna miaezi 4 tu ya kutimiza aliyoyasema Dr. Slaa kwamba Richmond, Kiwira, ticts etc wanazipeleka kwa wananchi baada ya kushindikana bungeni. Hali ya CCM ni mahututi kabisa huu ni wakati wa operation sangara na zinduka.

Swali langu kwa CUF na CHADEMA operation hizo zimeishia wapi? Wito wangu kwenu huu ndiyo wakati wa kuvua sangara, huu ndiyo wakati wa kuzindua. Mnatu-let down sana.

Kabisa mkuu haoa tupo ukurasa mmoja, ubarikiwe sana...exactly ndicho nilichomhoji Mh.Zitto hapa,

Imekuwa kama wamemwagiwa maji...nilitegemea baada ya timbilitimbwili la uchaguzi Chadema waendelee kuvua sangara wao, hata kwa kuchangisha wananchi najua isingeshindikana, CUF nao wangeendelea kuzindua watu, lakini ndo kwanza Maalim anazindukia Ikulu! can u get it mkuu? Yaani kuua tembo kwa ubua tu, lakini hakuna kinachoendelea!
 
Tatizo la Seif ni njaa, amekuwa kama call box hafanyikazi mpaka utie pesa!

Kishaahidiwa fungu, ofisi, gari, ving'ora nk basi anawatosa wenzie. Kazi kweli kweli.....
 
Si kweli kwa hili Mkuu,
Imeonekana kuwa bila ya umoja wa Wazanzibari mengi hayatopiga hatua,hivyo imeamuliwa watu wameze viburi vyao na kujitolea muhanga,kuachana na maslahi binafsi...tuelekee kuijenga Zanzibar kwa umoja wetu jambo ambalo linawezekana...na tumeanza BLW...na tunategemea tutakuwa pamoja katika mambo tunayofanana kimaslahi...kwa wananchi wote. CCM wakitugeuka tena Wazanzibari watakuwa mahakimu tunakwenda kwa nia safi(political will)...na Wazanzibar watakua mashahidi kuwa tupo pamoja nao...na mnafiki atajitokeza mwenyewe na kutengwa.Usifkiri mkutano huo ulikuwa wa ghafla...mchakato ulikuwa mrefu...mikutano ya siri ilikuwa mingi ndo maana hata waandishi wa habari wameipata dakika za mwisho.
 
Mkuu unaamini CCM ni wa kweli? mara ngapi wameenda kinyume na makubaliano na muafaka? Kimebadilika nini sasa?

Changa la macho!
 
Mara ngapi wananchi wazanzibar wamekuwa mashahidi ndugu? hapa mtavurugwa na wapenda vyeo..siungi mkono hii move...dawa ya CCM ni jino kwa jino...otherwise ni kanyaboa lol. let wait and see another kilio..
 
Naamini CCM si wakweli...mkutano wa Seif na Karume...mbali na kuwa ni presha za wafadhili lakini ni hitaji la Wazanzibari...mara hii wamekubali kuwa watahukumu wenyewe.Kwa kuwa weshachoka na shida za maisha zinazosababishwa na misuguano ya kisiasa isiyokwisha...wakati wenzetu huko wanatafunana.

Siasa za Zanzibar zinamazonge mengi ndg kila nafasi lazima ipewe advantage,hatubahatishi, na tunajuwa kilichotokea kaitka muwafaka 1&2,lakini hatuwezi kusema kuwa kwa matokeo hayo yote,tusiipe nafasi hatua hii kwa maendeleo ya demokrasia
 
Kwa hiyo chama kipi ndo cha upinzani Zanzibar?. Kama hawa wameamua kuungana nani atampinga mwenzie?
 
Naamini CCM si wakweli...mkutano wa Seif na Karume...mbali na kuwa ni presha za wafadhili lakini ni hitaji la Wazanzibari...mara hii wamekubali kuwa watahukumu wenyewe.Kwa kuwa weshachoka na shida za maisha zinazosababishwa na misuguano ya kisiasa isiyokwisha...wakati wenzetu huko wanatafunana.

Siasa za Zanzibar zinamazonge mengi ndg kila nafasi lazima ipewe advantage,hatubahatishi, na tunajuwa kilichotokea kaitka muwafaka 1&2,lakini hatuwezi kusema kuwa kwa matokeo hayo yote,tusiipe nafasi hatua hii kwa maendeleo ya demokrasia
kwa kubali kukaa meza moja jamaa ndio wameshawapiga janga la macho..kilio hicho...wacha kudanganya watu hapa JF..huo utakuwa upuuzi wa mwisho kuufanya ..kuwaamini CCM..jino kwa jino ingewaaibisha sana..lol
 
Upinzani kati ya CAF na CCM Zanzibar unaelekea kufa kama bado upo ila kinachooneka kuzaliwa ni upinzani wa Zanzibar dhidi ya Tanzania bara na matunda ya huu upinzani ni kupatikana kwa Taifa lililo huru la Zanzibar na baada ya hapo ndipo U CAF na U CCM utarudi mahala pake.
 
hapana muungano ndugu ni ushirikiano for common purposes
Kwa maana hiyo CUF wameyakubali mabaya yote ya CCM na CCM yameyakubali mabaya yote ya CUF je kuna maana yoyote ya CUF kwenda mitaani (oparesheni zinduka) na kuwaambia wananchi kuwa CCM ni chama kisichofaa?. Je kipi kinachofuata kwa CUF barua zote walizoandikia UN about CCM watazi withdraw?
 
kwa kubali kukaa meza moja jamaa ndio wameshawapiga janga la macho..kilio hicho...wacha kudanganya watu hapa JF..huo utakuwa upuuzi wa mwisho kuufanya ..kuwaamini CCM..jino kwa jino ingewaaibisha sana..lol
sasa siasa za kusuguana tu kila siku zinakufikisheni wapi....tunapozungumza matatizo ya zanzibar katika muungano...tunajuwa kuwa Zanzibar yenyewe kwnza ni tatizo,hivyo, narejea tena kuwa...hatua yoyote ya kuleta umoja wa wazanzibari tunaiunga mkono...ili tusonge mbele...hakuna adui au rafiki wa kudumu katika siasa...tuna matatizo mengi tunahitaji kutafakari kwa pamoja hasa katika mambo tunayofanana kimtazamo kwa maslahi ya zanzibar...najuwa maadui zetu hawapendi but we have swallowed our prides...and move on.
Kwa maana hiyo CUF wameyakubali mabaya yote ya CCM na CCM yameyakubali mabaya yote ya CUF je kuna maana yoyote ya CUF kwenda mitaani (oparesheni zinduka) na kuwaambia wananchi kuwa CCM ni chama kisichofaa?. Je kipi kinachofuata kwa CUF barua zote walizoandikia UN about CCM watazi withdraw?
Politics is dirty game,waafrika ndo mmezoeshwa hivyo...ndo maana nashangaa kwa baadhi ya watu kujidai wana mikono safi katika siasa...siasa za vurugu si faida kwa yoyote...kwa hali yetu tunahitaji umoja kwa gharama yoyote ikibidi hata kuvunja vyama vyetu ni sawa tu.
 
- Pasco, una maana hizi siku zote CUF walikuwa hawamtambui Karume? Are you serious mkuu wangu au?

- Una maana walikuwa hawaendi bungeni au kwenye Baraza la Wawakilishi ambako Karume ni makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar?

Respect.

FMEs!
Mkuu FMES,
Katiba ya Zanzibar inamtaka rais wa ZnZ ateue angalau wawakilishi wawili kwenye toka CUF kwenye ZEK na Barazani baada ya majadiliano na uongozi wa CUF.
Baada ya uchaguzi 2005, CUF ikapeleka majina yake 4 kwa Karume ili achague mawili ya barazani. Karume akawaita CUF wajadiliane majina yapi, CUF wakakataa kwa kushikilia msimamo hawamtambua Karume.

Karume nae ni jeuri, kiburi, ukijumlisha na whisky kichwani, akagoma katakata kuteua. Just stalmate. Huku wawakilishi wa CUF wakiiingia barazani kushiriki vikao mpaka kuipongeza serikali ya Zanzibar kuwa ni De-Facto (serikali ya kinyume na sheria) na sio De-jure (Serikali kwa mujibu wa Sheria).

