Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Ubungo kura za maoni zapigwa upya


PostDateIcon.png
Wednesday, 04 August 2010 05:18

Na WaWetuandishi
MCHAKATO wa kuwatafuta wagombea ubunge katika majimbo manane ya Mkoa wa Dar es Salaam, umeendelea kukumbwa na vituko vya rushwa za hapa na pale na kulazimisha Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) kufanya doria usiku kucha na kuwatia mbaroni wapambe 14 wa mmoja wa wagombea.

Wakati TAKUKUTRU wakiwakamata wapambe hao 14 maofisa wa taasisi hiyo wameponea chupuchupu kupigwa na baadhi ya wapambe wa wagombea hao baada ya kuzingirwa na kundi la wapambe na kulazimika kuomba msaada wa Jeshi la Polisi.

Matukio ya rushwa yalionekana kutawala zaidi katika Jimbo la Ubungo huku mmoja wa wagombea akitajwa kugawa fedha waziwazi na kutumia jina la Rais Jakaya Kikwete, kuwaomba wana CCM wa matawi ya Makabe na Msumi A na B kutomwacha kwa madai kuwa itakuwa aibu kwa mwenyekiti huyo wa CCM kwa kuwa anamtaka.

Majira ilishuhudia maofisa zaidi ya wanane wa TAKUKURU wa Kinondoni wakiwa na magari mawili wakizunguka maeneo ya upigaji kura tangu asubuhi hadi saa 10 jioni huku kukiwa na wasiwasi wa wapambe wa mgombea huyo kuwazunguka.

"Hali ni mbaya sana, hivi nchi hii imefikia hatua ya mtu asiyekuwa na fedha kutopewa uongozi hata kama anafaa?," alihoji Bi. Mary Mwaisope aliyejitambulisha kuwa kada wa CCM anayekerwa na rushwa.
"Leo hapa watu hawajalala, usiku kucha kulikuwa na mshikemshike wa kugawa fedha na kanga, hata sasa unaona TAKUKURU wanavyozunguka hali ni mbaya sana, angalia magari ya kifahari yanavyoleta watu hapa bila kujua wanafuata nini na wanatoka wapi," alisema.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Bw. John Kabale alithibitisha kukamatwa kwa watu 14 katika eneo la Makabe na mtu mmoja kutoka eneo la Mkongeni kwa tuhuma za rushwa katika msako uliofanyika usiku wa kumkia jana.
"Baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa matukio ya rushwa tulijipanga na kuanza doria, tulifanikiwa kuwatia mbaroni watu 14 katika eneo la Makabe na Msumi A na B, baada ya kuona tumezungukwa sana na watu wengi nilimpigia simu RCO (Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa) wa Mkoa wa Kinondoni alitusaidia kwa haraka sana.

Baada ya kuwahoji watuhumiwa tunaendelea kutafuta ushaidi, tukipata tutawahoji wagombea maana ni wajanja kweli wanatumia wapambe, wao wanakaa mbali.

"Tuliwakamata na sh. 380,000 wakiwa wanajiandaa kuanza kuwagongea wapiga kura na kuwagawiwa nyumba kwa nyumba, wengine walikimbia kwa kutumia gari namba T640 BBC na kutokomea kabisa," alisema Bw. Kabale

Aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano kwa kutoa taarifa na vyombo vya habari hususan gazeti la Majira kuendelea kufuatilia kwa karibu matukio ya rushwa katika mchakato wa kura za maoni na kuweka wazi kwamba tabia hiyo inapaswa kuendelea bila kukoma.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya wana-CCM waliwatupia lawama viongozi wao wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni kushindwa kusimamia taratibu za kura za maoni na kuhoji uhalali wa eneo hilo la Makabe yenye wanachama zaidi ya 800 na msumi A na B kushindwa kupiga kura kwa kucheleweshewa masanduku.

Walisema kitendo hicho ni dalili ya viongozi hao kumbeba mmoja wa wagombea anayetuhumiwa kutoa rushwa na kutumia jina la Rais Kikwete kuwarubuni wananchi kumpigia kura huku wakitishia kukihama chama hicho iwapo matokeo yatakwenda kinyume na matarajio yao.

Walisema hawaoni sababu ya maeneo ya Kibamba ambayo ni mbali zaidi kufikishikiwa vifaa mapema siku ya Jumapili huku wahusika wakiruka eneo lao na kuleta vifaa saa tisa jioni, hivyo kusababisha wasitishe kazi hiyo hadi jana.

Wana CCM hao ambao baadhi yao walikiri wazi kupewa rushwa ya fedha na kanga, walidai kwamba licha ya kupokea vitu hivyo wasingemchagua kiongozi huyo waliyemtaja kwa jina na badala yake watachukua hatua iwapo atachaguliwa kwa kuwa hafai kuwaongoza.
Hata hivyo Majira ilipomtafuta mgombea aliyetajwa kugawa rushwa na wapambe wake kutiwa mbaroni na TAKUKURU hakupokea simu yake ya kiganjani hadi tunakwenda mtamboni.

Jimbo la Kinondoni
Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azzan ameshinda katika kura za maoni katika Jimbo la Kinondoni kwa kupata kura 6,192 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Bw. Mustafa Muro aliyepata kura 3,055 na kufuatiwa na Bi. Shy-Rose Bhanji aliyepata kura 2,830.

Jimbo la Kawe
Bi. Angela Kiziga ameshinda katika kura hizo baada ya kupata kura 3,140 kwa kumshinda Kipi Warioba ambaye alipata kura 2,752.

Jimbo la Ilala
Kwa upande wa Jimbo la Ilala kazi hiyo pia ilikuwa kitendwawili kigumu baada ya Katibu Msaidizi wa CCM wa Wilaya hiyo Bw. Harun Mkalimoto kuiambia Majira kwamba jana walikuwa wakiendelea kupiga kura katika matawi yote ya Kata ya Jangwani huku tawi moja la Kariakoo ukitarajiwa kumaliza mchakato huo leo.

Majimarefu awa majimarefu Korogwe

Mganga wa tiba za jadi, Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Majimarefu ameibuka kidedea baada ya kuwashinda wenzake 16 kwenye kinyang'anyiro cha Jimbo la Korogwe Vijijini kwa kura 12,441.

Bw. Ngonyani ambaye kwenye kampeni zake hakuwaficha watu kuwa yeye yake ni darasa la saba, alimbwaga msomi na mchumi mwenye Shahada ya Uzamivu, Dkt. Edmund Mndolwa aliyepata kura 2, 286, huku akiwaacha midomo wazi baadhi ya watu.

Mbunge wa jimbo hilo mwaka 2000 hadi 2005 Bw. Mussa Lupatu alishika nafasi ya tatu kwa kura 1,579 na Mbunge aliyemaliza muda wake, Injinia Laus Mhina alishika
nafasi ya nne kwa kura 1,362.

Baadhi ya watu waliohojiana na mwandishi wa habari hizi walisema wao sio wajinga kumchagua mtu wa darasa la saba, bali wanaelewa umuhimu wa Bw. Ngonyani hasa kwenye shughuli za kijamii.

"Tumechoka na wasomi, tangu uhuru ndiyo wamekuwa wawakilishi wetu, ngoja tumpeleke mtu tunayefanana naye, lakini watu wasubiri muda sio mrefu mafanikio ya Korogwe Vijijini," alisema mtu aliyejitambulisha kwa jina moja la Bw. Omar, mkazi wa Kijiji cha Bwiko.

Katika uchaguzi huo, Rais Jakaya Kikwete amepoteza Manaibu Waziri wake watatu katika mkoa wa Tanga baada ya aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Bi. Mwantumu Mahiza kudondoka.

