Matokeo kidato cha nne

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
p { margin-bottom: 0.08in; } Nawashangaa wanaoyashangaa matokeo ya kidato cha nne


Na Juma Kidogo


Ni siku nyingine tena ndugu zangu wapendwa tunakutana katika makala hizi tamu za kupendeza.
Nawaandikia makala haya wakati ambapo jahazi kongwe la nchi yetu linazidi kwenda mrama. Nyangumi na mapapa wenye hasira wamemega upande wa Jahazi hili na kusababisha maji kuanza kujaa taratibu huku nahodha akijaribu kuliokoa bila ya mafanikio.
Kila kitu kinakwenda ndivyo sivyo, umeme hakuna wa kutosha na, wakati wowote kuanzia sasa nchi nzima huenda ikagubikwa na giza nene kutokana na mgao wa umeme usio na kikomo.
Hali ya maisha kwa wananchi wa hali ya chini sasa imekuwa ngumu kupita kiasi huku watawala wetu wakila vyakula na familia zao mpaka wanasaza bila ya kujua kuwa Watanzania wanaoishi chini ya dola moja wanapata mateso makubwa. Lakini siku zinaasonga mbele, wanachi hawa ni wapole sana, wananyamaza kimya.. hawana shida ya kuandamana ili kuishinikiza serikali yao iondoke madarakani kama huko Misri na kwingineko duniani.
Wanaogopa kupasuliwa vichwa vyao kwa risasi za moto kutoka kwa askari wa kutuliza ghasia, kwa kuhofia maisha yao kupotea, wanaamua kufa na tai zao shingoni. Wanaamua kufa kikondoo.
Akari ambao nao hata kodi zao za nyumba zinawashinda huko mitaani, askari ambao wanaishi katika vijumba vya bati maarufu kama fulusuti. Niachane na hayo, niachane na hayo kwa sababu haikuwa mada yangu kuu kwa leo, leo nimelenga kujadili japo kwa ufupi kushuka kwa kiwango cha elimu katika nchi yetu. Elimu ni muhimu katika ujenzi na maendeleo ya Taifa hili, bila ya elimu Taifa linaweza kujikuta likiwa na watu wajinga kila kona hapo baadae, viongozi watawala watakuwa wajinga, raia watawaliwa nao watakuwa wajinga pia.
Yapo mambo mengi sana yanayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini lakini leo ntagusa machache sana. Wiki chache zilizopita Baraza la mitihani lilitangaza matokea ya mitihani ya kidato cha nne. Matokeo ambayo yalikuwa mabaya kiasi cha kuwashangaza watanzania walio wengi wakiwemo viongozi wenye dhamana kubwa ya kuliongoza Taifa hili.
Wote wanashangaa wakitafakari sababu ya matokeo hayo mabaya hasa kwa shule hizi za kata. Kwa upande wangu mimi siyashangai matokeo haya kwani nilikuwa najua tangu siku nyingi kuwa yatatokea. Nawashangaa wale wote ambao wanayashangaa matokeo hayo.
Nawashangaa kwa sababu sioni kitu cha ajabu ambacho wanakishangaa. Sababu kubwa ya matokeo haya mabaya ni sekondari hizi za kata, ni sekondari za kata kwa sababu wale wote wanaopata sifuri ni wale ambao hawakuwa na sifa za kuendelea na masomo ya sekondari.
Nimewahi kuwa mwalimu nikifundisha katika shule ya za msingi na baadae sekondari, sifa na uwezo wa wanafunzi wanaochaguliwa kujiunga na shule hizi naufahamu vizuri sana.
Hebu chukulia kuwa kata moja ina shule moja ya sekondari pamoja na mbili au tatu za msingi. Ili shule hiyo ya sekondari itimize idadi ya wanafunzi wanatakiwa kujiunga na shule hiyo inabidi ichukuwe wanafunzi wote wanaomaliza darasa la saba katika shule za msingi zilizomo katika kata hiyo.
Jiulize hapa mwanafunzi ambaye alikuwa akishika nafasi ya 30 katika darasa la saba matokeo yake yatakuwaje huko sekondari? Mwanafunzi ambaye alishindwa kujibu swali katika lugha ya Kiswahili atawezaje kujibu swali hilohilo achilia mbali swali jipya katika lugha ya kiingereza.
Hapa ipo sababu ya kushangaa na kuanza kujiuliza maswali eti nini kimetokea? Kwa nini tunasahau maana halisi ya kufanya mitihani?
Kutahini lengo lake kuu ni kuchuja kilicho bora kutoka katika kundi moja na kwenda kuchanganya na vingine vilivyo bora ili kuacha makapi. Sasa makapi yanaonekana bayana, makapi ni wale wote ambao hata ukiwapa miaka mia warudie mitihani ya kidato cha nne bado wataambulia patupu.
Tuwape maarifa tu vijana hawa lakini wakipiga chini katika mitihani yao tusianze kutizamana nyuso zetu tukimsaka mchawi huku tukiwa tumesahau kuwa tumejenga mashule mengi ambayo hayana watoto wa kutosha kufaulu vyema katika ngazi hiyo ya elimu.
Hebu jiulize swali dogo, ulipokuwa ukisoma darasa la saba katika mitihani mliyokuwa mkifanya kulikwa hakuna mwanafunzi aliyekuwa akishika mkia?
Je unategemea matokeoa gani kwa mwanafunzi huyo atakaposukumwa na kujikuta akiwa sekondari.
Tena kwa bahati mbaya zipo sekondari za kata ambazo hujikuta zikiambulia idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa wakishika nafasi za chini katika shule zao, hawa wanategemea wafundishwe na walimu ambao ni manabii kama Yesu ili wafaulu katika viwango vinavyotakiwa.
Ndio maana shule za binafsi huwa zikifanya usaili kabla ya kuwakubali vijana wanaojiunga na shule zao..
 
sio hilo tu mkuu tukumbuke hawa wanafunzi wa mwaka 2010 ndio wale ambao mheshimiwa sana Raisi wetu aliamuru kuwa kuanzia mwaka 2008 wasirudie mwaka wakifeli kidato cha pili.

Kwa kweli tusitafute mchawi kuhusu hili,mchawi anajulikana. na kama hatuamini afute tena kufeli kidato cha nne na miaka miwili badaye tuone matokeo ya kidato cha sita.
Nakuambia mchawi anajulikana
 
:rain: Mimi sishangai lakini naisikitikia nchi yetu. Nashukuru Mungu maana kufutwa kwa mtihani wa mchujo kidato cha pili,umeficha mengi ambayo yangewafumbua macho watanzania walio wengi.Hali ya matokeo inaonyesha kwamba kama mtihani wa mchujo kidato cha pili ungeendelea kuwepo,tungeshuhudia shule nyingi zikikosa kabisa wanafunzi wanao faulu kuingia kidato cha tatu,hivyo hata hao kidato cha nne ambao tunaona hawakufanya vizuri mwaka huu wasingepatikana.

 
:rain: Mimi sishangai lakini naisikitikia nchi yetu. Nashukuru Mungu maana kufutwa kwa mtihani wa mchujo kidato cha pili,umeficha mengi ambayo yangewafumbua macho watanzania walio wengi.Hali ya matokeo inaonyesha kwamba kama mtihani wa mchujo kidato cha pili ungeendelea kuwepo,tungeshuhudia shule nyingi zikikosa kabisa wanafunzi wanao faulu kuingia kidato cha tatu,hivyo hata hao kidato cha nne ambao tunaona hawakufanya vizuri mwaka huu wasingepatikana.

 
Back
Top Bottom