Hili tangazo la leo ndilo la kwanza la CUF kuithibitisha serikali ya Karume kuwa ni De-jure. Hivyo kauli ya jino kwa jino imefutika rasmi pamoja na zile kelele zao zote za kupokwa tonge mdomoni, yaani CUF wamekubali walishindwa na mshindi ni Karume, hivyo uhasama wote kwisha.

Mambo yangu yakiwa mazuri, next week natinga ZnZ, Pemba specifically kupima upepo wa impact ya utambuzi huu, na insha-allah nitawaletea nitakayo yashuhudia.
 
Nafikiri kwa wale wanaoijua siasa Tanzania iko katika spot light kuwa ni nchi ya amani ila doa la Zanzibar lili mu hunt Mkapa , na Linaharibu image ya Kikwete na ndio ukaona Wakati Kikwete alipokua USA alipotoa kauli ya kuwa Mgogoro wa Zanzibar unashughulikiwa ni kuwa Zanzibar iko katika sport light katika East Afrika kuwa Zanzibar ikikosa stability basi Tanzania pia haitokua na amani.
Hakuna hata mmoja mwenye akili timamu atakesema kuwa tuwagonganishe Wazanzibari ili tuendelee kuwatawala , la kujiuliza jee Wazanzibari si Watanzania wenzenu kama , wazanaki au Wachaga au Wanyachusa ?
Tanzania inahitaji viongozi imara na ukweli usiofichika Kikwete amewafelisha Wazazinzibari kama Hilary Clinton alivyofeli last week kuwaweka pamoja Waisrail na Wapalestina na kumfanya Rais wa Palestine kuamua kutogombea tena Urais .
Zanzibar ikiwa prosperous ni neema ya Watanzania kwani kila mtu alikua akiend shopping Zenj week end wakati Zanzibar ilipokua na uongozi afadhali kidogo , Zanzibar ikiwa ni njema kila mtu atanuafaika.
 
karume keshachoshwa na ngonjera za wabongo na kujipapatua hawezi kwavile sera za chama zinambana soooo anahitaji kibega kutoka kwa maalim seif na cuf. na maalim seif keshajua kwamba kiubabe ubabe ccm haiondoki madarakani bora aende nayo kimpera mpera na soo anahitaji kibega kutoka kwa rais ili angalau kuwe na imani ya serikali ya mseto au tume ya mseto, na wote wawili washajua kwamba wazanzibari wanagonganishwa vichwa sooo inabidi watulie ili nchi igomboke. kaeni mkao wa kula . kuna big bang itatokea kabla uchaguzi wa mwakani. bravo seif na karume. bravo zenji! na watanganyika eleweni kwamba kugomboka kwa zenji ndio kuogomboka kwa tanganyika. bravo tanganyika! our beloved brothers!
 
Mkuu FMES,
Katiba ya Zanzibar inamtaka rais wa ZnZ ateue angalau wawakilishi wawili kwenye toka CUF kwenye ZEK na Barazani baada ya majadiliano na uongozi wa CUF.
Baada ya uchaguzi 2005, CUF ikapeleka majina yake 4 kwa Karume ili achague mawili ya barazani. Karume akawaita CUF wajadiliane majina yapi, CUF wakakataa kwa kushikilia msimamo hawamtambua Karume.

Karume nae ni jeuri, kiburi, ukijumlisha na whisky kichwani, akagoma katakata kuteua. Just stalmate. Huku wawakilishi wa CUF wakiiingia barazani kushiriki vikao mpaka kuipongeza serikali ya Zanzibar kuwa ni De-Facto (serikali ya kinyume na sheria) na sio De-jure (Serikali kwa mujibu wa Sheria).

Hili tangazo la leo ndilo la kwanza la CUF kuithibitisha serikali ya Karume kuwa ni De-jure. Hivyo kauli ya jino kwa jino imefutika rasmi pamoja na zile kelele zao zote za kupokwa tonge mdomoni, yaani CUF wamekubali walishindwa na mshindi ni Karume, hivyo uhasama wote kwisha.

Mambo yangu yakiwa mazuri, next week natinga ZnZ, Pemba specifically kupima upepo wa impact ya utambuzi huu, na insha-allah nitawaletea nitakayo yashuhudia.

Pasco unanifanya niipende JF. Sio leo tu. Kila mara post zako ni za kina sana. You are very objective, thoughtful and informative. Keep it up brother!
 
Back
Top Bottom