Bi. Mahiza ambaye aliwania ubunge Jimbo la Mkinga alipata kura 9,182 na kupigwa mweleka na Bw. Dustan Kitandula aliyepata 10,867. Mshindi wa tatu ni Bw. Athuman Ngenya aliyepata kura 1,666.

Kama haitoshi aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Aisha Kigoda amepigwa mweleka wa aina yake baada ya Mbunge aliyemaliza muda wake Jimbo la Kilindi, Bi. Beatrice Shelukindo kupata kura zaidi ya asilimia 90 mbele ya wagombea wanane.

Mbunge wa Handeni aliyemaliza muda wake Dkt. Abdallah Kigoda amewagaragaza wenzake tisa baada ya kupata kura 11,227, akifuatiwa na Dkt. Mohamed Mhita aliyepata kura
4,318, huku nafasi ya tatu ikishikwa na Bw. Simon Lupatu.
Mbunge wa Mlalo aliyemaliza muda wake Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi ameshinda kwenye kinyang'anyiro kwa kupata kura 2,813 na kuwabwaga wenzanke 11 akiwemo
Bw. Moez Kanji aliyepata kura 2,106.

Mbunge kwa miaka 15 wa jimbo hilo, Bw. Charles Kagonji alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura 1,676, huku Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga Bw. Rodgers Shemwelekwa
akishika nafasi ya nne kwa kura 1,076.

Pwani watakiwa kuvunja makundi
Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Bagamoyo Fikirini Masokola amewataka wagombea wote ambao wameshindwa katika kura za maoni za kuwapata wagombea kwa ngazi ya ubunge katika jimbo la Chalinze mjini hapa kuvunja makundi ili kukinusuru chama katika uchaguzi ujao wa wabunge na madiwani.

Kauli hiyo aliitoa wakati alipokuwa akitangaza rasmi matokeo ya kura za maoni kwa wabunge wa jimbo la Chalinze na la Bagamoyo jana kwenye makao makuu ya chama mjini Bagamoyo.

“Kabla ya kura za maoni kulikuwa na makundi kwa wagombea na wapambe wao ambapo mara baada ya kupigwa kwa kura za maoni sasa ninawataka wagombea na wapambe wao
kuvunja makundi hayo na kuwa kitu kimoja, hasa kwa wale ambao hawakubahatika kuongoza kwenye kura hizo,” alisema katibu huyo.
Alisema kuwa wapinzani huwa wanatumia makundi kama yalivyokuwa na kuwachukuwa wanachama wetu.

Katibu huyo aliongeza kuwa kutokana na tathimini ambayo ameifanya walaya ya Bagamoyo wanachama wa CUF na wa CHADEMA hawafiki hata 700, ila wakati wa kupiga kura wanapata nyingi, kitu ambacho ni cha kukitazama
sana.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, Dkt. Shukuru Kawambwa
amemshinda Bw. Andrew Kasambara kwa kupata kura 6,170 sawa na asilimia 86.4 dhidi ya kura 969 sawa na asilimia 13.6 za Bw. Kasambara.
Jimbo la Chalinze ambalo lilikuwa na wagombea 10, aliyeongoza na Said Bwanamdogo aliyejizolea kura 8,083 sawa na asilimia 44.5 akifuatiwa na Bw. Iman Madega (4,240), Ramadhan Maneno (3,727) na wengine chini ya kura 400.
Imeandaliwa na Yusuf Mussa, Korogwe; Edgar Nazar, Bagamoyo; John Daniel na Gladnes Mboma, Dar es Salaam
 
uthibitisho....uthibitisho....uthibitisho!!! Nchi hii itakuja kuangamia katika kutaka uthibitisho -- kitu ambacho ccm wanaking'ang'ania sana pindi ukigunduliwa ufisadi wao. Mramba atakuwa mbunge tena kwa sababu hadi sasa hakuna uthibitisho wa ufisadi wake!!!! Chenge atakuwa mbunge tena kwa sababu hakuna uthibitisho wa ki-bongo, uko ule wa majuu tu ambao serikali ya ccm haiutaki.

Lakini uthibitisho mmoja ni kwamba bashe ni mtu wa rostam 100 percent -- alimpatia kazi pale habari corporation, na mshahara wake unajulikana, alimnunulia pikipiki za kampeni ambazo aliibiwa kutoka ofisi za habari corp.

Lakini kwa upande mwingine matokeo ya kyela na urambo east ni pigo kubwa sana kwa rostam kwa sababu ameshindwa vibaya sana kuwang'oa wawili hawa waliomng'oa swahiba wake mkuu el. Ilikuwa faraja kubwa kwangu, na bila shaka kwa wengine. Bado mtataka ushahidi kwamba mwakyembe na sitta hawakuwa maadui wa rostam walipangwa kuangamizwa?

acha pumba wee
 
jamani Mpologomyi vipi, Nsansugwako vipi, eng.Chiza wapo hali gani?
 
Huko kibondo CCM yateua mtuhumiwa mkubwa wa ujambazi wa kuteka magari.......TAKUKURU wahongwa magari....KATIBU CCM WILAYA naye ahongwa gari? Mbunge agalagazwa...NTAGAZWA ALALAMA.....na mengine mengi.....!
 
Kangi ni "Bomba" kambwaga mbunge anayemalizia muda wake Bw. Kajege katika jimbo la Mwibara, Bunda
 
CCM yameguka
• Shibuda atajwa kutaka kujiunga CHADEMA

na Mwandishi wetu


amka2.gif

KATIKA hali inayoashiria uwezekano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumeguka, baadhi ya wagombea wanaodaiwa kushindwa kwenye kura za maoni kwa hila, wamedaiwa kutaka kujiunga na vyama vya upinzani.
Mbali ya baadhi ya wagombea kudaiwa kutaka kujiunga na kambi ya upinzani, baadhi ya wapiga kura wametishia kutokipigia kura kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, mwaka huu endapo baadhi ya wagombea wanaodaiwa kushinda, lakini wamedhulumiwa ushindi wao, hawatarejeshewa ushindi huo.
Mmoja wa wabunge waliomaliza muda wao wanaodaiwa kutaka kujiunga na upinzani baada ya kufanyiwa uhuni kwenye kura za maoni ni John Maghale Shibuda (Maswa).
Habari ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata jana, zilidai kuwa Shibuda amefuatwa na kundi la wanachama wa CCM katika jimbo lake, wakimshawishi ajiunge na CHADEMA na kuwania ubunge katika jimbo hilo.
Shibuda ambaye alijitoa kuwania kiti cha urais hivi karibuni kumpisha Rais Kikwete, anadaiwa kuwa katika wakati mgumu wa kuamua hatima yake kisiasa kutokana na matokeo ya kura za maoni na shinikizo jipya la kumtaka ajiunge CHADEMA. "Kweli watu wengi wamenifuata kunishawishi nijiunge CHADEMA, lakini ni mapema mno kwa sasa maana hata matokeo kamili hatujayapata na hivi sasa ndio tunaenda wilayani kupata matokeo, lakini mimi siku zote naamini kugombana na sheikh au askofu, si kugombana na msikiti au kanisa," alisema Shibuda bila kufafanua.
JIMBO LA KAWE

