Ujue ugonjwa wa Goita Dalili na Tiba yake

KAKA A TAIFA

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
566
80
Huu ugonjwa nitamwomba dr yeyote wa JamiiForums auzungumzie kwa undani ni mbaya na hatari.

Kuna goiter za aina 2.

Ya kwanza ni ile ambayo uvimbe huonekana juu ya koo
Nyingine ni ile ambayo ipo ndani kwa ndani ya koo.

Kwa kawaida huu ugonjwa unaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland).

Inapokuwa kidogo hufanya eneo juu ngozi /nyama ya koo kuvimba, hii inaashiria kwamba tezi linafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo.

Madini hayo yanapokuwa mengi basi huzidi kwenye mzunguko wa damu na kuchanganyika na vitu vingene ambavyo husababisha kutengeneza kama sumu fulani ambayo huchoma mafuta yaliyo kwenye hifadhi mwilini, mishipa ya fahamu huathirika kiasi kidogo.

Mtu ambaye ameathiriwa na aina hii ya pili, huanza kupunga uzito na umbo la mwili taratibu baadaye madhara yanapoongezeka mtu anaanza kupoteza kumbukumbu, anakuwa na hasira, anakula sana, nywele zinanyonyoka mpaka anapata upara, magoti yanakosa nguvu na mtu anashindwa kutembea.

Moyo kwenda mbio (high blood pressure), macho yanavimba sehemu ya juu kope na jicho lenyewe linatoka nje kama vile linadondoka.

Ugonjwa huu una dalili kidogo zinazofanana na ukimwi kama mtu hatatambulika haraka.

Ni vizuri kuwahi hosipitali ili kupata vipimo na tiba mapema.

goitre-large.jpg

----
Damalu anasema,

Matibabu ya Uvimbe wa Tezi shingo (GOITA)


Neno Goita ni jina linalotumika katika kuliita tatizo la kuvimba kwa tezi ya thairoidi iliyo katika eneo la shingo. Kiufasaha, huu ni ugonjwa wa tezi ya thairoidi. Ugonjwa huu pia unaweza kutokea bila kuonekana uvimbe katika eneo hilo. Ugonjwa huu unaonekana kuwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume, hasa wale wanawake wasiopata muda wa kutosha wa kupumzika na kupata utulivu.

Dalili za Ugonjwa wa Kuvimba Tezi ya Shingo (GOITER)

Dalili za mwanzoni za goita kwa kawaida huwa ni za muda mfupi na hutokea kama mabadiliko madogo ya kihisia na huweza kupitia bila kugundulika. Baadae mtiririko wa dalili nyingine kama vile huzuni, kupoteza uwezo wa kuzingatia na kulia vinaweza kuonekana vikiambata na kuharibika kwa hisia. Pia mgonjwa mwenye tatizo hili huwa anakwazika kirahisi sana.

Kunaweza pia kukawa na kuvimba kwa tezi ya shingo lakini hili haliashirii ukubwa wa tatizo kwani hata tatizo linapokuwa kubwa mara nyingine inawezekana usionekane uvimbe ulio wazi. Dalili hizi huweza kufuatiwa na hisia za uchovu uliopitiliza na kutetemeka kwa mikono pamoja na ukosefu wa nguvu za kuwezesha kutumia misuli ya aina yoyote mwilini. Kwa baadhi ya wagonjwa macho huweza kutokeza kwa nje.

Kupungua kwa uzito ni kati ya dalili zinazoweza kujitokeza zaidi kwa wale wanaoumwa ugonjwa huu na huweza kudumu mpaka kufikia hatua ambapo mgonjwa anajisikia kuwa mdhaifu kupindukia.

Visababishi vya Ugonjwa wa Kuvimba kwa Tezi ya Shingo

Chanzo kikuu cha kuvimba kwa tezi ni ukosefu wa madini joto katika chakula na kutokea kwa maudhi mengine ya kihisia na kimwili kunaweza kuliongezea tatizo Zaidi. Chanzo kingine cha kuvimba kwa tezi ya shingo ni pamoja na mazoea ya kula chakula kilichoondolewa uhalisia wake na ambacho hakikupikwa, pia ulaji wa kupita kiasi wa vyakula vilivyopitia kiwandani na vilivyoondolewa ladha asili

Matibabu

Tunatumia splina liquid chlorophyll na Hawaii spirulina pamoja na bubble C

Hizi ni dawa ambazo zinasaidia kuongeza madini joto mwilini kwa sababu zina madini joyo kwa wingi

