Matokeo Kidato cha Sita 2009

Nakumbuka wakati namaliza A-level darasani letu karibu watu 12 walipata division one PCM but wote walienda kusoma BCom Udsm .Darasani tulikuwa 60 na karibia wote tulienda vyuoni lakini walioenda kusoma Science hata 10 hawafiki
Serikali inatakiwa kuliangalia hili suala bila hivyo wanafunzi wengi watasoma Science wakifika vyuoni wanakimbilia Uhasibu na Biashara
 
Last edited:
Kwa wale wanaofuatilia matokeo haya wanaweza kutembelea hii link:

http://www.necta.go.tz/acsee2009/acsee2009.html

Ahsanteni
 
Nakumbuka wakati namaliza A-level darasani letu karibu watu 12 walipata division one PCM but wote walienda kusoma BCom Udsm .Darasani tulikuwa 60 na karibia wote tulienda vyuoni lakini walioenda kusoma Science hata 10 hawafiki
Serikali inatakiwa kuliangalia hili suala bila hivyo wanafunzi wengi watasoma Science wakifika vyuoni wanakimbilia Uhasibu na Biashara

Mzee, usiniambie kuwa na wewe ni mmoja wa waliokimbia sayansi...tehe tehe tehe tehe
 
No Mpita Njia mimi ni mmojawapo ya wachache tuliobaki kwenye sayansi
 
S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL DIV-I = 34 DIV-II = 67 DIV-III = 115 DIV-IV = 40 FLD = 32
chama langu lazamani div zero nyingi sana

S0342 SHAABAN ROBERT SECONDARY SCHOOL DIV-I = 30 DIV-II = 33 DIV-III = 44 DIV-IV = 4 FLD = 0
hawa jamaa siku hizi wanafaulu wame improve kiasi hicho mhhh

S0347 TAMBAZA SECONDARY SCHOOL DIV-I = 33 DIV-II = 74 DIV-III = 224 DIV-IV = 72 FLD = 56
hawa jamaa na kufeli kwingi sana

S0335 MZIZIMA SECONDARY SCHOOL DIV-I = 0 DIV-II = 6 DIV-III = 17 DIV-IV = 5 FLD = 9
hawa jamaa walikuwa wanafanyiwa practicals zote enzi zetu sijui siku hizi imekuwaje maana yake hamna hata one moja​
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake

Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!
 
Mkuu, I support your observation.

Tatizo siku hizi nchi yetu imeshakuwa ya ujanja ujanja..kila mtu anataka maisha ya mkato. NANI aende FoE kuvaa overoli..wakati anajua akila Bcom...anaingia CRDB au NMB chapchap? I can assure you, at least from experience..asilimia kubwa ya hawa vijana wataishia Biashara na Law....au Computer Science...Vijana wanajitahidi..swala ni serikali kurudisha heshima ya elimu kwa ujumla. Unapomuona Professor wa Physics na Chemistry akiwa frustrated kwa mshahara mdogo..wakati akina Chitalilo darasa la saba wakiwa wanapeta..you wonder what is wrong with a young man going to specialize in Bs Physics au Chemistry...Ukweli siku hizi ni vigumu sana kwa Tanzania yetu kuukimbia umasikini kupitia taaluma ya sayansi. Inwezekana lakini ni ngumu mno. Zamani mtu alikuwa akipata A ya kemia au hisabati..anaonekana kipanga..lakini siku hizi....hali imebadilika sana. Utakuta "ngwini" waliokuwa wanachekwa..ndo wameshikilia mpini...Sayansi unasoma...na GPA yako nzuri....inabidi ukapange foleni Vodacom au Zain..kupanda minara.....We really need to put science in its rightful place. For now..we are on a wrong course.

Masanja huu i ukweli tena ukweli unao umma,

Taifa lisipo fanya kitu, tutaangamia si uongo. Vijana wote wenye akili sana siku hizi wanaikimbia sayansi, hawataki kuwa madaktari kwani mshahara wa daktari ni laki nne, nani hataki kwenda kuwa PR wa vodacom alipwe dola 3000 kwa mwezi?

Lakini fikiria kama kila mwenye akili atakimbilia huko unguin, sheria, biashara, tutatpata wapi madaktari wazuri? maengin. archtech, n.k? Mpaka serikali itakapo tambua umuhimu wa watu hawa na kuanza kuwalipa vyema sijui kama tutakuwa bado tuko salama.

Nchi zingine zilizo endelea, madaktari, ma eng. na sayansi kwa ujumla wanapata malipo mazuri, na ajira nyingi kwenye viwanda mbali mbali., Bongo yetu hata viwanda hakuna tumebaki kuwa dampo la wachina!
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake

Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!

Mkuu,

Hakuna bahati wala nini..ni kusota tuu ndugu yangu. Mtu kama umekulia kwenye familia ya kiwango cha kati au cha chini..na ukawa na uelewa..unajua kabisa elimu ndo mkombozi wako.

Tatizo la vijana wengi siku hizi..especially hawa wanaosoma academies kwa kuchukuliwa na magari special nyumbani kwao....wanakuja kujua umuhimu wa elimu wakishamaliza shule na kufeli..wakiingia mtaani ndo wanagundua kwamba life halina shortcut (unless wewe ni mtoto wa Lowassa au vingunge wengine wachache wa CCM..ambao ukimaliza shule uwe na zero au div. one utapelekwa Uingereza..na siku hizi naona wanapelekwa China na India) Otherwise..msingi wa mtoto kufaulu masomo..ni kujua umuhimu na nafasi ya shule katika maisha yake ya kila siku. Hakuna miracles. If you work hard with determination and discipline. Hakika utavuna. Ingawa siyo kwa mwendo wa DECI-Lol!
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake

Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!

Economics A; duh...mkuu huyu anastahili hongera sana...hilo somo liko "tricky" sana.
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake

Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!

Hongera zake, naamini wazazi wake wamefurahi sana. Inatia moyo kuona mtoto amejitahidi shuleni na amefumua vizuri.
Hata wewe kama ni mzazi unaelewa kuwa jitihada binafsi za mtoto/mwanafunzi ndiyo kigezo cha kufaulu. Mengine ni ziada kama kwenda na taxi au gari shule.
Umpe zawadi yake,usije kusahau!!

Economics A??!!si mchezo...
 
BelindaJacob,

1. Nimemwambia nitamnunulia laptop..ni ahadi yangu lazima niitizime kabla hajanza chuo. Ndo anauliza asome nini?? ana A 3 ktk Econ, Hist. & Geog.

2. Pia O level alipata A 8..na alikuwa kati ya binti waliopewa zawadi na JK 2007.

Yaani kila mtu amefurahi..tangu wazazi, waalimu hadi majirani!
 
Inapendeza pia chaguo la zawadi ni zuri sana aende na teknolojia. Kuhusu asome nini chuoni, inategemea kama amefocus kuwa na career ipi na options anazo ni kuamua mojawapo kati ya atakazo-opt.

Binti kipanga huyo, f4+6 kafanya vizuri kwakweli na anastahili kupongezwa ili kuona jitihada zake zinathaminiwa sanasana na wazazi.Bravo!!
 
chama langu lazamani div zero nyingi sana

Siku hizi wame-import sketi pale mzee..lazima graph i-decay ..Si unajua tena utozz mwingi ^_^

Hao watoto wa Mzizima kweli walikuwa wanalishwa huku wakiwa wamesinzia, sijui siku hizi imekuwaje? Labda channel zao za NECTA kwishehi, c unajua bongo uwizi mtupu
 
BelindaJacob,

1. Nimemwambia nitamnunulia laptop..ni ahadi yangu lazima niitizime kabla hajanza chuo. Ndo anauliza asome nini?? ana A 3 ktk Econ, Hist. & Geog.

2. Pia O level alipata A 8..na alikuwa kati ya binti waliopewa zawadi na JK 2007.

Yaani kila mtu amefurahi..tangu wazazi, waalimu hadi majirani!

Mkuu hapa ni murua kabisa.

In all all economics kupata A kwa kweli anastahili pongezi..I got a B of economics..though I never became one....I dont regret where I ended up. Its a good feeling kufaulu economics. Trust me. Ila nilikuwa nalaza miguu kwenye karai la maji ya baridi mpaka alfajiri! Duh..ama kweli mtaka cha uvunguni sharti..ainue kitanda--oopss..ainame...This is the period I learnt that maisha siyo lelemama...Yaani I had no alternative. I either had to pass or pass. Failure was not an option on the table. Siku hizi watu wana option ya kufeli.

By the way..ni vyema mmpe ideas ni course gani akasome pale mlimani au kwingineko, (au wazazi wanampeleka China huyo mtoto-lol). Otherwise kama ni hapa bongo..awe careful with open mind na university opportunities! She/he will excel!
 
Raha sana kuna mtoto wa jirani alikuwa Jangwani kapata pointi 3..yaani History A, Geog. A na Economics A!!

Halafu alikuwa anapanda tu daladala, anakaa Ubungo, ama kweli kila mtu na akili na bahati yake

Kudadeki: inabidi nimnunulie zawadi nzuri!

hehehehe hiyo zawadi inabidi umpe mzazi sio yeye tutakwelewa vibaya mkuu...
 
BelindaJacob,

1. Nimemwambia nitamnunulia laptop..ni ahadi yangu lazima niitizime kabla hajanza chuo. Ndo anauliza asome nini?? ana A 3 ktk Econ, Hist. & Geog.

2. Pia O level alipata A 8..na alikuwa kati ya binti waliopewa zawadi na JK 2007.

Yaani kila mtu amefurahi..tangu wazazi, waalimu hadi majirani!

Mkuu,

Kama ni zawadi basi umemchagulia nzuri sana...nakupa hongera na wewe kwa kuonyesha moyo huo; safi sana.

Mimi ningeshauri aangalie katoka masomo yote aliyosoma ni lipi analipenda kwa DHATI na kwamba yeye binafsi anaamini amelipasi kwa jitihada nafuu kuliko mengine yote. Kupata A masomo yote 3 inaonyesha anayapenda na kumudu yote lakini lazima kuna moja linazidi mengine, na hilo ndilo namshauri alikomalie mpaka chuo kikuu...huko pia atafanya vizuri sana...akifaulu digrii vizuri then sky's the limit.

Asifanye kosa la kuangalia na kufuata demand iliyopo kwenye "Job Market" kwa wakati huu ndio imchagulie somo la Chuo Kikuu...nilifanya makosa hayo na ilipofika kipindi namaliza Chuo job market ilikuwa imebadilika sana ikanibidi kujifunza skills nyingine upya.

Kila la kheri.
 
Du ukiyaangalia haya matokea kwa makini utaona ni matokeo ya shule zaid kuliko watoto binafsi. Utaona shule either imefaulisha wanafunzi au imefelisha. Nawaonea huruma watoto waliofelishwa na shule.
 
Mkuu,

Kama ni zawadi basi umemchagulia nzuri sana...nakupa hongera na wewe kwa kuonyesha moyo huo; safi sana.

Mimi ningeshauri aangalie katoka masomo yote aliyosoma ni lipi analipenda kwa DHATI na kwamba yeye binafsi anaamini amelipasi kwa jitihada nafuu kuliko mengine yote. Kupata A masomo yote 3 inaonyesha anayapenda na kumudu yote lakini lazima kuna moja linazidi mengine, na hilo ndilo namshauri alikomalie mpaka chuo kikuu...huko pia atafanya vizuri sana...akifaulu digrii vizuri then sky's the limit.

Asifanye kosa la kuangalia na kufuata demand iliyopo kwenye "Job Market" kwa wakati huu ndio imchagulie somo la Chuo Kikuu...nilifanya makosa hayo na ilipofika kipindi namaliza Chuo job market ilikuwa imebadilika sana ikanibidi kujifunza skills nyingine upya.

Kila la kheri.

Wazee ahsante kwa ushauri,

Ni hivi wazazi wake hawana uwezo asome nje ya Tz na pia ana wadogo zake nao wanasoma!

Yeye anasema somo alililiopenda zaidi ni Economics na pia alipata A. Je vipi mnashaurije akisoma Pure Ecomomics course BA (Econ.) say Mlimani? Then akaja kuwa Economist!

Au vipi akisoma BCOM ambapo pia ili awe na uwanja mpana zaidi ya Economics? Y

Je asome Laws?

Family background wazazi ni watu wa kipato kidogo: na anategemewa aje kuwasidia wadogo zake ili kuwapunguzia mzigo wazazi wake..na ndo maana alishauriwa achukue masomo ya Arts ili pengine apate kazi mapema ili aweze kuwasaidia wazazi na wadogo zake!

Tunaomba mawazo!
 
Back
Top Bottom