Wakati hayo yakiendelea jimboni Maswa, jijini Dar es Salaam katika Jimbo la Kawe vurugu imezuka katika ofisi za CCM, Wilaya ya Kinondoni, baada ya wapambe wa mgombea ubunge katika jimbo hilo, Kippi Sinde Warioba, kuandamana kupinga mgombea wao kunyimwa ushindi.
Wapambe hao ambao walikuwa katika ofisi hizo tangu saa tatu asubuhi wakiimba na kutoa maneno ya jazba, walisema wamefika ofisini hapo baada ya kusikia kwenye moja ya vituo vya redio nchini, kikimtangaza mgombea Anjela Kizigha, kwamba ndiye mshindi katika kura za maoni jimboni humo wakati mshindi ni Kippi.
Walisema baada ya kusikia taarifa hizo, waliamua kufika katika ofisi hizo za chama kudai ushindi wa mgombea wao ambaye walidai ndiye aliyetakiwa kutangazwa kuwa mshindi kutokana na kura alizopata.
Wapambe hao ambao walikuwa wakiimba kwamba "Tunamtaka Kippi wetu...tunamtaa Kippi wetu," walisema endapo mgombea wao hatapatiwa ushindi wake kama walivyoona akiongoza katika kata mbalimbali za jimbo hilo, watafanya maamuzi wasiyoyatarajia.
"Tumenyimwa haki yetu...tunataka mgombea wetu kwa sababu tulikuwa na wagombea 16 katika Jimbo la Kawe, sisi tuliamua kumpigia Kippi, ambaye tunaamini ameshinda kutokana na yeye kuongoza katika kata nyingi za jimbo letu," alisema Mwamvita Hussein. Akitangaza matokeo hayo ambayo ndiyo chanzo cha vurugu jana, Katibu wa Wilaya hiyo, Godfrey Tondo, ambaye pia ni mkurugenzi wa uchaguzi huo, alisema mgombea Anjela Kizigha ameshinda kwa kura 3,140, akifuatiwa na Kippi kura 2,752, ambapo nafasi ya tatu ilichukuliwa na Zainudin Adamjee kura 2,466.
Jimbo la Kinondoni
Katika Jimbo la Kinondoni, mbunge ambaye anamalizia muda wake, Iddi Azzan, ameibuka kidedea baada ya kuwabwaga wagombea wenzake 10 kwa kura 6,196 akifuatiwa na Mustafa Mulo kura 3,055 na wa tatu ni Shy-rose Bhanji kura 2,830.
Jimbo la Ubungo
Jimbo la Ubungo ambalo lilikuwa na upinzani mkubwa baada ya kuachwa wazi na Charles Keenja, mgombea Hawa Ng'umbi, anaelezewa kuongoza katika kata nyingi, huku Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga na kijana machachari, Nape Nnauye, wakichuana kwa kura.
Jimbo la Segerea

Katika hali isiyotarajiwa, wagombea 11 wa Jimbo la Segerea wamemwandika barua ya kukata rufaa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yussuf Makamba, ya kutoridhishwa na matokeo ya awali ya kura hizo ambayo yanaonyesha kuwa Dk. Makongoro Mahanga anang'ara.
Akitangaza matokeo ya awali kwa waandishi wa habari, Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Chale Ernest, alisema ingawa bado hawajapata kura za majimbo mawili ya Kipawa na Kiwalani, Dk. Makongoro anaongoza kwa kura 2,148, akifuatiwa na Joseph Kesi kura 1,435 na wa tatu ni John Jambele kura 1,054. Tanzania Daima lilifanikiwa kuzungumza na baadhi ya wagombea hao ambao walikiri kufanya hivyo.
Jimbo la Ilala

Hadi tunakwenda mitamboni, Mbunge wa Ilala anayemaliza muda wake, Mussa Zungu, anang'ara kwa kura 4,962 akifuatiwa kwa mbali na mgombea Sakia Kaikai kura 303, huku wagombea Blandina Mnozya na Jafary ole Koimele, wakifungana kwa kuwa 280 kila mmoja. Hata hivyo kura hizo zitaongezeka baada ya kufanyika uchaguzi wa kata mbili; ya Kariakoo na Jangwani, ambao uliahirishwa kutokana na malalamiko ya wagombea kwamba kulipelekwa mamluki toka chalinze.
Jimbo la Ukonga

