Matokeo KAMILI ya bunge la EALA

Walisahau kundi la Wanaume, Watoto, Vijana, Wazee na Makundi ya kidini.

Yaani kwa kifupi namaanisha aliepanga uchaguzi wa kuwakilisha taifa uwe kwa makundi hana upeo mzuri wa mawazo. Hii ni kuligawa taifa na kupunguza uwajibikaji wa wahusika! kila mwakilishi hapo ana kundi lake na kibaya zaidi amepelekwa na chama fulani, kwa hiyo hoja itakayokua nje ya kundi lake au chama chake kilichompeleka haitapata msemaji mwenye kujua kwamba ni jukumu lake.

Ukweli hii nchi sasa imekuwa na mambo ya ajabu,hadi Bernard Mrunya nae eti leo hii anakuwa mbunge wa bunge la Africa Mashariki.
 
Mfano kundi la kina mama. Ukijumlisha idadi ya kura zao (waliopigiwa kura) unakuta ni 588 lakini cha ajabu wabunge waliopiga kura walikuwa 305 tu. Hizo nyingine zimetokea wapi? Au kulikuwa na utaratibu gani wa kupiga kura?

Mchanganuo bado hautoshi kuchochea mjadala, ingekuwa vizuri ungeonesha kila mgombea na kura alizopata na jumla ya kura katika kundi hili
 
Hivi inakuwaje ukipiga hesabu ya idadi ya kura kwa kila category unakuta imezidi idaidi ya wapiga kura ambao walikuwa 305 tu.

Kumbuka wapiga kura walikuwa wanachagua mtu zaidi ya mmoja kwenye kila kundi.
 
Walisahau kundi la Wanaume, Watoto, Vijana, Wazee na Makundi ya kidini.

Yaani kwa kifupi namaanisha aliepanga uchaguzi wa kuwakilisha taifa uwe kwa makundi hana upeo mzuri wa mawazo. Hii ni kuligawa taifa na kupunguza uwajibikaji wa wahusika! kila mwakilishi hapo ana kundi lake na kibaya zaidi amepelekwa na chama fulani, kwa hiyo hoja itakayokua nje ya kundi lake au chama chake kilichompeleka haitapata msemaji mwenye kujua kwamba ni jukumu lake.

Ukweli hii nchi sasa imekuwa na mambo ya ajabu,hadi Bernard Mrunya nae eti leo hii anakuwa mbunge wa bunge la Africa Mashariki.

Tatizo kwa sasa CCM wanainjoy hiyo power waliyonayo ya mojority bungeni........... kunasiku watakuwa wanalilia hizo kanuni na sheria zibadilishwe wakati wapinzani watakuwa wameshika mpini. Time will tell!!
 
Duh, kweli Magamba noma, yaani pamoja na Mrisho Gambo kujieleza kwa ufasaha na kuonyesha uwezo wa juu katika kujibu maswali aliyoulizwa lakini hajapewa?
 
Matokeo ya bunge la EALA

3. Kundi la Wapinzani
No.
Jina
Chama
Kura
1
Nd. Antony Calist Komu
CHADEMA
93
2
Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha
UDP
58
3
Nd. Juju Martin Danda
NCCR-M
23
4
Nd. Micah Elifuraha Mrindoko
TLP
66
5
Nd. Mwaiseje S. Polisya
NCCR-M
42
6
Nd. Nderakindo Perpetua Kessy
NCCR-M
113
7
Nd. Twaha Issa Taslima
CUF
175

Hapa CCM kwa makusudi waliamua kum support mke wao CUF
 
Hiyo ndio bongo ndugu yangu,Mpaka wakukubali magamba lazima kuna kitu umewapa,imagine yule Mbene na Mndolwa walivyokuwa wanapangua maswali kama vile hamnazo,Na ni vichwa ambavyo watanzania wanavikubalia sana,
Angela Kizigha,Anyway huyu nasikia ni mzigo wa mtu ndio maaana watu walipambana mpaka akapita,Kweli Komu alipwaya hiyo wote tunakubali na pia Cuf na Tlb ni CCM hilo tupende tusipende.Ingawa wa TLP She deserve it PHD in Marthematics..... haha hilo ni katapila ni zaidi ya jembe.
 
Mimi nimefurahi, Charles Makongoro Nyerere kupata, kwanza anajua kujieleza, inaonekana hana jazba na anaweza kujenga hoja. Pia nimefuahi at least tunapata mtu kutoka kizazi cha mwalimu ingawa sina hakika kama na yeye ana uzalendo kwa Tanzania kama baba yake. Tuwape ushirikiano wakatuwakilishe vyema EALA.
 
Kumbea hata huyu ex-demu wa Jaffarai nae kapata tena kuanzia mchakato wa mchujo? Hivi ni ulize wadau huyu kicheche nani anamlinda aisee, maana kila akigombea kitu lazima apate au chakula cha wakubwa huyu?
 
Hivi jamani, hadi leo sijaelewa jambo moja.Ali Hassan Mwinyi kazaliwa wapi? Na je ni Mbara au Mzanzibari??
Knowledge yangu inajua Mwinyi ni Mbara, Zanzibar kapelekwa na Ticha, akawe Rais, majuzi dogo wake - Hussen alikuwa mbunge wa Mafia, mara sasa hivi ni mbunge huko Z'bar.

Sasa na hapa naona dogo mwingine - Abdullah kaja na kura za Z'bar ilihali kila siku yuko huku Dar, na Hammer lake, na firm yake - pale Alpha House.

Au Zanzibar ndo kuna u-slope wa kura na sie twende!?

Hussein alikua mbunge Mkuranga siyo mafia, kabla ya kuhamia huko znz na Adam malima kuchukua mkuranga..hawa jamaa ndiyo ni wabara na tukivunja muungano hii familia itataabika sana baba mtu atabaki Tanganyika kwa sababu ana heshima zaidi huku, watoto kujijenga kisiasa au la wanaweza kwenda zenji
 
Hivi kama vipi kumbe Mzenji akiona vipi anaweza kuja Bara kugombea Ubunge lakini M-bara hawezi kugombea ubunge Zenji! duh kweli Muungano huu ni uchawi mtupu.
 
Hawa ndio walioshinda kuwa wabunge wa Afrika Mashariki ,Shayrose Banji,Anjela Charless Kizigha,Mwinyi Hassan,Taslim Twaha Issa, Kesi Ndelakindo Perepetua, Kimbisa Adam Omary,Murunya Bernad,Makongoro Nyerere na Yahya .

Tunawapongeza kwa ushindi huo na pia tunawatakia kila la kheri katika majukumu yaliyo mbele

Huyo Angela Kizigha ndiye alikuwa mgombea wa CCM jimbo la Kawe?
 
Hongera sana Madam NDERAKINDO PERPETUA KESSY (NCCR)..! Ni dhahiri una sifa zote za kutuwakilisha EALA.! Pia hongera kwa kujibu vizuri sana swali la mh january makamba hapo jana bungeni.!
 
navyojua mwinyi ni mtu wa bara tangu babu yake ukoo wao upo wilaya ya mkuranga tarafa ya mitaranda pembezo mwa kijiji cha kitomondo jina la kijiji chao nimelisahau ila huwa anahudhuria sana kule na mwaka 2000 husen aligombea ubunge kipindi hicho nasoma kitomondo na ndugu zake walifanya kampeni za nyumba kwa nyumba
 
Hivi kama vipi kumbe Mzenji akiona vipi anaweza kuja Bara kugombea Ubunge lakini M-bara hawezi kugombea ubunge Zenji! duh kweli Muungano huu ni uchawi mtupu.

Umetaja moja ya kero za Muungano.Hata hivyo...shiiiii! usiitoe hoja hiyo kwa katiba mpya tarajali.Toa maoni ya kudumisha Muungano tu!
 
6Nd. Nderakindo Perpetua KessyNCCR-M113
7Nd. Twaha Issa Taslima
CUF175


Hawa wamenifurahisha saaaaaaaaaaaaaaana jana kwenye kuomba kura. Mama Perpetua Kessy Prof wa Namba UD so happy for you mama!.
Hili Gwiji Twaha Issa Taslima nakukubali mzee wangu, wewe ni mwanasheria uliebobea. nadhani CUF wamepata mtu hapo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom