Matokeo ya Arumeru: Salaam kwa Edward Ngoyai Lowassa!

ngoja nianze kujenga nyumba kutokana na hela tuliyogawiwa na ccm arumeru, halafu kura tukapeleka chadema
Nadhani sasa wamejifunza, watakuwa waangalifu sana kugawa hela zao. Nadhani watazitoa kwa viapo kabisa.
 
Kimsingi lowassa ameanguka moja kwa moja!!maana ni kweli ana nguvu ndani ya chama ndiyo maana mkwe alipitishwa!lakini kuanguka kwa sioi imethihirisha kuwa ikiwa atatumia nguvu ya pesa na akapitishwa na chama kugombea 2015 kwa wananchi ccm itavuna vijiasilimia vichache vya kura. (samaki nje ya maji atambi like wise lowassa nche ya chama hatambi

Kaka una akili sana wewe, jamaa nje ya CCM ni papa nje ya maji, hana ujanja!
 
Anguko la Siyoi ni anguko la Lowasa na ni anguko la Jk aliyempitisha kwenye vikao kwa lazima huku akijua ananuka rushwa na mwisho ni ANGUKO WA CCM.

Binafsi naamini JK alilazimisha Sioi apitishwe na kikao ili aje ashindwe na wapiga kura ili ile hoja yake kuwa EL hawezi kuwa mgombea kwa CCM kwenye uraisi ipate confirmation. kama ameshindwa kuchukua jimbo tena lililo kwenye ngome yake (kaskazini) ataweza kushinda uchaguzi wa nchi nzima? Naunga mkono hoja kuwa huu ndo mwisho wa EL kisiasa Tz. atajitahidi kutapatapa kutafuta vijisababu, kama kawaida ya mfa maji, ila kisiasa kwa kweli EL na kambi yake ndani ya taasisi yao (CCM) imetoka! na ndio maana wengine ndani ya CCM hao hao wanashangilia pamoja na Chadema kwa ushindi wa CDM Arumeru!
 
Mwenyekiti wake JK alimpa kamba ndefu sana ili ajinyonge mwenyewe. Naye kwa kujiamini kuwa ameshinda kumptisha Sioi kugombea ubunge akasema yuko tayari kwa mapambano, sasa inaonyesha kumbe hawezi tena mapambano mtu huyu ni Kwishney sasa hivi, hata Monduli sidhani kama anaweza jiokoa mwenyewe
 
Nimefarijika sana,nimefurahishwa sana nimeona fahari pia kuona ukombozi wa Tanganyika ukiletwa na CHADEMA
 
Binafsi naamini JK alilazimisha Sioi apitishwe na kikao ili aje ashindwe na wapiga kura ili ile hoja yake kuwa EL hawezi kuwa mgombea kwa CCM kwenye uraisi ipate confirmation. kama ameshindwa kuchukua jimbo tena lililo kwenye ngome yake (kaskazini) ataweza kushinda uchaguzi wa nchi nzima? Naunga mkono hoja kuwa huu ndo mwisho wa EL kisiasa Tz. atajitahidi kutapatapa kutafuta vijisababu, kama kawaida ya mfa maji, ila kisiasa kwa kweli EL na kambi yake ndani ya taasisi yao (CCM) imetoka! na ndio maana wengine ndani ya CCM hao hao wanashangilia pamoja na Chadema kwa ushindi wa CDM Arumeru!
Umenena kama ulikuwepo mahala fulani. Nasikia hata Sioi mwenyewe alilazimishwa tu na familia yake haikutaka. Hata jinsi alivyokuwa akiomba kura niliona kama mtu ambaye anasema kama vile maneno hayatoki ndani ya nafsi ukilinganisha na Nassari jinsi alivyokuwa akiomba kura kwa kujituma na kuonyesha kweli kwamba anautaka ubunge.
 
SAFI. Lowassa si lolote si chochote. LOWA anaweza (1) siasa za gizani, na (2) nguvu yake iko CCM vikaoni tu. Low hana lolote nje ya hapo, believe me. i ya chama ndiyo maana mkwe alipitishwa!lakini kuanguka kwa sioi imethihirisha kuwa ikiwa atatumia nguvu ya pesa na akapitishwa na chama kugombea 2015 kwa wananchi ccm itavuna vijiasilimia vichache vya kura. (samaki nje ya maji atambi like wise lowassa nche ya chama hatambi[/QUOTE]
 
Binafsi yangu nawashukuru sana wana Arumeru kwa kufanya maamuzi ya busara. Wananchi wa Arumeru wamezungumza hakuna cha JK alitaka nini au EL sijui kafanya nini maana haikutosha hadi Mkapa alikuwepo pia. Ni uamuzi wa wananchi wa Arumeru pekee unaojenga hoja zote.. CCM wanakumbwa na Tsumani kama ya Japan.. wanakwenda na maji.
 
Yule mtoto mtoa matusi amepotelea wapi, natamani kumsikia kidogo maoni yake. Matusi yao aibu yao wenyewe.
 
Nilimshauri hakusikiliza!. Pia nitamshauri aachane na ndoto za urais 2015, Chadema inachukua nchi!.
Ah Pasco sasa vipi kikundi chenu cha Friends of EL ndio mwisho wa malengo yake ,uchaguzi wa ARM ni rasha rasha tu El Nino au Tsumami vinakuja jiandaeni hapatatosha 2015
 
Binafsi naamini JK alilazimisha Sioi apitishwe na kikao ili aje ashindwe na wapiga kura ili ile hoja yake kuwa EL hawezi kuwa mgombea kwa CCM kwenye uraisi ipate confirmation. kama ameshindwa kuchukua jimbo tena lililo kwenye ngome yake (kaskazini) ataweza kushinda uchaguzi wa nchi nzima? Naunga mkono hoja kuwa huu ndo mwisho wa EL kisiasa Tz. atajitahidi kutapatapa kutafuta vijisababu, kama kawaida ya mfa maji, ila kisiasa kwa kweli EL na kambi yake ndani ya taasisi yao (CCM) imetoka! na ndio maana wengine ndani ya CCM hao hao wanashangilia pamoja na Chadema kwa ushindi wa CDM Arumeru!
Kaka unamuonea JK,yeye si ndie alimlazimisha ''mkwe ''kuwa amrithi baba yake,yeye JK hakuwa mtoaji wa mafungu ambayo takukuru imeshikwa na kigugumizi,sio JK aliyemwambia aliyemwambia Lowasa apande jukwaani ni yeye mwenyewe EL game limemfia au mumesahau kauri za ''mapambano yanaendelea'' alizozitoa pale VIP aliporudi kutoka Ujerumani,nafikiri alisahau kuwa wapiga kura sio wajumbe wa NEC ya CCM!
 
CCM wasome maandishi ukutani, maana hata maeneo ya vijijini walipokua wanategemea wanatoswa mbaya, hakika Mungu yupo upande wa wenye haki!
 
Nilimshauri hakusikiliza!. Pia nitamshauri aachane na ndoto za urais 2015, Chadema inachukua nchi!.

Kigeu geu... ulimshauri lini? wewe umekuwa mkewe? kama ni hivyo mshauri ahamie CHADEMA, apende sipende, upende usipende saa ya ukombozi inakuja, na tutakumbuka yote mliyotufanyia na kulipa..... tunza bahasha zako...
 
Back
Top Bottom