Matokeo Biharamulo: Chadema yaongoza Mijini, CCM vijijini!

Hizo tatu kwanini hayaja jumlishwa? ama ndo wana anza kuzikiteto na kuzibusanda?

Lakini 4/7 ni dalili njema.. twasubili kwa hamu mkuu.
Tuendelea kusubiri maana haya matokeo ndio tutaingia nayo kwenye uchaguzi mwakani na pia yatatumika kama mwanga kwa ajili ya CHADEMA na pia Pasco tupo Pamoja katika kuleta habari. by the way tunashukuru sana kwa kutuletea matokeo
 
Mh,

Naambiwa CCM viongozi wao washaanza kupotea taratibu... Kuna dalili za CHADEMA kushinda tofauti na mwelekeo wa awali!

Ndani ya 2hrs tutakuwa na matokeo rasmi labda wayang'ang'anie tu
 
tunaendelea kufuatilia ze dataz kutoka kwa wapiganaji wetu... pasco, na wengine... wakuu tunangojea kusikia habari kama zinavyojiri kule mahali....
 
Nadhani zimeshajulikana kata 7 ambapo CHADEMA ilikuwa inaongoza kwa 51% na CCM ikiwa na 48% hivi...

Ngoja tusubiri matokeo ya kueleweka
 
Nadhani zimeshajulikana kata 7 ambapo CHADEMA ilikuwa inaongoza kwa 51% na CCM ikiwa na 48% hivi...

Ngoja tusubiri matokeo ya kueleweka

Mkuu invisible, shukran!!!

hiyo 51% vs. 48% ndio joto linapogoma kushuka.... Nashukuru makeke ya Biharamulo hayakuwa na vibweka kama vile vya Busanda, i would rather see as many Biharamulo campaign style kuliko za busanda ambako vyama vyote tulifuja rasilimali (watu na mali) kibao kwa jimbo moja tu
 
Masikini Mukasa, 2010 hataruhusiwa kukiwakilisha chama chake kwasababu ya issue ya uraia hata hivyo sioni namna ya kuwabadilisha wana Biharamuro within one year and three months. Walichoshindwa wana Kiteto na Busanda, Biharamuro wanakiweza.
 
Wakuu, unajua sasa nadata, ina maana ndo tayali 51% mbadala Vs Fisadi 48% ??
 
Tuvute pumze tungojee matokeo kamili kwani nduli CCM ni kibaka mzoefu bado anamiliki tume ya uchaguzi.
 
Wakuu, unajua sasa nadata, ina maana ndo tayali 51% mbadala Vs Fisadi 48% ??

bado tunasubiri madata yenye uhakika, hata hivyo gape la 3% ni kubwa, ni vigumu sana kuliziba. Hawa jamaa wa Biharamuro wapo poa sana, wanamkoma nyani kimya kimya.
 
Back
Top Bottom