Zinasaidia kuongeza vichocheo vya mwili

Zinaondoa uvimbe

Zinaondoa cell zilizokufa na kusaidia kuzalishwa kwa cell hai kwa wingi

Zinaondoa sumu kwenye damu

Zinauwa bacteria wabaya mwili

Zinasawazisha acidic kuwa alkaline hivyo hakuna ugonjwa unaoweza kuendelea kukaa mwilini kwani magonjwa yanashambulia mwili kwa kuwa unakuwa na acid nyingi hivyo kuruhusu magonjwa kushambulia mwili kwa kasi

------------

Influenza anasema

Goita (Goiter) ni hali ya kuvimba kwa tezi ya thyroid. Uvimbe huu hautokani na saratani na kwamba goita si saratani. Tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo. Kazi kuu za tezi ya thyroid ni kuzalisha homoni mbalimbali ambazo husaidia mwili kuthibiti na kufanya kazi zake mbalimbali.

Aina za goita na visababishi vyake
Kuna aina kadhaa za goita. Goita ya kawaida (simple goiter) inaweza kutokea bila kuwepo kwa chanzo chochote cha kueleweka. Wakati mwingine, yaweza kutokea wakati tezi ya thyroid inaposhindwa kuzalisha homoni/vichocheo vya kutosha vya thyroid kwa ajili ya mahitaji ya mwili. Ili kuweza kuendana na hali hii, tezi ya thyroid huongezeka ukubwa ili kufidia upungufu wa homoni za thyroid.

Kuna aina mbili za goita ya kawaida, Goita inayowapata wakazi wa eneo fulani (endemic goiter). Aina hii pia huitwa colloid goiter, na Goita inayotokea maeneo tofauti (sporadic goiter). Aina hii pia hujulikana kama nontoxic goiter.

Endemic goiter au colloid goiter huwapata makundi ya watu wanaoishi maeneo yenye udongo wenye upungufu mkubwa wa madini ya Iodine. Maeneo ya aina hii mara nyingi ni yale yaliyo mbali kutoka pwani ya bahari au yaliyo katika nyanda za juu kutoka usawa wa bahari kama vile mikoa ya Mbeya, Iringa na Rukwa.

Iodine ni madini muhimu yanayohitajika katika utengenezaji wa homoni mbalimbali zinazozalishwa na tezi ya thyroid. Watu wanaoishi kwenye maeneo kama haya wapo katika hatari ya kupata goita kwa vile hawapati madini ya kutosha ya Iodine katika chakula chao.

Matumizi ya chumvi ziliongezwa madini ya Iodine yamesaidia sana kupunguza matatizo ya upungufu wa Iodine miongoni mwa watu wengi nchini Tanzania na duniani kwa ujumla. Hata hivyo, upungufu wa madini ya Iodine bado umeendelea kuzikumba sehemu nyingi za Afrika ya kati, Amerika ya kusini pamoja na Asia ya kati.

Chanzo cha sporadic goiter au nontoxic goiter bado hakifahamiki vema miongoni mwa wagonjwa wengi. Hata hivyo, matumizi ya baadhi ya dawa kama vile lithium pamoja na aminoglutethimide yameelezwa kuwa chanzo kimojawapo cha aina hii ya goita.

Vihatarishi vya goita
Kuna baadhi ya mambo yanayohusiana na kurithi yanayoweza kusababisha mtu kupata goita. Vihatarishi hivi ni pamoja na:
• Kuwa na umri kuanzia miaka 40 na kuendelea
• Historia ya ugonjwa wa goita miongoni mwa wanafamilia
• Hali ya kuwa mwanamke
• Na, kutopata iodine ya kutosha katika lishe

Dalili za goita
Dalili kuu ya goita ni kuvimba au kuongezeka ukubwa kwa tezi ya thyroid. Ukubwa wa tezi unaweza kuwa kijiuvimbe kidogo katika tezi au uvimbe mkubwa kama nundu sehemu ya mbele ya shingo. Kuvimba kwa tezi ya thyroid kunaweza kusababisha mgandamizo katika njia ya hewa na mrija wa chakula, hali ambayo inaweza kusababisha:
• Shida katika kupumua
• Kikohozi
• Sauti kuwa ya mikwaruzo
• Shida wakati wa kumeza chakula
• Wakati mwingine, mishipa ya damu ya shingoni inaweza kuvimba pia na kusababisha mtu kujihisi kizunguzungu pindi anapoinua mikono yake juu

Uchunguzi na vipimo
Ili kuweza kutambua iwapo mgonjwa ana uvimbe kwenye tezi ya thyroid, daktari huchunguza shingo ya mgonjwa pindi anapojaribu kumeza mate yake ili kuona kama kuna uvimbe unaopanda na kushuka wakati mgonjwa anapojaribu kumeza. Daktari pia hupapasa sehemu za mbele za shingo ili kuchunguza iwapo kuna uvimbe wowote maeneo hayo.