Katika Jimbo la Ukonga, Eugen Mwaiposa, ameng'ara kwa kura 2,541, akifuatiwa na Ramesh Patel aliyepata kura 2,244, nafasi ya tatu imechukuliwa na Godwin Balongo kura 1,510, mtoto wa Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Kapteni mstaafu, John Balongo. Kura hizo zitaongezeka baada ya kuhesabiwa kura za kata mbili ya Kipawa na Kiwalani, ambazo mpaka tunakwenda mitamboni zilikuwa hazijakamilika.
Jimbo la Kigamboni
Mbunge anayemaliza muda wake wa Jimbo la Kigamboni, Mwichuoum Msomi, ambaye naye alikuwa miongoni mwa wagombea 19 wa jimbo hilo akiomba ridhaa ya wana CCM, naye ameangukia pua baada ya mgombea Dk. Faustine Ndugulile kung'ara
Jimbo la Temeke
Mbunge Abbasi Mtemvu ameibuka kidedea baada ya kupata kura za kishindo 7,761 akifuatiwa na Salim Chikago kura 3,456 na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mohamed Ngulangwa kura 1,910.
JIMBO LA TABORA MJINI

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Tabora Mjini, Mwanne Mchemba, amegoma kusaini matokeo ya kura za maoni zilizopigwa kwa madai kuwa yamepikwa. Mgombea huyo ambaye alikuwa mwanamke pekee kati ya wanaume sita na mbunge wa zamani viti maalumu, alisema takwimu hizo haziko sahihi na amewasilisha malalamiko yake kimaandishi katika ofisi za chama wilaya kwa hatua zaidi.
JIMBO LA BUSEGA

Hali ya mambo imeanza kuchafuka kwenye Jimbo la Busega wilayani Magu, mkoani Mwanza, baada ya baadhi ya wanachama wa CCM jimboni humo kushindwa kupiga kura zao za maoni kwa siku tatu mfululizo, kutokana na uchaguzi huo kugubikwa na mchezo mchafu, rafu na vurugu.
Sanjari na hayo, kuna taarifa kuwa baadhi ya wagombea ubunge wa jimbo hilo, tayari wameshawasilisha pingamizi kwa uongozi wa CCM wilayani hapa, wakipinga kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni katika jimbo hilo na kuomba uchaguzi urudiwe na kwamba pingamizi hiyo imemlenga mgombea mwenzao aliyeshinda nafasi hiyo, Dk. Titus Kamani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka Jimbo la Busega, wilayani Magu zinadai kuwa wanachama wa CCM kutoka matawi ya Amboni na Lutubiga Kata ya Lutubiga, wameshindwa kupiga kura hadi jana kutokana na zoezi hilo kuvurugwa mara kwa mara na wafuasi wa mmoja wa wagombea hao. JIMBO LA MVOMERO

Katibu wa Fedha wa CCM, Amos Makalla, ameshinda katika kura za maoni ya kuwania kuteuliwa na chama hicho kugombea ubunge wa Jimbo la Mvomero, nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiriwa na Suleiman Saddiq. Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo, Poroleti Mgema, alisema jana kuwa Makalla alipata nafasi hiyo baada ya kupata kura 13,479 katika kata zote 23 huku Saddiq akipata kura 6,476. Wagombea wengine waliojitokeza katika kinyang'anyiro cha kura za maoni na kura zao katika mabano ni Leoni Msimbe (1,078), Ackley Limoso (367), Albanie Mgweno (315), Hussen Sungura (137) na Mussa Mruma (139).
 

Majimarefu awa majimarefu Korogwe

Mganga wa tiba za jadi, Bw. Stephen Ngonyani maarufu kama Majimarefu ameibuka kidedea baada ya kuwashinda wenzake 16 kwenye kinyang'anyiro cha Jimbo la Korogwe Vijijini kwa kura 12,441.

.....Bw. Ngonyani ambaye kwenye kampeni zake hakuwaficha watu kuwa yeye yake ni darasa la saba, alimbwaga msomi na mchumi mwenye Shahada ya Uzamivu, Dkt. Edmund Mndolwa aliyepata kura 2, 286, huku akiwaacha midomo wazi baadhi ya watu.



Nadhani kugombea ubunge , mgombea anatakiwa awe na elimu walao ya kidato cha nne. Sasa huyu prof. amekiri kuwa na elimu ya darsa la saba. Anaweza kuondolewa na wenzake huko ktk vikao vya CC na NEC kwa kigezo hicho. Iwapo atapitishwa na ccm , CHADEMA itapeta, maana atawekewa pingamizi kwa kukosa kigezo cha elimu ya chini (minimum) kinachotambulika kisheria ili kugombea ubunge.
 
Mzindakaya achekelea vigogo kubwagwa


PostDateIcon.png
Thursday, 05 August 2010 06:27

Na Godfrida Jola
SIKU mbili baada vigogo kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubwagwa katika kura za maoni, aliyekuwa Mbunge Kwela Dkt. Chrisant Mzindakaya amesema kwamba ni halali kwao kutemwa kutokana na kuwepo madarakani kwa muda mrefu kwa kuwa kila kitu kina kikomo chake.

Alisema kutokana na kutambua umuhimu wa kuachia madaraka kabla ya kuachishwa, aliwashauri baadhi ya yao kung'atuka kwa malengo ya kupisha damu mpya na mbichi kuendeleza ujenzi wa Tiafa, lakini hakusikilizwa.

Alisema kutokana na 'uroho wa madaraka na kushindwa kusoma alama za nyakati' watu hao walimdharau na kumwona hafai, hivyo kuamua kurudi tena katika mchakato.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana, Dkt. Mzindakaya alisema kushindwa kwa viongozi hao kunadhihirisha ni jinsi gani wanachama wa CCM walivyochoshwa na viongozi waliokaa kwa muda mrefu madarakani.

Alisema kuwa ushauri wake aliutoa kwa wakongwe hao si kutokana na uzee wao, bali kutokana na kutumikia Taifa kwa muda mrefu, na kuwataka kusoma alama za nyakati hasa katika kipindi hiki kinachohitaji mabadiliko makubwa.

"Sikushangaa na wala matokeo hayo hayashangazi, kwani baadhi yao niliwashauri waondoke na hawakutaka kunisikia, ishu sio uzee ila muda uliowatumikia wananchi wako," alisema Dkt. Mzindakaya

Alisema, ukiwa kiongozi wa ngazi ya juu, pia ukiwa na nia ya kugombea, unatakiwa kuwa makini na kupima ni kwa kiasi gani wananchi wako wanakukubali kutokana na utendaji kazi wako kwa kipindi chote ulichanza kuwatumikia.

Dkt. Mzindakaya alifafanua kuwa, viongozi waliotumikia majimbo yao kwa muda mrefu wanapaswa kuwa watulivu na wastahamilivu, hawapaswi kuamini kuwa ni chuki ama njama za kisiasa.
Aliwataka kuwa na imani na kukubaliana na hali halisi ya wapiga kura wao ambao ndio kielelezo cha utendaji na uhusiano wao katika kazi.

"Tunatakiwa kuwa na utamaduni wa kuacha madaraka kwa kupenda wenyewe au baada ya kulitumikia taifa muda mrefu, kwa kuwa kila kitu kina ukomo, ukisuburi kutolewa na unaanza visingizio wakati si kweli," alisema.

Dkt. Mzindakaya ambaye amekuwa akipingana sana na vitendo vya matumizi ya fedha katika kupata madaraka alisema, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ina jukumu kubwa la kuwatia nguvuni wanachama wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

Alisema kwa muda mrefu CCM imekuwa ikilaumiwa kuwa na matumizi makubwa ya rushwa katika kuwapata wagombea na kwamba vitendo hivyo vinahitajika kukomeshwa ili kulipa taifa ahueni.
Alisema kuwa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ilianzishwa kwa malengo maalumu ikiwemo kudhibiti viongozi walau walio na tabia ya kununua uongozi.
"Tulipitisha sheria ili itumike, hiyo ni moja ya mikakati ya CCM kupambana na rushwa, pia tumekuwa tukipiga kelele waache kutoa rushwa lakini wahakutaka kuacha, sasa ngoja sheria ichukue mkondo," alisema Dkt. Mzindakaya.

Wakati wa kuliaga bunge la tisa mwezi uliopita, Dkt. Mzindakaya alisema taifa linaelekea pabaya kutokana na viongozi wengi kupatikana kwa misingi ya utajiri na rafu za kisiasa.

Aliionya CCM kutokana na hulka ya matumizi ya fedha au rushwa katika kuwapata viongozi na kwamba, Taifa litaangamia kutokana kuongezeka kwa kundi la walionacho na wasionacho.
Mwanasiasa huyo wa muda mrefu akiwa ameanza kazi akiwa na umri wa miaka 25 na kuacha akiwa na miaka 70, alieleza kutoridhishwa kwake na namna siasa inavyoendeshwa kwa sasa ambapo matumizi ya fedha yamekuwa makubwa zaidi kuliko ilivyokuwa awali wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema, vyama vyote kwa sasa vinanuka kwa rushwa katika michakato yao ya kuwapata viongozi kitu ambacho kimejidhihirisha katika kura za maoni za CCM.
 
Na January Makamba ameshinda for 85&....Lau Masha ameshinda pia...hahaha C.C.M!....

Najua utakuwa umefurahi sana dada kely01, kwani ulidai January rafiki yako.

Ukweli ni kuwa kama alianza kampeini tangu mwaka jana kupitia kwa baba yake kwenye mashina ya CCM, basi alikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda hasa baada ya malalamaiko ya Mzee Shelukidno kutaka kampeini jimboni mwake zisianze mapema kuwa zimeishia pagumu; kesi ya tumbili kuamuliwa na nyani. Ndivyo Tanzania ilivyo.
 
Kwanza hongera zako kushinda udiwani, pili hongera kwa Bashe kumshinda mpiganaji Seleli hata kama ni kwa kutumia masalia/mabaki ya Kagoda.

Wapenzi wa Selelii wasiwe na shaka, hata kama Bashe angeshinda kwa asilimia 99% na Selelii asilimia 01%, bado CCM itampitisha Selelii na kumtosa Bashe, kuna secret agreement kwa wabunge makamanda waliahidiwa kupitishwa no matter what, nao ndio wakakubali kuitosa CCJ.

Hivyo kama wana CCM wa Nzega, wanawakilisha wakazi wote wa Nzega, na chaguo lao ni Bashe, basi atakayekwenda upinzani na awe Bashe, asimame na Selelii kwenye sanduku la kura, hivyo Jimbo la Nzega tuanze kulihesabu upinzani.

Kama na kuchekelea ushindi, kambi ya Bashe, chekeni sana, mkisubiria panga la NEC na mtalia sana, piga ua CCM haiwatemi makamanda wake, almanusura waimege ikatike vipande viwili, wakakubali kuinusuru CCM, sasa ni zamu ya CCM kuwanusuru.

Bashe ajiandae kwa safari, the only choice ni Chadema, tatizo langu kwake ni jee Chadema itawakubali hawa makuwadi wa RA?. Jee itafungua milango yake kuwakaribisha nyoka?.

Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.

Nimefanya kama nilivyoahidi.
Bravo Pasco!
 
quote_icon.png
Originally Posted by Pasco

Mwito wangu kwa Chadema, acha milango wazi kwa yoyote ajaye bila kujali alikuwa akimtumikia nani, concetration yao kwa sasa, iwe ni idadi ya viti vingi bungeni.

Chama kifungue milango kwa kina Bashe kwa tamaa tu ya kuwa na viti vingi bungeni? Hell no!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom