Matokeo Form 4: Je, NECTA imewahujumu Wazanzibari?

Status
Not open for further replies.
..nilikuwa kule mzalendo.net nikakutana na malalamiko ya waZNZ kuhusu matokeo ya form 4.




Kama huyu mlalamikaji ndo msomi/mzazi wa zanzibar basi tutarajie jamii ya wa wajinga namba moja duniani kutokea hapo zanzibar.
Mtoto anapofaulu mtihani kwa kuibia ni kujidanganya yeye mwenyewe, watoto wanaolelewa na wazazi wenye mitazamo kama ya huyu mlalamikaji wa zenji hupelekea kuzalisha kizazi cha wajinga ambao watazidi kuifanya zenji kubaki nyuma kitaaluma milele.
Mtoto asiyejisomea kwa jitihada hawezi kufaulu, na mtoto anayejisomea hawezi kupoteza muda wake kuingia na FUTUHI kwenye chumba cha mtihani.
Ni dhahiri mlalamikaji huyu wa zenji anatetea uovu kwa kutumia kivuli cha UISLAM bila kujua kuwa kwa kufanya hivi ni kuzidi kujididimiza kifikra yeye kama yeye pamoja na watoto wa kiislam (regadless of their religious belief) anaowatetea kwa hoja dhaifu za kutafutiza huruma za wananchi kwa kutumia dini.
Otherwise ni ngumu sana mtoto kufaulu kama mda mwingi ataupoteza kufanya maandamano ya kushinikiza uongozi wa shule kujenga msikiti shuleni hapo badala ya kuconcetrate na masomo.
 
Shule nyingi za Zanzibar zimepewa alama ya W.

kwa mfano
S3000 MAZIZINI ISLAMIC SECONDARY SCHOOL DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 1 DIV-IV = 0 FLD = 0 . hawa ni zaidi ya

wanafunzi 51.



Shule inayoapakana majengo , Skuli ya Kiembe Samaki Hakuna W. kina F na D.

Mikunguni, kati ya wanafunzi 42, 5 tu walionekana wameletewa matokeo yao .

Shule ya Jangombe kati ya wanafunzi 176 , 53 wameletewa matokeo yao ya alama za D na F huku mengine yakindikwa (W) .


Shule ya Jangombe ipo karibu na Kidongochekundu ambayo haina W


Shule ya High View ,kati ya wanafunzi 78 , 9 tuShule ya Laureate ni wanafunzi 2 kati 48 . Hizi shule mbili zipo pua na mdomo na Shule ya Chukwani ambayo hakuna aliepewa W.kuna F za kumwaga.


S1352 SUFA SECONDARY SCHOOL DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 5 FLD = 2 kati ya wanafunzi 40, 7 ndio nacte imewaachia.

Hii imepakana na Mwanakekwe C ambayo haina W hata moja


. Shule ya Hamani kati ya wanafunzi 176 wanafunzi 14. shule hii ipo pua na mdomo na shule ya Benbella, haile salas, vikokotoni na Tumekuja hizi zote hakuna W


. Bilali Seminary ni wanafunzi 4, kati ya 46 ndio waliokoswa kubakwa na NECTA. waliobaki ni D na F. shule hii ipo pua na mdomo na Shule ya Nyerere ambayo haina W, imejaa D na F


Shule za Zanzibar zote zipo karibu sana.wanafunzi wanaishi pamoja, wanadurusu pamoja


. Kwa hali ya kawaida inaonyesha mtihani umevuja tena umevuja kupindukia. MTIHANI UNATUNGWA BARA. NA KAMA UMEVUJA ZANZIBAR BASI HATA DAR UMEFIKA, HATA IRINGA NA TABORA UMEFIKA.LKN ZANZIBAR IMETOLOEWA KAFARA

KAZI IPO YA SIMU ZA MKONONI?

