Matokeo form 4: Asilaumiwe mtu

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
15,406
31,387
Matokeo yalyotangazwa na baraza la mithihani yanaonekana kuamsha hisia kama si hasira kwa makundi mbali mbali ya jamii. Hisia hizo ni kwasababu kuu mbili, kwanza wingi wa wanafunzi waliofeli na pili kwanini shule za serikali zimeendelea kudorora.
Ni kufuatia mambo hayo mawili, wasomi, wanasiasa na wadau mbali mbali wa elimu wamekuwa wakinukuliwa kwa kauli mbali mbali lakini kubwa ni kuilaumu serikali kwa matokeo hayo. Wengi wameeleza ubovu wa matokeo hayo ni pamoja na kuanzishwa shule za kata.

Wanafilosofia wanasema ukitaka kuua taifa basi sehemu muhimu ni kuua elimu. Na kwahahika sehemeu yoyote duniani yenye maisha duni moja ya sababu ni ukosefu wa elimu. Kwa muktadha huo nakubaliana na hasira za wote waliosemea jambo hili nikijua fika wana uchungu kuona tunaua taifa letu pole pole.

Wakati yote haya yakitokea, hakuna shaka kuwa ongezeko la shule za sekondari bila kujali ubora ni chanzo muhimu sana cha ubovu huu. Ingawa wapo wanaodai kuwa shule za kata zimewezesha watoto wengi kwenda shule, mimi napata taabu kuelewa kama division 0 ina tofauti yoyote na darasa la saba. Nashindwa kuelewa ikiwa elimu ya sekondari tumeigeuza kama Day care ambapo vijana waliobalehe wanakwenda kukutana na pengine kutongozana kuanzia asubuhi hadi jioni na baada ya miaka minne wanakuwa wamehitimu form 4.

Hatuwezi kukwepa ukweli kuwa suala la elimu ni la kitaaluma zaidi kuliko kisiasa. Kama likiongelewa kisiasa basi ukweli utokane na utaalamu(facts). Kwa bahati mbaya katika nchi yetu suala hili liliamuliwa na vikao vya chama na kupangiwa mikakati ikulu, na kisha Lowasa kuingia mitaani na kuwalazimisha watu wanaoishi kwa dola moja kwa siku kuchangia dola 3. Hili sina tataizo nalo, lakini ni Mh huyo huyo ana siri moyoni ya jinsi mabilioni yanavyotafunwa na watu wasiozidi 3 kwa msaada wa viongozi. Huenda haya yote yalifanyika kwa mantiki za kisiasa na sina shaka na hilo.

Kampeni za uchaguzi viongozi wote wa CCM walipita kwa wapiga kura na kuonyesha idadi ya shule za kata walizojenga hata kama ni mbili au moja kwa miaka mitano ya ubunge, lakini walipita vifua mbele. Leo wamekaa kimya kwasababu matokeo mabaya hayagusi watoto wao wanaosoma ''academy'' na wengine kindagateni huko South na Nairobi. Hili si tatizo linalowagusa, na kisha wamesharejea mjengoni Dodoma, tatizo ni nini tena!

Huko nyuma vyombo vya habari vimekuwa vikitoa uchambuzi wa hatari ya shule za kata. Hata humu JF kuna makala nyingi zinazohusu suala hili. Jambo la kusiskitisha ni kuwa mada kama hizi hazina wasomaji wala wachangiaji kwasababu nisizo zijua. Huenda ni kwasababu wengi tumekaa kwenye kompyuta na tunalipwa angalau vizuri kurepea corolla zetu, basi hili halitugusi. Tusichojua ni kuwa taifa likifa kieleimu ndio mwanzo wa maradhi, ujinga na uhalifu ambao unatukuta tutake tusitake. Tunasau kuwa waliofeli ni wadogo, watoto, binamu zetu n.k na kwamba hawa watageuka kuwa vijakazi wa watoto wa vigogo si miaka mingi ijayo.

Kawaida ya Watanzania ni kuwa Reactive na si Pro-active. Sasa tunasikia maandamano kila mahali na malalmiko mengi. Hivi hatukujua kuwa shule bila walimu, maktaba au maabara si shule kamili? Hivi wakati watoto wetu wanapotoka shule tumewahi kuwauliza wana wlimu wangapi na wamejifunza nini? Kama tungeuliza tungejua kuwa shule X ina wanafunzi 400 na walimu 4 wawili wamefeli kidato cha sita na wanajishikiza. Hapo tungejua kuwa matokeo hayatakuwa mazuri na mkakati mpya ungeanza mapema asubuhi, na si kuandamana jioni.

Humu JF ukitaka thread ipate wasomaji na wachangiaji wengi, ongelea dini au kabila, hapo ndipo akili zetu zilipojikita utadhani ndilo tatizo la taifa letu. Sasa tujiulize hizo division 0 (39%) zimechagua dini au kabila? ninani hazikumgusa kama raia wa kawaida! Kuanza kuilaumu serikali sasa hivi ni uvivu na ujuha(Ignorance) kwani tulitakiwa tukemee mikakati ya elimu kupangwa na kamati kuu na kutekelezwa na wanasiasa ambao wengine hata muundo wa darasa hawaujui miaka 5 iliyopita.

Hakuna sababu ya kuilaumu serikali kwasababu lengo ni kutawala majuha na inapotokea hivi kwa wao ni ushindi maana majuha wataongezeka na watoto wao watapeta wakirudi kutoka mamtoni kama wanavyoita.
Kwasasa wananchi wanawajibu wa kuwauliza wabunge wao waliodai kuwa wamejenga shule, je hizi ndizo shule wabunge walizotarajia ziwasaidie wananchi? Waulizeni kabla ya kwenda Dodoma. Wakisema serikali haina pesa waulizeni zile za haraka haraka za kuwalipa Dowans zimetoka wapi?
Na humu JF natoa changamoto kuwa majadiliano yalenge kuboresha maisha ya jamii yetu, malumbano ya kipuuzi juu ya udini na ukabila yasipewe nafasi kwasababu janga linapotekea kama hili halichagui.

Ni kwasabau hizo ninaona maandamano au tuhuma dhidi ya serikali ni reaction isiyo na maana. Tulipaswa tumwambie JK walimu wa form6 aliowaajiri wameanza kuua taifa. Tulipaswa tumwambie JK mkakati wa elimu ni shughuli za wasomi ambao tunao wengi tu na si za chama. Tulipaswa tukemee jambo hili humu JF na tupeleke ujumbe kwa wahusika.
Leo watu wanalalama na kuandamana, hawakuona hatari hii miaka 4 iliyopita tulipowaeleza!! Tusiilaumu serikali kwa uzembe wetu, tujilaumu kwa kutokuwa na mitazamo na fikra za kujenga, kwa kutokuwa makini na kwa kutokuwa Active na sasa tunafanya reaction kufuatia inactivity zetu.
Kama tunadhani elimu ni ghali tujaribu ujinga.

Tusimlaumu mtu, tujilaumu wenyewe.
 
Back
Top Bottom