Matokeo kidato cha nne ni standardization ya matokeo halisi baada ya wanafunzi kufeli

Nicazius

Senior Member
Feb 6, 2008
143
17
Habari za KI-Intellegence: MATOKEO KIDATO CHA NNE NI STANDARDIZATION YA MATOKEO HALISI BAADA YA WANAFUNZI KUFELI KUPITA KIASI.

HABARI NILIZO ZIPATA KUTOKA SOURCE MOJA ILIYOKUWA KWENYE KUSAHIHISHA MITIHANI NI KUWA WANAFUNZI WALIFELI SANA MWAKA 2010 KIASI CHA HALI KUWA MBAYA NA NECTA KUAMUA KUFANYA STANDIZATION AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA, KIASI KWAMBA BAADHI YA 'B' ZILIPELEKWA NA KUWA 'A' NA ZILE 'C' CHOKA MBAYA KUWA 'B'

MATOKEO YALIKUWA MABAYA ZAIDI KWENYE SHULE ZA KATA, KWANI MATOKEO YA SAFARI HII NDIYO UZAO WA KWANZA WA SHULE ZA KATA (SHULE ZA KIKWETE), SWALI NI KWANI NINI NECTA WALIAMUA KUFICHA UKWELI WA MATOKEO HALISI KIASI HIKI? AU WALIOGOPA WANANCHI KUHOJI MWASWALI NA KUJUA HALI ILIVYO MBAYA KWA SHULE ZA KATA?

NAENDELEA KUFANYA UTAFITI, NITAKUJA NA UKWELI ZAIDI...
 
kwa kweli hakuna kitu kilicho niudhi mwezi huu wa kwanza kama hoyo matokeo.Hiv mmewahi kujiuliza kwa nn mtihani wa kidato cha pili ulifutwa?:A S 20:
 
Mkuu ukiyapata matokeo halisi itakua vizuri.shule za kata zifungwe tubakie na shule chache ambazo zitapewa huduma nzuri.
 
hapo ndio anguko la jk linapoanzia. hawa vijana waliofeli wan ghadhabu na jk ni ukweli ni kuwa ndio watakao mhukumu jk na ccm yake 2015
 
Hali ya elimu katika nchi yetu inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na kila matokeo yanapotangazwa kumekuwa na sintokufahamu pasina kuchukuliwa tahadhari ya nini kifanyike kukomboa nchi. Ni lazima kurudisha mfumo wa zamani wa elimu yenye tija na yenye ushindani ili kuinua kiwango cha elimu kwa ujumla.

Tuanze na kurudisha ushindani wa darasa la 4 ilirudi kama zamani kama mwanafunzi amefeli basi arudie. Kisha shule za sekondari ziwe na mitihani ya mwisho wa mwaka ambayo mwanafunzi akishindwa kufikisha wastani basi na arudie darasa hii itawasaidia wanafunzi wengi kujijengea hali ya kusoma mara kwa mara tofauti na hali ilivyo sasa ambapo watoto wengi hawasomi mpaka ifike kidato cha nne karibu na mitihani ndio wanashituka. IKibidi shule za kata basi zipunguzwe ili zilite tija badala ya kugeuka kuwa viwanda vya zero kama ilivyo sasa.
 
Sipati picha hawa vijana wooote wliofeli watafanya nini? Hope wote watajiandikisha kupiga kura na kuitumia vema kura yao, maana watakuwa wakisema 'nimemaliza form four lakini sina kazi na sina pa kwenda' .... poleni sana vijana wangu hakuna jinsi ambavyo mngefaulu kwakweli inauma na kusikitisha sana ... hipe at least compulsory education itapanda angalau iwe form six ili vijana kama hawa miaka ijayo wawe na nafasi ya kuadjust lau hata dk za mwisho
 
Hali ya elimu katika nchi yetu inazidi kuwa mbaya siku hadi siku na kila matokeo yanapotangazwa kumekuwa na sintokufahamu pasina kuchukuliwa tahadhari ya nini kifanyike kukomboa nchi. Ni lazima kurudisha mfumo wa zamani wa elimu yenye tija na yenye ushindani ili kuinua kiwango cha elimu kwa ujumla.

Tuanze na kurudisha ushindani wa darasa la 4 ilirudi kama zamani kama mwanafunzi amefeli basi arudie. Kisha shule za sekondari ziwe na mitihani ya mwisho wa mwaka ambayo mwanafunzi akishindwa kufikisha wastani basi na arudie darasa hii itawasaidia wanafunzi wengi kujijengea hali ya kusoma mara kwa mara tofauti na hali ilivyo sasa ambapo watoto wengi hawasomi mpaka ifike kidato cha nne karibu na mitihani ndio wanashituka. IKibidi shule za kata basi zipunguzwe ili zilite tija badala ya kugeuka kuwa viwanda vya zero kama ilivyo sasa.

Hili ni swala muhimu sana, kwani hata mimi wakati niko primary nilianza kusoma nilipofika darasa la nne na pia wakati naingia form two ndio nilikaza buti kwani nilijua nikifeli hapo narudia mwaka, mtindo wa kuwarudisha madarasa au kuwatimua shule waliofeli kabisa itasaidia wengi kusoma na kupata matokeo mazuri kuliko zero za mwaka huu.
 
Habari za KI-Intellegence: MATOKEO KIDATO CHA NNE NI STANDARDIZATION YA MATOKEO HALISI BAADA YA WANAFUNZI KUFELI KUPITA KIASI.

HABARI NILIZO ZIPATA KUTOKA SOURCE MOJA ILIYOKUWA KWENYE KUSAHIHISHA MITIHANI NI KUWA WANAFUNZI WALIFELI SANA MWAKA 2010 KIASI CHA HALI KUWA MBAYA NA NECTA KUAMUA KUFANYA STANDIZATION AMBAYO HAIJAWAHI KUTOKEA, KIASI KWAMBA BAADHI YA 'B' ZILIPELEKWA NA KUWA 'A' NA ZILE 'C' CHOKA MBAYA KUWA 'B'

MATOKEO YALIKUWA MABAYA ZAIDI KWENYE SHULE ZA KATA, KWANI MATOKEO YA SAFARI HII NDIYO UZAO WA KWANZA WA SHULE ZA KATA (SHULE ZA KIKWETE), SWALI NI KWANI NINI NECTA WALIAMUA KUFICHA UKWELI WA MATOKEO HALISI KIASI HIKI? AU WALIOGOPA WANANCHI KUHOJI MWASWALI NA KUJUA HALI ILIVYO MBAYA KWA SHULE ZA KATA?

NAENDELEA KUFANYA UTAFITI, NITAKUJA NA UKWELI ZAIDI...

Mimi nafikiri yale matokeo yaliotolewa mwaka jana ndio walistandardize. Je umeishasahau yale ya mwakajuzi waliopata daraja la kwanza, pili na tatu walikuwa ni asilimia17 tu ya watahiniwa wote wa darasa la kumi na mbili, form four? Naomba uelewe kuwa kufanya vibaya, kufeli, hakujaanza mwaka huu bali ni kansa, mdudu anaekula maendeleo ya Tanzania taratibu. Chukulia stem hii ya kufeli ikiendelea kwa miaka 5, sawa na muda wa siasa wa wabunge na rais, tutakuwa tumetengeneza taifa gani. Kumbuka ukipata daraja sifuri au la nne haupewi cheti, so nisawa na darasa la saba tu. Bora wangerudisha ile mitaala ya ufundi stadi mashuleni labda tungeweza kitengeneza wajasiliamali wawiliwatatu kati ya fungu linalofanya vibaya wakawezakujifungulia vijiwe vyao mitaani badala ya kuwa wazururaji na wababaishaji.
 
mfumo wa elimu TZ ni miongoni mwa mifumo mibovu duniani...! mtoto anaanza chekechea hadi f4 bila kuchujwa kwa mitihani...! lengo ni nini, kutembea tumbo mbele ukijidai eti kiwango cha wanafunzi shuleni imeongezeka kwa asilimia kubwa kumbe uozo mtupu...! wanawapotezea watoto wa watu muda bure, hizo sifuri watazifanyia nini, skills zozote hawana, bora hizo shule za kata zigeuzwe 'vocational training center' miaka 4 lazima mtu atoke na ujuzi fulani...CCM, CCM, CCM mmewageuza watoto wa walalahoi wa nchi hii matambara ya deki, ole wenu....!
 
Na bado so soon tutapewa TUZO ya ELIMU BORA na Umoja wa mataifa ! Hawa viongozi wetu wanastahili ya Mubarak !
 
Duh! Kwa matokeo niliyoyaona,basi ilikua ni failure ya ajabu! Yaani kwa upupu huo niliouona,kumbe umekua standardised?!

Hapa tusipoishinikiza hii serikali dhalimu kuondoka,hakika hata MUHAS wataambiwa wastandardise matokeo ya wanafunzi wa udaktari!
 
smilie.png
kuna umuhimu wa kuliangalia upya hili suala la kufungua shule nyingi za kata bila kujali uwepo wa walimu bora wenye vitendea kazi vya kutosha. nadhani ni wakati wa kuona uelekeo wa nchi kwa jicho la hayati mwalimu JK Nyerere.
 
Ili kuiokoa thamani ya elimu nchini ni lazima turudi tulipotoka.Tupunguze idadi ya shule za sekondari at least kila tarafa iwe na sekondari mbili.Hii itafanya nafasi ya kuendelea na masomo ya sekondari kwenda kwa watoto ambao kweli wamefanya vizuri mitihani yao ya la saba.Tukubali ukweli kwamba sio kila mtoto anayamudu masomo ya sekondari.Mtindo wa sasa wa kujaza nafasi ili kupata takwimu kubwa ziwanufaishe kisiasa watawala ndo unaomaliza taifa.Shule zile ambazo zitaachwa ndani ya tarafa tuzigeuze kuwa vocational training centres na vyuo vya kilimo ambavyo vitawapa ujuzi wa fani mbalimbali wale watakaokosa nafasi ya elimu ya sekondari ili waweze kujitegemea na kuinua uchumi wa taifa.Shule mbili teule ndani ya tarafa zipewe uwezo kwa kuwa na walimu wote ndani ya tarafa,kupewa vifaa na vitabu, kujengewa library bora,nyumba za walimu,maabara nk.Turudishe mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili na watakaofeli wakariri darasa.Mi nadhani yakifanyika haya hatutakuwa na matokeo kama haya.
 
Back
Top Bottom