.Haya sio yale ya kutumia simu za mkononi. hi lkn jee kama umevuja Zanzibar ushindwe kufika bara?Hivi wabara hawapendi. Kwa upande wa Tanzania bara hamna W. Jee hizi shule zilizofutiwa hao waliopatiwa matokeo wote ni div 4. NECTA IMETUMIA FORUMULAR GANI?


SHULE KAMA KIBASILA, SHULE YA BENJAMINI MKAPA, JANGWANI LICHA YA KULALAMIKIWA KWAMBA WATU WANAFUNZI WAMEKAMATWA NA MTIHANI HAKUNA W
 
Umefanya utafiti au unaandika propaganda za misikitini? Mbona mimi nawafahamu wengi sana waliopitia seminary na wame perform vizuri vyuoni.

Ushahidi wa kimazingira unaonyesha hivyo..(besides msikitini hakuna propaganda usichanganye mambo show respect to other peoples believes)..

Kuna namna tatu shule za kanisa zinapata feva; a. wanapewa mitihani ili waendelee kufaulisha na kuaminiwa b. wamepewa resources through MoU hivyo wana uwezo wa kuajiri walimu wazuri c. wanapendelewa wakati wa kusahihisha mitihani kwani mitihani inasahihishwa kwenye kumbi za kanisa mara nyingi why? wanafanya lobbying..kuhakikisha shule zao zinafaulu d. walimu wanaosahihisha wengi ni wakristo..

Hizo zote ni sababu za kimazingira kuonyesha kuwa kuna upendeleo, mwalimu anaweza kufukuza watu kwakuwa wanataka kusali (level hii ya chuki) akifika kusahihisha mitihani ya shule za zanzibar na kiislam atakuwa na huruma?? ataonyesha chuki full time..

Tuna safari ndefu kuondoa udini Tanzania; yetu macho
 
..hii ni taarifa ya gazeti la Nipashe kuhusu matokeo ya mitihani ya form 4.

MATOKEO KIDATO CHA NNE MAAFA!!

-- shule za serikali zaburuzwa.

-- waliofeli ni asilimia 47.

Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne (CSEE) iliyofanyika nchini Oktoba, mwaka jana, huku kiwango cha kufaulu kikionyesha kuwa kiasi cha asilimia 46.63 na cha kufeli kwa kupata daraja sifuri ni asilimia 53.37
Matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Joyce Ndalichako, yanaonyesha kuwa, licha ya kiwango cha kufaulu kuongezeka kwa asilimia 3.13, bado wanafunzi wengi wameendelea kufanya bibaya katika mtihani huo.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, kati ya watahiniwa 426,314 sawa na asilimia 94.67 waliofaulu kati ya daraja la kwanza hadi la nne ni 180,216.
Hata hivyo, waliofaulu kwa daraja la nne ndio wengi wakiwa ni 146,639 sawa na asilimia 81.3 ya waliofaulu huku wale wa daraja la kwanza, pili na tatu wakiwa ni 33,577 sawa na asilimia 9.8.
Wakati hali kwa watahiniwa ikiwa hivyo, shule za sekondari za kata, zimeendelea kufanya vibaya kulinganisha na zile za watu binafsi.
Pia watahiniwa 3,303 wamefutiwa matokeo kutokana na baadhi kufanya udanganyifu na wengine kuandika matusi katika karatasi zao za majibu ya mitihani.
Hata hivyo, matokeo hayo yanaonyesha wavulana wakiongoza kufaulu mitihani hiyo kwa asilimia 53.53, huku wasichana wakifaulu kwa asilimia 44.36.

WATAHINIWA WA SHULE WALIOFAULU MTIHANI

"Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 177,021 sawa na asilimia 50.40 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo. Hivyo, kiwango cha kufaulu kimeongezeka kwa asilimia 3.13," alisema Dk. Ndalichako. Ongezoko hilo ni sawa na watahiniwa 12,789.

