Matokeo : Manyara stars v/s uganda.....................

kumbe ndo maana tv za kibongo zilikuwa zinasuasua mi naona julio ni msemaji wa timu hiyo na sio kocha ni hayo tu r i p U 23 Tanzania..
 
Sisi tunasubiri kuoteshwa na MUNGU kuwa tumeshinda kombe la dunia, hatuna jitahada za dhati za kuibua vipaji na kuwekeza kwenye mpira. Maneno mengi, siasa nyingi na IIMANI za kishirikina kila mahali..
 
Jamani si muwe tu wazalendo? Msikimbie huko! Wengine tulishaacha kuhudhuria!
Mimi sikuweza kukimbia, nguvu yenyewe yakuondoka nilikuwa nayo basi, kwanza nimeingia nimechelewa,kuiangalia screen inasoma 2 bila,pale pale nikawepo kuwepo,kipindi cha pili baada ya kupata goli kidogo matumain yakarejea ikabidi nijipongeze na soda, baadaye kidogo tukapigwa la tatu, du nikachoka kama kale kajamaa kwenye tangazo la coca.
 
Ndo yale yale mi shazoea jamani TZ yetu hatufiki popote. Labda kucheza viduku ndo inaweza kututoa! achaneni na soccer jamani ramani yenu haisomeki na haitasomeka unless mikakati thabiti ya kuzibiti walafi pale tff.

Wajiunge na INDIA na Paki kwenye ile michezo ya kike
 
Mimi sikuweza kukimbia, nguvu yenyewe yakuondoka nilikuwa nayo basi, kwanza nimeingia nimechelewa,kuiangalia screen inasoma 2 bila,pale pale nikawepo kuwepo,kipindi cha pili baada ya kupata goli kidogo matumain yakarejea ikabidi nijipongeze na soda, baadaye kidogo tukapigwa la tatu, du nikachoka kama kale kajamaa kwenye tangazo la coca.

jamani kushindwa nako ni moja ya matokeo hahahahahahahhahahhaa
kuna kuzidiana mbinu wakati mwingine, ila kama tuliwatoa Cameroon sijui kwanini Uganda wametushinda labda ni kujisahau
 
Siku moja tutafika. Siku tutakapopata viongozi wa dhati katika siasa, michezo n.k .
Mimi TBC wananiboa sana, inakuwaje huoneshi mechi kama hii. Hili ni shirika la umma, linapata fedha kutoka kodi zetu kwa ajili ya kujiendesha, tofauti na TV binafsi. Jamani, TBC mnategemea nani atuoneshe mechi ya Timu ya Taifa, Chanel 10? Star TV? ama?....Kumbukeni Timu ya Taifa ni timu ya watanzania wote .., Lindi, Masasi, Shinyanga....hawa wote waje dar?
Miaka hii ni ya IT watu tunataka tuwaone Samata, Ulimwengu..wakicheza na si kusikia tu katika redio
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom