Nimemwangaliwa waziri wa Elimu wa Kenya akitangaza matokeo ya KCSE muda mchache uliopita kupitia Citizen Tv. Kwanza alitanza amejiamini, ana furaha, anapigiwa makofi. Amesema kuwa kiwango cha Elimu kimepanda, na kiwango cha Ufaulu pia kimepanda. Mtindo wao wa utangazaji matokeo sio kama wa Tanzania, alitaja kimikoa, na baadaye akataja wanafunzi kumi bora kitaifa, shule kumi bora kitaifa, akaweka msisitizo wa haya yafuatayo ambayo binafsi nimeona ni Tatizo kwa upande wa Tanzania.
NIMEMALIZA KUSIKILIZA HIVYO, NIKALINGANISHA NA MATOKEO YETU YA MAJUZI YALIYOTANGAZWA, Nimejiuliza sana sisi tumekosea wapi Watanzania?. 'Tukosoane, turekebishane, tuwajibishane ndipo tusameheane'. Wanaong'ang'ania kukaa ofisini na wanaambiwa kuwa wametufelisha watoto kwa kutowajibishana, au kwa kufuata sheria kwa uleglege wachukuliwe hatua gani?
- Watahiniwa walikuwa 437,762= Waziri akasema Transition to higher Education is 100%
- Akakiri kuwa Ratiba ilibadilika kidogo kwa wiki 3 kwa sababu ya mgomo wa Waalimu
- Akasisitiza; Cheating is no longer option in Kenyan Examination process, yaani hakuna udanganyifu
- Waziri akasema watu 88 WAMEFUNGWA kwa sababu ya kudanganya katika mitihani, au irregulaties mbalimbali
- Wavulana wamefaulu kwa 55%, na Wasichana 45%...................
- Akasema wataangalia upya madai ya waalimu kama walivyokuwa wamekubaliana