WATAHINIWA WOTE
Alisema jumla ya watahiniwa 225,126 (asilimia 53.37) wamefaulu mtihani huo, wakiwamo wasichana 90,885 sawa na asilimia 48.25 ya wasichana waliofanya mtihani na wavulana 134,241 sawa na asilimia 57.51 ya wavulana waliofanya mtihani.
"Mwaka 2010 watahiniwa waliofaulu walikuwa 223,085 sawa na asilimia 50.74. hivyo, kufaulu kumeongezeka kwa asilimia 3.13," alisema Dk. Ndalichako.

WALIOSAJILIWA KUFANYA MTIHANI
Alisema jumla ya watahiniwa 450,324 walisajiliwa kufanya mitihani hiyo, kati yao wakiwamo wasichana 201,799 (aslimia 44.81) na wavulana 248,525 (asilimia 55.19), idadi ambayo imepungua kwa watahiniwa 7,790 (asilimia 1.70) kati ya watahiniwa 458,114 waliosajiliwa mwaka juzi.

WALIOFANYA NA AMBAO HAWAKUFANYA MTIHANI
Dk. Ndalichako alisema watahiniwa waliofanya mtihani huo ni 426,314 (asilimia 94.67) na kwamba, watahiniwa 24,010 hawakufanya mtihani, ambao ni sawa na asilimia 5.33 ya watahiniwa wote waliosajiliwa.


WATAHINIWA WA SHULE WALIOSAJILIWA
Alisema watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 349,390 wakiwamo wasichana 150,371 (asilimia 43.04) na wavulana 199,019 (asilimia (56.96), idadi ambayo inaonyesha kupungua kwa watahiniwa 14,209 (asilimia 3.91) kati ya watahiniwa 363,589 wa shule waliosajiliwa mwaka juzi.

VITUO VYA MITIHANI
Dk. Ndalichako alisema jumla ya vituo 4,795 vilitumika katika kufanya mitihani hiyo ikilinganishwa na vituo 4,653 vilivyotumika mwaka juzi.

WALIOFAULU MTIHANI WA MAARIFA
Alisema katika Mtihani wa Maarifa (QT) wa mwaka jana, jumla ya watahiniwa 9,069 (asilimia 40.70) ya waliofanya mtihani wamefaulu ikilinganishwa na asilimia 35.17 ya waliofaulu mtihani mwaka juzi.
"Hivyo, kiwango cha kufaulu kwa Mtihani wa Maarufu kimeongezeka kwa asilimia 5.53 ikilinganishwa na mwaka 2010," alisema Dk. Ndalichako.
Alisema katika mtihani huo, watahiniwa waliosajiliwa ni 29,447 ambapo wasichana walikuwa ni 18,019 na wavulana ni 11,428 na kwamba, jumla ya watahiniwa 22,400 (asilimia 76.07) ya waliosajiliwa wamefanya mtihani, wasichana wakiwa ni 13,898 na wavulana ni 8,502.

WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA
Dk. Ndalichako alisema watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 44,910 (asilimia 52.52) ya waliofanya mtihani; wasichana wakiwa ni 20,972 (asilimia 47.90) na wavulana ni 23.938 (asilimia 57.38).
Alisema mwaka juzi watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 46,064 (asilimia 52.09) walifaulu mtihani huo.

UBORA WA KUFAULU KWA JINSIA
Dk. Ndalichako alisema jumla ya watahiniwa wa shule 33,577 (asilimia 9.98) wamefaulu katika madaraja I-III; wasichana wakiwa 10,313 (asilimia 7.13 na wavulana 23,264 (asilimia 12.13).

SHULE BORA
Alizitaja shule 10 bora zilizoko katika kundi la shule zenye watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni St. Francis Girls iliyoko mkoani Mbeya; Feza Boys (Dar es Salaam); St. Joseph Millenium (Dar es Salaam); Marian Girls (Pwani); Don Bosco Seminary (Iringa); Kasita Seminary (Morogoro); St. Mary's Mazinde Juu (Tanga); Canossa (Dar es Salaam); Mzumbe (Morogoro) na Kibaha (Pwani).
Pia alizitaja shule 10 bora zilizoko katika kundi la shule zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Thomas More Machrina (Dar es Salaam); Feza Girls (Dar es Salaam); Dung'unyi Seminary (Singida); Maua Seminary (Kilimanjaro); Rubya Seminary (Kagera); St. Joseph Kilocha Seminary (Iringa); Sengerema Seminary (Mwanza); Lumumba (Unguja); Queen of Apostels-Ushirombo (Shinyanga) na Bihawana Junior Seminary (Dodoma).

SHULE ZA MWISHO
Vilevile, alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa 40 na zaidi kuwa ni Bwembwera (Tanga); Pande Darajani (Tanga); Mfundia (Tanga); Zirai (Tanga); Kasokola (Rukwa); Tongoni (Tanga); Mofu (Morogoro); Mziha (Morogoro); Maneromango (Pwani) na Kibuta (Pwani).
Kadhalika, alizitaja shule 10 za mwisho zenye watahiniwa chini ya 40 kuwa ni Ndongosi (Ruvuma); St. Luke (Ruvuma); Igigwa (Tabora); Kining'inila (Tabora); Ndaoya (Tanga); Kilangali (Morogoro); Kikulyungu (Lindi); Usunga (Tabora); Mto Bubu Day (Dodoma) na Miguruwe (Lindi).

WANAFUNZI WALIOFANYA VIZURI ZAIDI
Aliwataja watahiniwa 10 bora kitaifa kuwa na shule wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Moses Andrew Swai (Feza Boy's-Dar es Salaam); Rosalyn Tandau (Marian Girls-Pwani); Mboni Maumba (St. Francis Girls-Mbeya); Sepiso Mwamelo (St. Francis Girls-Mbeya); Uwella Rubuga (Marian Girls-Pwani); Hellen Mpanduji (St. Mary's Mazinde Juu-Tanga); Daniel Wallace Maugo (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Benjamin Tilubuzya (Thomas More Machrina-Dar es Salaam); Simon William Mbangalukela (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam) na Nimrod Deocles Rutatora (Feza Boy's-Dar es Salaam).

WASICHANA 10 BORA KITAIFA
Pia aliwataja wasichana 10 bora kitaifa kuwa ni Rosalyn Tandau (Marian Girls-Pwani); Mboni Maumba (St. Francis Girls-Mbeya); Sepiso Mwamelo (St. Francis Girls-Mbeya); Uwella Rubuga (Marian Girls-Pwani); Hellen Mpanduji (St. Mary's Mazinde Juu-Tanga); Lissa Chile (St. Francis Girls-Mbeya); Elizabeth Ng'imba (St. Francis Girls-Mbeya); Doris Atieno Noah (Kandoto Sayansi Girls-Kilimanjaro); Herieth Machunda (St. Francis Girls-Mbeya) na Daisy Mugenyi (Kifungilo Girls-Tanga).

WAVULANA 10 BORA KITAIFA
Vilevile, aliwataja wavulana 10 bora kitaifa kuwa ni Moses Andrew Swai (Feza Boy's-Dar es Salaam); Daniel Wallace Maugo (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Benjamin Tilubuzya (Thomas More Machrina-Dar es Salaam); Simon William Mbangalukela (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Nimrod Deocles Rutatora (Feza Boy's-Dar es Salaam); Simon Gabriel Mnyele (Feza Boys-Dar es Salaam); Paschal John Madukwa (Nyegezi Seminary-Mwanza); Henry Justo Stanley (St. Joseph Millenium-Dar es Salaam); Frasisco Paschal Kibasa (Mzumbe-Morogoro) na Tumaini Charles (Ilboru-Arusha).

MATOKEO YA MTIHANI YALIYOSITISHWA
Katibu Mtendaji huyo alisema Baraza limesitisha kutoa matokeo ya watahiniwa 264 wa kujitegemea waliofanya mtihani wa kidato cha nne, 116 waliofanya mtihani wa maarifa na 873 wa shule za binafsi mwaka jana bila kulipa ada ya mtihani hadi watakapolipa ada pamoja na faini.
Alisema ikiwa watahiniwa hao hawatalipa baada ya miaka miwili tangu matokeo yatakapotangazwa, matokeo yatafutwa.
Dk. Ndalichako alisema wengine ni watahiniwa 67 ambao hawajawasilishiwa alama za tathmini ya masomo (Continuous Assessment) katika masomo yote waliyofanya hadi hapo Mkuu wa Shule husika atakapowasilisha pamoja na sababu za kutowasilisha mapema.

WALIOFANYA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI
Alisema Baraza pia limefuta matokeo ya watahiniwa 3,303 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba mwaka jana; ambao kati yao alisema watahiniwa 3,301 ni wa mtihani wa kidato cha nne na wawili ni wa maarifa.
Alizitaja aina za udanganyifu zilizobainika kufanywa na watahiniwa hao kuwa ni pamoja na watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa na notes, simu kufanyiwa mitihani na watu wengine na kubainika wamesajiliwa kufanya mtihani kwa kutumia majina ya wengine wakati walishafanya mtihani.
Aina nyingine za udanganyifu ni watahiniwa kubainika kuwa na mfanano wa majibu usio wa kawaida, kuwa na karatasi zao kuwa na miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika katarasi ya somo moja, kubadilishana karatasi za maswali/vijitabu vya kujibia mtihani ili kuandikiana majibu, au kujadiliana ndani ya chumba cha mtihani.
Pia watahiniwa kukamatwa na vijitabu vya kuandika mitihani zaidi ya moja ambayo moja hakupewa na msimamizi, kubainika kuwa na kesi mbili tofauti; kama vile, mfanano wa majibu, notes, kijitabu cha kujibia zaidi ya kimoja na kubadilishana karatasi ya majibu au kijitabu cha kujibia mtihani.

WATAHINIWA WALIOANDIKA MATUSI
Dk. Ndalichako alisema matokeo mengine yaliyofutwa na Baraza ni ya watahiniwa wanane walioandika matusi katika karatasi za majibu yao.
Alisema kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5 (13) cha kanuni za mtihani.
Dk. Ndalichako alisema kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu, kinaonyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu na kwamba Baraza halitavumilia hata kidogo watahiniwa wa aina hiyo.
"Hivyo, pamoja na kuwafutia matokeo ufuatiliaji zaidi utafanyika ili kuona hatua zaidi wanazoweza kuchukuliwa," alisema Dk. Ndalichako.
Aliwataka watahiniwa walioanza mitihani ya kidato cha sita jana kujiepusha na udanganyifu katika mitihani na pia kuepuka mtindo wa kuandika matusi katika skripti zao au mambo yasiyohusiana na mtihani.

HATMA YA WATAHINIWA WALIOFUTIWA MATOKEO
Alisema Baraza limekuwa likifuta matokeo ya watahiniwa wanaofanya udanganyifu, lakini idadi ya wanaojihusisha na vitendo hivyo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.
"Hivyo, katika kikao chake cha 86 kilichofanyika tarehe 7/2/2012, Baraza liliamua kuwa watahiniwa wote waliofutiwa matokeo yao kutokana na kujihusisha na udanganyifu au kuandika matusi kwenye karatasi zao za majibu hawataruhusiwa kufanya mtihani wa Baraza kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu," alisema Dk. Ndalichako.

VITUO NA WALIOHUSIKA NA UDANGANYIFU
Alitoa onyo kali kwa wamiliki wote wa vituo na shule ambazo zimejihusisha na udanganyifu.
"Tunapenda kuwajulisha wamiliki wote wa vituo vya watahiniwa wa kujitegemea kuwa ni wajibu ao kuhakikisha kuwa kanuni zote za uendeshaji mitihani zinazingatiwa ipasavyo," alisema Dk. Ndalichako.



SOURCE: NIPASHE

Shule nyingi za Zanzibar zimepewa alama ya W.

kwa mfano
S3000 MAZIZINI ISLAMIC SECONDARY SCHOOL DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 1 DIV-IV = 0 FLD = 0 . hawa ni zaidi ya

wanafunzi 51.



Shule inayoapakana majengo , Skuli ya Kiembe Samaki Hakuna W. kina F na D.

Mikunguni, kati ya wanafunzi 42, 5 tu walionekana wameletewa matokeo yao .

Shule ya Jangombe kati ya wanafunzi 176 , 53 wameletewa matokeo yao ya alama za D na F huku mengine yakindikwa (W) .


Shule ya Jangombe ipo karibu na Kidongochekundu ambayo haina W


Shule ya High View ,kati ya wanafunzi 78 , 9 tuShule ya Laureate ni wanafunzi 2 kati 48 . Hizi shule mbili zipo pua na mdomo na Shule ya Chukwani ambayo hakuna aliepewa W.kuna F za kumwaga.


S1352 SUFA SECONDARY SCHOOL DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 5 FLD = 2 kati ya wanafunzi 40, 7 ndio nacte imewaachia.

Hii imepakana na Mwanakekwe C ambayo haina W hata moja


. Shule ya Hamani kati ya wanafunzi 176 wanafunzi 14. shule hii ipo pua na mdomo na shule ya Benbella, haile salas, vikokotoni na Tumekuja hizi zote hakuna W


. Bilali Seminary ni wanafunzi 4, kati ya 46 ndio waliokoswa kubakwa na NECTA. waliobaki ni D na F. shule hii ipo pua na mdomo na Shule ya Nyerere ambayo haina W, imejaa D na F


Shule za Zanzibar zote zipo karibu sana.wanafunzi wanaishi pamoja, wanadurusu pamoja


. Kwa hali ya kawaida inaonyesha mtihani umevuja tena umevuja kupindukia. MTIHANI UNATUNGWA BARA. NA KAMA UMEVUJA ZANZIBAR BASI HATA DAR UMEFIKA, HATA IRINGA NA TABORA UMEFIKA.LKN ZANZIBAR IMETOLOEWA KAFARA

KAZI IPO YA SIMU ZA MKONONI?

.Haya sio yale ya kutumia simu za mkononi. hi lkn jee kama umevuja Zanzibar ushindwe kufika bara?Hivi wabara hawapendi. Kwa upande wa Tanzania bara hamna W. Jee hizi shule zilizofutiwa hao waliopatiwa matokeo wote ni div 4. NECTA IMETUMIA FORUMULAR GANI?


SHULE KAMA KIBASILA, SHULE YA BENJAMINI MKAPA, JANGWANI LICHA YA KULALAMIKIWA KWAMBA WATU WANAFUNZI WAMEKAMATWA NA MTIHANI HAKUNA W
 
Much as shule za kiislam na kutoka zanzibar zina matatizo ya ndani lakini naamini shule hizo zinafanyiwa ujinga fulani baraza la mitihana pamoja na wizara..

Kuna uwezekanao mkubwa kuwa pia baraza wanauza mitihani kwa shule za kikristo kwa siri ili ziendelee kuongoza; kwani watoto hao st. wakifika chuo ni mabogus ile mbaya..

naamini shule za kikanisa zinapewa mitihani; ili ziendelee kuongoza..

Hoja za kitoto kama hizi ndo zinazidi kuongeza jamii ya wajinga ktk dini ya waislam coz nyie kama wazazi badala ya kuchukua jukumu la kukataza watoto wenu waache kupoteza muda ktk faisbuku nyinyi mnatafutiza public sympathy kwa style flani za kilimbukeni chini ya mwavuli wa UISLAM na matokeo yake mnazalisha jamii ya wajinga kuanzia babu mpaka kitukuu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom