Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Na hilo Tinga Tinga la CCM limeangushwa, basi sasa naanza kuamini Uchaguzi mwaka huu utashangaza wengi.
 
Harison Mwakyembe anaongoza ktk vituo 50 kwa kura 4,901 George Mwakalinga 417 Elius Mwakalinga 262, Elius Mwanjala kura 227, Rhoda Mwamunyange 109 (Awali nilisema unarudiwa, hapana, zilikuwa ni taarifa zisizokamilika, nimerekebisha), vituo vilivyobaki ni vichache, ni wazi Mwakyembe atashinda!

Hapa nilitaka kukuona unaplay comedy, aksante kwa kusahihisha.
 
Halafu huko Kyela bila jina lako kuwa "Mwa"-somebody ina maana ndio usahau kabisa ubunge eeh?
 
Kama nilivyoahidi:

NAMPA HONGERA DR. MWAKYEMBE KWA KUSHINDA KURA ZA MAONI HUKO KYELA.

Ninaamini safari hii ukirudi bungeni, utakuwa mkali zaidi kwani utafahamu kuwa Mwakalinga yupo pembeni.

Ila ombea Mungu asihamie CHADEMA maana mpambano utakuwa mkali zaidi na Dr. Slaa akiwa na Mwakalinga.

Hatimaye sasa itakuwa rahisi kumwambia Mwakalinga ahamie CHADEMA.

Yote tisa, kumi ni DR. SLAA FOR PRESIDENT 2010.
 
Lakini haya ni matokeo ya kura za maoni za kuomba uteuzi. CC na NEC wanaweza kuwaruka washindi/walioongoza na wakachukua walioshika nafasi za pili na tatu. Kumbukeni yaliyomfika Aden Rage (Tabora Mjini) na Adamjee (Kawe). Jamaa walioongoza, lakini wakapigwa chini na nafasi zao kuchukuliwa na Prof. Mgombelo (Tabora Mjini) na Rita Mlaki (Kawe).

Kwa hiyo lolote linaweza kutokea na hasa kwa kutumia kivuli cha waliohusishwa na tuhuma za rushwa.
 
HONGERA MWAKYEMBE KWA USHINDI wa jimbo la KYELA.

La muhimu mwaka huu ni DR. SLAA AWE RAIS WA TANZANIA.
 
Huku Musoma Mathayo kachukuwa tena kama amesamama mbali na kuwa na watu tisa kwenye mchakato
 
Wakuu hivi Dar hakukuwa na kura za maoni leo? Matokeo yake hayasikiki na ndo jiji lenyewe
 
Lakini Tinga tinga si alisema wananchi wa Mtera bado wanamuhitaji?
 
Lakini haya ni matokeo ya kura za maoni za kuomba uteuzi. CC na NEC wanaweza kuwaruka washindi/walioongoza na wakachukua walioshika nafasi za pili na tatu. Kumbukeni yaliyomfika Aden Rage (Tabora Mjini) na Adamjee (Kawe). Jamaa walioongoza, lakini wakapigwa chini na nafasi zao kuchukuliwa na Prof. Mgombelo (Tabora Mjini) na Rita Mlaki (Kawe).

Kwa hiyo lolote linaweza kutokea na hasa kwa kutumia kivuli cha waliohusishwa na tuhuma za rushwa.

Mzee Malecela hawezi kushindwa uchaguzi Mtera kwa kura ya maoni....CC na NEC watarudisha jina lake na huyo aliyeshinda kweli jimboni atapozwa na cheo fulani serikalini.

Malecela will go when he is ready!!

Watch this space.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom