Matokeo ya form four 2008

wandugu,

..tuwe makini ktk kuzitafsiri takwimu tunazolishwa toka baraza la mitihani.

..mkoa wa kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 50. zinazosifiwa kufanya vizuri ktk mtihani wa taifa 2008 ni kama shule 6. kati ya hizo shule 6, zipo shule zenye wanafunzi chini ya 35!!

..ni vizuri ikaeleweke kwamba, shule hizo chache zilizoko Kilimanjaro, zinazosifika kwa kufaulisha, zina-admitt wanafunzi toka maeneo mbalimbali nje ya mkoa huo.

..vigogo wameacha kupeleka watoto wao kusoma sekondari Kenya na Uganda. badala yake wanasomesha watoto wao ktk shule nzuri-nzuri kama Kifungilo, St.Mary's,Marian Girls,Feza, Don Bosco, etc.

..hali ya elimu ni mbaya sana huko vijijini. imefika mahali wananchi wameanza kuhoji ulazima/uhalali wa kupeleka watoto shule.
 
JokaKuu:

Rafiki yangu mmoja alisoma kwenye shule moja ambayo kuwa na wastani wa D, kulimfanya mtu afukuzwe shule. Na walipofika form 4 darasa lilikuwa na wanafunzi chini ya 35 na wote walipata division 1 na 2.

Sasa ukiangalia sacrifies zinazotumika ili kupata division 1 na 2, hazina mpango wowote kwenye maendeleo ya elimu.
 
Stiff Competition friends,

Tukiwa UMBWE Moshi mid 80's ktk O level we competed for Single Digit yaani 7-9 points na sii kupata division 1. Yaani tofauti ya marks 2 kati ya 97% na 95% ilifanya wanafunzi wazipige..na kumzonga mwalimu! Amini tulikuwa 70 form IV na 50 tulipata Division 1!

Raha tulikuwa na waalimu wazuri mno..na maabara na vitabu na hali safi ya hewa!

Sasa this was a public school....natamani % kubwa ya public schools Tz zingekuwa bora kwani zinachukua Watz toka kila kona ya nchi!
 
....matokeo hayana tofauti na kazi waliyofanya hao waliotengeneza website, website gani huwezi hata navigate,huwezi hata kutafuta jina la shule mpaka ufinye macho juu chini juu chini...yaani unaweza kutumia saa nzima kutafuta unachotafuta,huu ulipuaji wa kazi sijui utaisha lini,ni aibu kubwa kwa watu wanaosimamia elimu kama NECTA kuwa website mbovu kama hii,next year tafadhari msionyeshe watu hii aibu!

Mmmh, angalia isije ikawa kwamba matokeo hayana tofauti na wanaoshindwa kutafuta jina la shule kwenye website kwa muda mfupi !. Mkuu unaweza kulipata jina la shule kwa muda mfupi sana, haiwezi kuzidi sekunde 10 (less than 10 seconds). Tatizo hapa ni watumiaji wa computer, na si web developers.
 
kwa bibi wasijazane ikullu,TRA,PPF ATCL BIMA MPAKA BOT,,QAACHENI TU JAMANI HIVI VICHWA,
 
Mimi siyo mchaga lakini nakubali kuwa wachaga wana akili. Hata wakisoma nje ya mkoa wao huwa kwenye mashule mengi wanaongoza. Hata shule niliyosoma wakati ule ilikuwa inachukua wanafunzi toka mikoa ya Mara, Dodoma, Singida, Arusha na Kilimanjaro. Unajua tena mambo ya Siasa za ujamaa na Nyerere kutaka kuchanganya makabila. Katika shule hiyo, waliokuwa wanaongoza ni wachaga kwa kupata divisions 1 kali. Nafikiri wengi wa wachaga walikuwa wanaishia Div 2. ni wachache au hakuna kabisa mchaga alikuwa anapata Dv 3 na 4. Na hali hiyo iliendelea kuwa hivyo hadi mwaka 1987 serikali ilipoamua kuwa watoto wawe wanasoma shule za jirani na warrant wa train ukaondolewa (mageuzi yalipoanza). Kuanzia pale shule ile ililazimika kuchukua wanafunzi wa mikoa ya jirani yake na kuanzi pale kufeli ni karibu shule nzima. Nakumbuka form 4 ya mwaka 1990 nilipata habari kuwa mkuu yule wa Shule matokeo ya kwanza kwa waafunzi hao yalitoka na ilianzia Div 3. Mkuu wa shule alizimia akakimbizwa hospital na mwishowe alihamishwa shule.

Sasa basi wachaga wanajitahidi mambo mengi, na ni wajanza.
 
Mkuu kwa analysis ya namna hii nadhani unapotoka kidogo.

Swala siyo kwamba wachaga wana akili than the rest, kikubwa hapa ni right attitude ya mzazi tangu mwanzo. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Mimi nimesoma na wachaga wengi tuu..lakini usahihi wa kauli yako siwezi kuuthibitisha..maana waliokuwa wanaongoza darasa...walikuwa tofauti..kutoka sehemu mbali mbali za Tanzania. Kwa hiyo assertaion yako siyo sahihi. Kwa mtizamo wangu.

Kikubwa ambacho unaweza kusema nikakubali hapa, ni kwamba wazazi wa kichaga tofauti na makabila yaliyo mengi hapa kwetu Tanzania..wanaweka msisitizo wa elimu sana kwa watoto wao tangu mwanzo. And they go extra mile to support them, irrespective of their economic means. Mfano, si rahisi uende kilimanjaro ukute mtoto anauza mbege eti kakosa karo ya kumsomesha..ni very rare sana (ofcourse wapo..lakini siyo chronic kama kwingineko). atachapwa viboko mpaka kieleweke..aende shule...Kifupi wazazi na ndugu wanajua umuhimu wa elimu hata kama hawakusoma. LAKINI ukija kwetu usukumani (mfano)..ni rahisi kukuta mtoto wa Masanja akichunga ng`ombe kisa kakosa karo wakati mjomba wake ni ANDREW CHENGE!. na wako wengi tuu. Sasa mzee..kwa mwendo huo lazima mtoto aliyepewa support afaulu...

Ni kama useme kwamba WAKATOLIKI wengi wana akili kwa sababu shule zao za seminary na nyinginezo wanafaulu sana! Hapa si swala la wakatoliki, swala ni kwamba hizi shule zinaweka mkazo thabiti katika elimu ya vijana. Kama ulisoma seminary au mission school utanielewa. Kwa hiyo hapa..umpeleke muislamu, msabato, mpagani..atafaulu tuu..maana mazingira yanaruhusu hivyo. N ashule imejijengea hiyo misingi tangu zamani. Na kama huwezi basi utaenguliwa..na utaenguliwa na hizo marks, siyo wao!

Mwisho kabisa, sipendi kuamini kwamba kuna makabila ambayo hawana akili No way. Ni kuwa na right and timely support in education tangia mwanzo. Na sana sana watu tujifunze kwa ndugu zetu wachaga: Kuthamini elimu. huwezi panda maharage ukavuna mahindi. Kama mtoto unampa malezi ya kupenda shule..lazima at the end of the day atafaulu tuu. Ni kama hapa watu wanalalamika kwamba wengi wamefeli hesabu: Si kwamba watu hawana akili hiyo..no way...ni kwamba..mwanafunzi alipokuwa form one akapata F ya hisabati..baba alimwambia.."naelewa hesabu ni ngumu..wewe jitahidi kwenye kiswahili na kiingereza..after all, siku hizi hesabu haina msaada mkubwa katika kupata kazi" Do you really expect huyu mtoto hata kama ungempeleka St. nani sijui atakuja afaulu hisabati?

Kwa hiyo swala la kufaulu ni maandalizi ya siku nyingi saana. Mtoto ambaye hakupenda shule siku zote..hata kama ungempeleka Ilboru au Maua Seminary..atafeli tuu..kwa sababu ile culture ya kupenda shule na kujibidiisha haikuwepo tangia mwanzo. Na hicho ndicho wachagga walikigundua mapema saaana kuliko akina Masanja na wengineo.
 
Mkuu Masanja good analysis.

Nadhani hali imeanza kubadilika vipi zile shule za serekali zilizokuwa na matokeo mazuri miaka ya karibuni zimeonyesha kiwango cha chini sana.Ilboru,Mzumbe na nk siku hizi hazifurukuti tatizo ni nini ?.Nasikitika sana kwa hizi shule kuwa na matokeo mabaya kwasababu zilikuwa ni kimbilio la watoto wa wanyonge.
 
Watanzania toka usingizini...meli inazama??? ndiyo kabisa wanapata usingizi mnono!

Matokeo yanasikitisha, je nini Kifanyike? Mara nyingi watanzania wamekuwa ni wengi wa lawama kuliko kutoa suluhisho. Si kwa maoni tu, bali hata kwa vitendo. Tanzania itaimarishwa na sisi wenyewe....watanzania wenyewe...ila kinachoonekana sasa ni lawama kuliko suluhu.

Kila aliyeko nje ya mfumo...hapa namanisha katika kutoa maamuzi ya utekelezaji wa sera kama mawaziri n.k anaonekana kulalamika. Wazazi pia badala ya kusaidia kujinasua na matatizo ya namna hii nao pia wanalalama. Mifumo ya kufundishwa ili wajibu mitihani na si kuelewa hasa huko sekondari inapelekea matatizo katika vyuo vikuu...wanafunzi hata vyuoni hawaonekani kusoma vitabu wenyewe wanataka "spoon feeding" hali hii inasikitisha.

Hata hao waliofuhulu wakifika vyuoni mambo ni yale yale...unashindwa kujua hata wamepitaje huko masekondari..wanakuja na hayo matokeo mazuri ya kujivunia, wengi wanatoka shule zinasifika kwa kufundisha kwa kiingereza nyingine zimejaa walimu toka jirani...lakini inawawia vigumu kufuatilia masomo ambayo hata hivyo yako kwa lugha ya Kiingereza..sasa nani wa kulaumiwa. elimu ni biashara kwa sasa.

Inapendeza mtoto wako akisoma shule inayofahulisha sana na akafahulu kwenye hizo grade nzuri tunazoziona, na kwa kuzingatia hivyo hakuna mwenye shule atakayependa kuona matokeo yanakuwa mabaya...kwa vile anataka kuvutia wazazi walete watoto wao katika shule hiyo na pia anaweza kupandisha ada anayotaka...waliosoma uchumi mnajua "supply and demand" Naomba nieleweke vema, hapa sisemi shule hizi zote zina matatizo au upungufu wa namna hiyo...huduma inayotolewa katika mashule haya pia inaridhisha kwa wazazi. Lakini ni asilimia ngapi ya shule za namna hii, na ni watanzania wangapi wanaweza kugharimia watoto wao katika shule hizi kuanzia mchakato wa kufanya usahili wa kuingia katika mashule haya...gharama ni kubwa, na je shule hizi ziko wapi? mjini au vijini?

Mweleke wa Elimu Tanzania ni hupi??? wazazi wanachangia haya, silaumu sana wazazi kwa vile baadhi yao hawana uelewa wa kutosha na wengi wao wanasukumwa na utajiri walionao, na pia sasa Tanzania inabadilika tunarudi katika mfumo wa Kibepari bila kujitambua, je mnasubiri Katiba ya nchi ibadilishwe ndiyo mjue kuwa sasa Tanzania ni nchi ya kibepari. Wenye nacho wataendelea kuwa nacho na pia wataendelea kutawala hii nchi hata kama uwezo wao wa kufikiri na kuchanganua mambo ya kusaidia maendeleo ya Taifa ni mdogo. Hili hatutalikwepa, majina ya viongozi, wakurugenzi, makatibu wakuu nk yatabaki kujirudia rudia rudia. Si elimu tu, watato wangapi wa "vigogo" wanasoma katika mfumo wetu, vigogo wangapi wanatibiwa katika hospitali za serikali? mengi yamesemwa!

Huu ndiyo mfumo, wanasayansi wamepungua, vijana na hata wazazi hawataki kusikia watoto wao wanasoma haya masomo ya sayansi..sababu zinajulikana...hakuna maslahi na serikali haijatilia mkazo..utashangaa serikali yaweza kuazima wasomi kutoka nje ya nchi..wanahitwa watalaam...madaktari, walimu hata vyuo vikuu..kisa hatuna wataalamu wa kutosha..wanalipwa pesa za kutosha...je ni wapi tumejikwaa? na je tuna mipango ya muda mrefu ya kuokoa taifa kutokana na utegemezi wa namna hii au mambo yataendelea kuwa kama yalivyo hadi lini? na hii ndiyo tunasema ni ufisani kila mtu anajitazama mwenyewe..

Wizi wa mitihani ni tatizo kubwa, linahitaji suluhu lakini hili linawezekana? sijui ni watu wangapi waliohusika wamefikishwa katika vyombo vya sheria na kuhukumiwa..nasikia mara vijana/wanafunzi wamekamatwa na paper...wanazitoa wapi? paper kuvuja kumeanza lini? na je wahusika ni akina nani? wazazi wanahusika pia...sasa mfumo huu utabadilishwa na nai????

Mimi ni mwalimu pia, utashangaa unawauliza wanafunzi maswali ambayo unafikiri kwa upewo wao wanaweza kuyajibu...wanakwambia wao wamefundishwa maswali na mjibu na si kufikiri na kutoa majibu kutokana na wanavyofikiri wa pia...mtihani ukifika wanakuuliza tusome wapi? ukiwambia wakasoma kwenye maktaba na kuwaeleza ni vitabu gani wakasome...hawana muda. wengine wanajichora pia kwenye viganja vya mikono, kuweka makaratasi vyooni n.k...ubaya zaidi mfumo wa elimu wa Tanzania kuanzia shule ya msingi ni kuangalia mwanafunzi amepata maksi ngapi..aliyepata nyingi ndiye mwanafunzi bora, hili ni tatizo, huku kwa wengine, mtihani wa mwisho unakuwa na maksi kidogo...mahudhurio, michango ya mijadala madarasani inapewa umuhimu pia....

Vyuo vikuu vilianzisha majaribio kabla ya kuingia kwenye vyuo hivyo...je hii ni biashara au kweli inachuja wanafunzi? mimi bado naona sasa imekuwa kama mazoea na "deal" kwa vyuo husika...na hawa kesho wanalalamika ni wanafnzi gani hawa wametoka wapi? wanatilia mashaka necta? mimi sijui...lakini utakuta mwanafunzi hawezi kujieleza darasani lakini mwanafunzi huyu amefahulu NECTA, amefahulu ENTR EXAMINATION za vyuo, ukiwa naye darasani hapo vyuo vikuu utashanga..tunaelekea wapi? ni nani wa kufungwa jiwe shingoni na kutupwa baharini??? Hii haiishii hapo vyuoni, waajiri nao wanafanya usahili ili kupata wafanya waajiriwa bora...utasikia wanaulizana kweli huyu katoka chuo kikuu? na tena kile tunachojua kuwa ni bora? waandishi wa habari anoa pia wako katika mkumbo huu....walimu pia. Viongozi hao usiseme! VIHIYO wataisha Tanzania au angalau kupungua????

Kazi kwetu.

Jasson
Korea Kusini
 
Mmmh, angalia isije ikawa kwamba matokeo hayana tofauti na wanaoshindwa kutafuta jina la shule kwenye website kwa muda mfupi !. Mkuu unaweza kulipata jina la shule kwa muda mfupi sana, haiwezi kuzidi sekunde 10 (less than 10 seconds). Tatizo hapa ni watumiaji wa computer, na si web developers.

...acha utani wewe,kuna namna yeyote ya search itakayonipa jina la shule bila scroll up/down repeatedly...pls saidia maana kuna shule mpaka leo sijaziona!
 
Mmmmmh! Na wasiwasi kama unajua fujo na "heated claims" ua zinakuwaje!?

Haya basi, walimu wa Tanzania si wababaishaji, wanafunzi si wababaishaji, wazazi si wababaishaji na li-serikali si la kibabaishaji.......hapo vipi mheshimiwa sana?

Tanzania mambo ni tambarare na elimu yake ni ya daraja la kwanza.......LOL!

You win.
 
Matokeo yanakuwa mabaya kutokana na msingi kuwa mbovu!mtoto anasoma shule za serikali ambazo siku hizi kama mzazi usipomfuatilia ujue anapotea, walimu wa shule za public wanalipua tu hii pia inaweza ikatokana na mishahara wapewayo hairidhishi!Ukiangalia watoto wengi waliofaulu ni wale toka msingi yupo private then akapelekwa sekondari private pia tena zile za ST's ambazo kuingia tu hadi interview!
 
Baraza letu la mitihani linatoa takwimu za ajabu sana, yani utafikiri linaongozwa na watu waliofeli somo la statistics. Huwezi kulinganisha ubora wa elimu katika mikoa kwa kuhesabu ni shule ngapi mkoa umeweza kuingiza kwenye top 10 au top 20 ikiwa mikoa ina idadi tofauti ya shule. Mathalani, tuseme mkoa wa kilimanjaro una shule 150, wakati mkoa wa Mtwara una shule 50, ikitokea mkoa wa kilimanjaro ukawa na shule 9 kwenye top 20 na Mtwara ukawa na shule 3; mikoa hii miwili itakuwa na ubora unaolingana, lakini baraza letu litatafsiri kuwa kilimanjaro umeongoza...nadhani wao pia wanahitaji somo la hesabu.
Kwa maneno mengine kitu kinachofanywa na baraza la mitihani hapa, ni sawa sawa na kulinganisha shabaha za watu watatu A, B, na C; A akiwa mawe 10, B mawe 3 na C mawe 3. Sasa kila mtu inatakiwa atungue embe kutoka mtini mpaka mawe yake yaishe na atakayetungua embe nyingi ndiyo mshindi. Sasa hapa ikitokea watu C na B wakatungua embe 1 kila mmoja huku mtu A akitungua embe 3 huwezi kusema mtu A ana shabaha kuliko watu B na C kwa sabau idadi ya mawe waliyotumia hailingani!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom