Matokeo mabovu ya IV na majibu ya ovyo kwa watendaji husika...tutafika kweli?

Wakuletwa

Senior Member
Oct 31, 2010
134
9
Ndio kila mtu kasikia juu ya uozo wa matokeo haya ya vijana wetu. Kwa kweli nchi ipo njia panda kuhusu elimu. Pamoja na uozo huo wa matokeo kilichonishangaza ni matendo au majibu yanayotolewa na hao wahusika ikiwemo walimu, watu wa baraza la mitihani pamoja nawaandishi wa habari.

1. Nianze na mama Ndali Chako.
Sikufurahishwa kabisa na mtindo huu wa kuonyesha hadharani majibu ya wanafunzi waliojibu majibu ya ajabu. Najua kwanini anafanya hivyo. Anafanya hivyo kama kinga au utetezi juu ya ubaya wa matokeo, lakini kimsingi na kimaadili sio sahihi kufanya hivyo. Mfano mwaka jana yule kijana alieandika BONGO FLEVA alipata sifa sana japo kuwa ni upuuzi alioufanya. Cha kushangaza na redio na Tv zikaanza kumtafuta ili kufanya nae mahojiano nae, matokeo yake ni kuongezeka vitendo hivyo vya kijinga ambavyo kimsingi ilitakiwa kubaki siri. Ndio siri kwa sababu kutangaza upuuzi ule kunatoa nafasi kubwa kwa wanafunzi waliopo kuiga ujinga ule na hatimae kufanya jambo kukua siku hadi siku. Waswahili wana msemo usemao ya Jandoni hayasemwi hadharani..

2. Mitaala mibovu
Nasikitika sana wataalamu wanapodai mitaala mibovu ndio chanzo cha wanafunzi kufanya vibaya. Hii inashangaza sana, nijuavyo mimi kwenye ubofu wa mitaala wanafunzi huenda wakafaulu sana isipokuwa ubora wa elimu yao ndio utakuwa wa kutia shaka. Hata kama mtaala ni mbovu basi na wafaulu kwani wanafunzi hufundishwa kile kilichioandikwa na hatimae kutungiwa mitihani ili kuona uelewa wao juu ya kile walichojifunza. Sasa hata kama walijifunza pumba watajibu pumba sasa hili la mitaala linatoka wapi.

3. Teknojia ya habari na mawasiliano.
Hiki nacho ni kichekesho kingine.Eti wanafunzi wamefeli kwa sababu muda mwingi wapo busy na simu zao hivyo kukosa muda wa kujisomea. Hii mimi sikubaliana nayo nilitaraji kuwa kwa uwepo wa teknolojia hii ingekuwa rahisi kwa wanafunzi kufanya vizuri kwani taarifa nyingi za masomo zipo humo kwenye mitandao. Tatizo hapa ni jamii kwa ujumla kuwasimamia watoto wetu nini cha kufanya na kwa wakati gani wa kufanya.

4. Walimu wasio na sifa.
Hii nakubaliana 100% ni kweli kuwa walimu tulionao sasa wamekosa ubora unaostahili juu ya ufundishaji wa watoto wetu. Walimu wachache wazuri tulionao hawakidhi mahitaji ya nchi kwa ujumla sasa basi inabidi jitihada za kina na utashi wa hali ya juu kuhakikisha kuwa walimu wanakuwa bora kwa kiwango kinachohitajika.


Naomba kutoa hoja.
 
Muhim kabla ya kuwashambulia vijana wetu ni muhm sana viongoz wa wizara na baraza la mitihan wawajibike. Cdhan kama vijana wa tanzania wanaupungufu wa akili

Pia hatukuwaweka pale kama mahakim wa elim bac kwamba matokeo yakiwa mazur au mabaya wao hawahucki mishahara yao ibakie safe No wako pale kuhakikisha ubora wa elim na majibu yanatupa picha kwamba wameshndwa bas n wajibu wao kung'atuka wawapishe watanzania wengne warekebishe hali

Pia kuna tuhuma za uchakachuaj matokeo, kwa mfano mkurugenz wa shule moja kataja majina na namba za wanafunz ambao hawakufanya mtihan lakn wamejaziwa kwamba wamefanya na wamefaulu. Ni muhm sana kuvivunja vyombo hv dhaifu vya usimamiz wa elimu na kuunda vyombo vipya
 
Back
Top Bottom