Matokeo ya Arumeru: Salaam kwa Edward Ngoyai Lowassa!

CDM kumbekeni kamba imekatikia Monduli, mkivuta mtaangukia upande mmoja

Moshi mjini (CDM, Jimbo la Hai (CDM), Jimbo la Arumeru Mashari (CDM) Jimbo la Arusha mjini (CDM), Jimbo la Monduli (CCM), Jimbo la Karatu (CDM, Jimbo la Mbulu (CDM). Bila kuunga kipande kilichokatika itakuwa vigumu kushambulia kwa pamoja kuendelea Bara...Kiteto, Babati, Hanangi na kuendelea
.
 
Nadhani cku zote mbio za sakafuni zinamwisho wake japo mwisho hua ni mgumu sana sisiem wamefika mbio za mwisho
 
Hili la Arumeru lime conclude kwamba huyu Bwana pamoja na tambo na mbwembwe zote hana mvuto kiasi hicho tunachotaka kuaminishwa. Hata Urais anaotaka kugombea ataangukia pua,, hili ndilo litakuwa pigo lake la mwisho na pengine litamuathiri kabisa kiafya. Wako wanasiasa wengine wenye umri mzuri tu wa kugombea urais,, ila si huyu tia maji tia maji

Wananchi 2 Lowa hasa 0 (Sioi na Buriani) mechi ikiendelea
 
CDM kumbekeni kamba imekatikia Monduli, mkivuta mtaangukia upande mmoja

Moshi mjini (CDM, Jimbo la Hai (CDM), Jimbo la Arumeru Mashari (CDM) Jimbo la Arusha mjini (CDM), Jimbo la Monduli (CCM), Jimbo la Karatu (CDM, Jimbo la Mbulu (CDM). Bila kuunga kipande kilichokatika itakuwa vigumu kushambulia kwa pamoja kuendelea Bara...Kiteto, Babati, Hanangi na kuendelea
.
Pana kila sababu ya kuunganisha huu ukanda ili sasa tusonge kuelekea kusini mwa nchi!
 
Ni Dhahiri sasa..,Ufalme wa Lowassa unaanguka na kufikia tamati kama ufalme wa Roma au Utawala wa Gaddafi!

Tulianza na yeye mwenyewe kuanguka uwaziri mkuu mwaka 2008,kwa kashfa ya Richmond

Na pia kushindwa kwa Batilda Buriani kwenye uchaguzi wa Arusha Mjini.2010 (huyu ni mtu wa Lowassa)

Na pia kushindwa kwa James Ole Milya kwenye kura za maoni CCM.mwaka 2010 na vile vile kutoswa kwenye kinyang'anyiro cha kugombea Ubunge Afrika Mashariki mwaka huu. (Huyu ni kibaraka wa Lowassa)

Na pia Kushindwa kwa mkwe wake Sioi Sumari kwenye ubunge wa Arumeru Mashariki..,ni pigo kubwa vile vile Kwa Mheshimiwa Lowassa...,

Hii ni dhahiri ufalme wa Lowassa unafikia mwisho ukizingatia anapata upinzani ndani ya chama chake na vile vile kutoka kwa Chadema (Nguvu ya Umma)

Namfananisha Lowassa na Hayati Muamar Gaddafi jinsi utawala wake ulivyoanguka ni kama sasa hvivi waasi wameuzunguka mji wa Tripoli (CHADEMA) na Wamarekani wakimpiga Mabomu (CCM-Kundi la Sitta)..,kazi ipo kwa yule Mtoto wake wa Kigoma (Peter Serukamba..Mbunge Kigoma Mjini) na yeye mwenyewe anayepatwa na shinikizo la Kujivua gamba..!

Sasa ni Muda wa Mh.Lowassa Kufanya Maamuzi magumu..Kukimbia ama kufa kiume kama Gaddaffi
 
Kwanza anajipanga kusema kwamba CCM imeshindwa kwa sababu hakwenda kwenye kampeni toka mwanzo. Pili atasema amehujumiwa na wagombea wenzake wa URAIS ndani ya CCM, tatu atasema Chadema wamefanya fujo kuwatisha wapiga kura wa CCM.

Lakini kuacha nia yake ya Urais Hawezi! Maji ameyavulia nguo lazima ayaoge. Amewekeza lazima apambane kuona faida. Ana watu nyuma yake hawezi kuwatosa, wataishi vipi? Kuna mambo mengi nyuma ya Lowassa, that's why anapata wakati mgumu hata akisema amechoka, itakuwa ni kishindo kikubwa. Kwa kweli kuna mnyororo wa watu wengi ambao wanaishi kwa matumaini makubwa. Tusubiri tuone.
 
...lowahasa, pole mzee, vita ya vijana huiwezi. Japo ulisema upo tayari kwa mapambano.
 
Kwa tofauti ya kura 6000 inaashiria lowassa na watu wake wameshindwa kabisa..
Lowassa alishinikiza sioi akachaguliwa pamoja na kutokua chaguo la nec..kikwete akaongoza mapambano kuhakikisha lowassa anaanguka
 
Wananchi wakiamua hakuna kitakachowashinda.Huu ni wakati muafaka wa kuonyesha jinsi nguvu ya umma inavyoweza kuleta mabadiliko.Nguvu ya hela haina nafasi tena.Arumeru mashariki wameonyesha njia.Namwomba Mungu aniwezeshe kushiriki uchaguzi wa 2015.
 
Sisi hatujui hayo. Tunachojua ni kwamba kama tutaweza kudhibiti wizi wa kura na vifo kwa wabunge wa CCM vikiongezeka maradufu tunaweza kujirudishia nchi yetu kabla ya 2015 basi.
 
cdm kumbekeni kamba imekatikia monduli, mkivuta mtaangukia upande mmoja

moshi mjini (cdm, jimbo la hai (cdm), jimbo la arumeru mashari (cdm) jimbo la arusha mjini (cdm), jimbo la monduli (ccm), jimbo la karatu (cdm, jimbo la mbulu (cdm). Bila kuunga kipande kilichokatika itakuwa vigumu kushambulia kwa pamoja kuendelea bara...kiteto, babati, hanangi na kuendelea
.

huku labda masia atue kwani watu wa huku ni akheri uwe na wanafunzi wa nasari wanaweza elewa unaongea nini.
 
haaingia akili kuuliza source wakati kitu kinachoelezewa kinafuata logic, ni vihumu kumjibu mtu akisema 2 + 2 = 4 alafu akasema 2 * 2 = 4 tuulize logic. naunga hoja ya Sangarara kuwa formula now ni - x wabunge wa CCM = + X wabunge wa CDM. na hapo bado M4C haijaanza kazi rasim hureee CDM
 
Wanajamvi, poleni na majukum na hongereni kwa kuendelea kufungua milango ya mabadiliko ndani ya nchi yetu tukufu iliyopoteza uelekeo kwa upofu, ubinafsi na hira za wanyonyaji wazawa walaghai na wanyonyaji wa kigeni.

Tudadisi kidogo juu ya ushindi wa kijana Nasari, ushindi wa chadema, ushindi wa wanaarumeru, ushindi wa wanaccm wanopenda mabadiliko na ushindi wa watanzania wote waliochoshwa na mwenendo wa kusuasua kimandeleo katika kutekeleza ilani ya ccm isiyotekelezeka kwa vitendo bali kwa maneno,

Nakumbuka wakati wa kampeni huko arumeru wapo watu kadha wa kadha walijitoa kifadha, kimawazo na mda kumpigia chapuo kijana Sioi Sumari, Kijana aliyekimbilia madaraka kabla baba yake hajamaliza siku 40 ardhini, namkumbuka mzee Mkapa, msema ovyo mwigulu nchemba nadhani huyu kuzaliwa alitanguliza miguu kwani mdomo wake unaonekana kuwa na ugonjwa wa vistula, pili tulimuona mzee wetu, mpenda madaraka na mkwilima bwana Edward lowassa aliyedriki kupanda jukwaani kumpigia kampeni mkwe wake lakini mwisho wa siku kaangukia pua.

Maana yake nini?

Tukumbuke zogo lililoshika kasi mda mfupi baada ya sioi kutangazwa, Zengwe liliibuka huku walio wekisema Salakikya kashinda huku wengine wakisema hapana, wengine wakisema hakufikisha asilimia fulani ya wapiga kura, hizo zote lilikuwa zengwe kwani kama walimtangaza mwanzo je hicho kifungu hawakukijua?lakini kimsingi mapambano hayo lisimamiwa vema na Nape Nnawiye, mzee 6, NA CHILIGATI sterling akiwa JK pale magogoni kashikiria remote mambo yote yakijipa, pesa iliyokatwa ni nyngi kwani pamoja na kurudia kupiga kura ya kumpata mgombea wa ccm bado kijana Nasari alishinda, futina ziliendelea ndani ya chama huku wakisema bora tukose kuliko Sioi kupata na mbinu chafu zilikemewa na kuruhusu uchaguzi wa haki bila kuchakachua kama ilivyozoeleka na mwisho CDM wakashinda, HII inaashiria siasa za mnyukano kuanza kasi upya ndani ya ccm! tutegemee makubwa sana na lazima itakuwa hivyo, nyerere alishayaona.

Tafsiri yake ni ipi?

Tafsiri yake ni kwamba, lengo kuu limetimia la kumpata mbunge, lakini kupanda kwa el kupanda kwenye jukwaa na kama Mkwe wake angeshinda kwanza cdm ingekuwa pigo sana kwani arusha ndo ngome ya chama pili Bwana mamvi anga gain momentum kubwa sna na umaarufu wake ungeongezeka sana ila mwisho wake wa kuangukia pua ni dalili mbaya sana kwani duru za kisiasa zinasema jamaa mbinu zake hazina mashiko yoyote pamoja na jeuri ya pesa yake, iwapo haelewani na malendari ndani ya chama, je atawezaje kukamilisha ndoto zake?mungu ni mwema sana na hana kinyongo na mtu, hutoa kwa mtu anachostahili kupata, waliosubortage hii nchi watalipwa taratibu na dunia nzima itashuhudia. asante Mbowe, Dr slaa na makamanda wa chadema chini ya kampeni Manager Vicent Nyerere!

CDM-winner
CCM looser!

GET WELL SOON MACHEMLI-NANSIO MP
KIWIA HIGHNESS-ILEMELA MP
FITINA ZAO ZINA MWISHO!
 
kila jambo lina mwanzo na mwisho!
 
Back
Top Bottom