Vipimo ni pamoja na:
• Kupima kiwango cha homoni ya thyroxine (free thyroxine fT4)
• Kupima kiwango cha homoni inayochochea tezi ya thyroid kuzalisha homoni nyingine yaani Thyroid stimulating hormone (TSH)
• Ultrasound ya tezi ya thyroid. Ikiwa vivimbe (nodules) vitaonekana wakati wa kufanya ultrasound, mgonjwa hana budi kufanyiwa biopsy (kukata sehemu ya vivimbe hivyo) kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ili kujiridhisha kuwa mgonjwa hana matatizo ya saratani ya thyroid.
• Mgonjwa pia anaweza kufanyiwa uchunguzi wa tezi ya thyroid kwa kutumia teknolojia ya mionzi ya nuklia yaani thyroid scan ambayo, pamoja na mambo mengine husaidia kuonesha jinsi tezi ya thyroid inavyofanya kazi (thyroid uptake)

Matibabu
Goita huitaji matibabu iwapo tu inasababisha dalili zinazomletea mgonjwa usumbufu. Matibabu ya goita hujumuisha:
• Matumizi ya madini ya mionzi ya iodine (radioactive iodine) yaani I-131 kwa ajili ya kupunguza ukubwa wa tezi ya thyroid hususani iwapo tezi hiyo inazalisha kiasi kikubwa cha homoni
• Upasuaji wa kuondoa tezi yote yaani (total thyrodectomy) au kuondoa sehemu ya tezi (partial thyrodectomy)
• Iwapo goita inasababishwa na upungufu wa madini ya Iodine, mgonjwa anaweza kupewa kiasi kidogo cha dawa ya maji aina ya Lugol's iodine au mchanganyiko wa potassium iodine
• Iwapo goita inasababishwa na tezi ya thyroid inayofanya kazi chini ya uwezo wake, mgonjwa anaweza kupewa homoni za thyroid ili kufidia upungufu wowote

Matarajio
Goita ya kawaida inaweza kuisha yenyewe au inaweza kuendelea kuongezeka ukubwa mpaka kumsababishia mgonjwa usumbufu. Kadiri uharibifu wa tezi ya thyroid unavyoendelea, hufikia wakati tezi hii huacha kabisa kutengeneza homoni hali inayoitwa kwa kitaalamu hypothyroidism. Mara chache, goita inaweza kubadilika na kuanza kuzalisha homoni za thyroid bila kuchochewa na kitu chochote. Hali husababisha kuwepo kwa kiasi kikubwa cha homoni za thyroid, hali inayoitwa kitaalamu kama hyperthyroidism.

Madhara ya goita
• Shida wakati wa kumeza au kupumua
• Kiwango cha chini cha homoni za thyroid (Hypothyroidism)
• Kiwango cha juu cha homoni za thyroid (Hyperthyroidism)
• Saratani ya tezi ya thyroid (thyroid cancer)
• Goita yenye vivimbe inayozalisha homoni kwa wingi (toxic nodular goiter)

Kinga
Matumizi ya chumvi ya mezani iliyowekwa madini ya iodine husaidia kuzuia uwezekano wa kupata goita. Aidha inashauriwa kumuona daktari au mtaalamu wa afya pindi unapoona kuna uvimbe wowote sehemu za mbele za shingo.
 
Habari ya mchana wa JF, Can any bady explain to me juu ya huu ugonjwa unaitwa goita
Ni nini chanzo chake au husababishwa na nini na nini matibabu yake, na vile unaweza kuavoid
 
Kuavoid; hakikisha unatumia chumvi ambayo imeandikwa kwamba ina madini ya joto.

Chanzo; kukosa madini joto, nadhani ni iodine kwa lugha ya kiingereza.

Matibabu, namimi cjui
 
A goitre is an enlargement of the thyroid gland that is NOT associated with inflammation or cancer.


Causes, incidence, and risk factors

There are different kinds of goitres. A simple goitre usually occurs when the thyroid gland is not able to produce enough thyroid hormone to meet the body's requirements. The thyroid gland compensates by enlarging, which usually overcomes mild deficiencies of thyroid hormone.
A simple goitre may be classified as either an endemic (colloid) goitre or a sporadic (nontoxic) goitre.

Endemic goitres occur within groups of people living in geographical areas with iodine-depleted soil, usually regions away from the sea coast. People in these communities might not get enough iodine in their diet. (Iodine is vital to the formation of thyroid hormone.) The modern
use of iodized table salt prevents this deficiency; however, it is still common in central Asia and central Africa. Certain areas of Australia, including Tasmania and areas along the Great Dividing Range (for example, the Australian Capital Territory), have low iodine levels in the
soil.

In most cases of sporadic goitre the cause is unknown. Occasionally, certain medications such as lithium or aminoglutethimide can cause a nontoxic goitre.

Hereditary factors may cause goitres. Risk factors for the development of a goitre include female sex, age over 40 years, inadequate dietary intake of iodine, residence in an endemic area, and a family history of goitre.


Symptoms

thyroid enlargement varying from a single small nodule to massive enlargement (neck lump)
breathing difficulties, cough, or wheezing due to compression of the trachea swallowing difficulties due to compression of the esophagus neck vein distention and dizziness when the arms are raised above the head Signs and tests Return to top measurement of thyroid stimulating hormone (TSH) and free thyroxine (T4) in the blood thyroid scan and uptake ultrasound of thyroid -- if nodules are present, a biopsy should be done to evaluate for thyroid cancer


Treatment

A goitre only needs to be treated if it is causing symptoms. The enlarged thyroid can be
treated with radioactive iodine to shrink the gland or with surgical removal of part or all of
the gland (thyroidectomy). Small doses of iodine (Lugol's or potassium iodine solution) may
help when the goitre is due to iodine deficiency.


Expectations (prognosis)

A goitre is a benign (harmless) process. Simple goitres may disappear spontaneously, or
may become large. Over time, hypothyroidism may develop due to destruction of the normal thyroid tissue. This can be treated with medications to replace the thyroid hormone.

Occasionally, a goitre may progress to a toxic nodular goitre when a nodule is making thyroid hormone on its own. This can cause hyperthyroidism and can be treated with radioactive iodine to destroy the nodule.


Complications

Progressive thyroid enlargement and/or the development of hardened nodules may indicate thyroid malignancy. All thyroid nodules should be biopsied to evaluate for malignancy.
A simple goitre may progress to a toxic nodular goitre.
Hypothyroidism may occur after treatment of a large goitre with radioactive iodine or surgery.

Call your health care provider if you experience any swelling or enlargement in the front of
your neck, increased resting pulse rate, palpitations, diarrhea, nausea, vomiting, sweating without exercise or increased room temperature, tremors, agitation, shortness of breath, or signs of hypothyroidism such as fatigue, constipation, or dry skin.


Prevention

The use of iodized table salt prevents endemic goitre.

Source: Goitre - Thyroid Gland Enlargement, Endemic Goitre, Sporadic Goitre, Sydney Australia
 
Wadau salama?nina dada yangu ana tatizo la goiter naomba mwenye kujua matibabu yake pamoja na dawa anijuze tafadhali ili niipate na tuinunue
 
ndugu ugonjwa goitre uko very tricky sababu mtu anaweza kuwa na goitre ukakuta homoni ziko nyingi au zipo kidogo kwa hiyo dawa lazima ujue kama homoni ni nyingi au kidogo, pia dawa zake huwa zina madhara kwenye moyo kwa hiyo mpaka mgonjwa apimwe vizuri ndio aanze kutumia kwa hiyo nivizuri kwenda hospitali akapatiwe vipimo, matibabu ya kudumu ni surgery au vidonge vya radioactive iodine(iodine zenye kutoa mionzi ambayo inaenda kuharibu seli zinazo tengeneza homoni)
 
Wakuu kuna dada yangu age 40+,amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa goita.
Ni shingon upande wa kulia japo uvimbe haujatokeza ila inaonekana kwa mbali sana,
macho huwa makubwa,kizunguzungu,kutetemeka.
Kuna vidonge alipewa akitumia anapata ahueni ila doz ikiisha anarudia dalili zilezile, sasa anawaza kuomba afanyiwe upasuaji maana hana raha kabisa! je, wakuu kuna mwenye ujuzi wa dawa nzuri ya kuponya kabisa?,hasa za kienyeji,
 
Sawa tumekusikia. Dawa ya asili ipo. Unapata dawa mbili , moja ni ya kunywa kila siku kwa mwezi mzima.
Ingine utakuwa unafunga shingoni juu ya goita kila siku kwa muda wa mwezi mzima pia maana zinakwenda
pamoja. Hiyo ya kufunga inabadilishwa mpya kila siku.
Ya kufunga imechanganywa madini ya Iodine, asali na powder ya mdudu aitwae emamau,na ya kula
imechanganywa maganda na mizizi ya miti aina 5 kwa maeleso zaidi piga 0754806828.
 
Wakuu naombeni msaada dawa ya goitre, kuna wifi yangu anaumwa imefika hatua hata akilala anasikia kama anakabwa.
Asanteni sana
 
Kuna vitu vinashangaza sana. Mtu anaumwa badala umpeleke hospital unakuja kuuliza jf

Stupid
 
Doctors...,
Naomba kufahamishwa kuhusu ugonjwa wa goita ,Tiba, na kinga .
 
Wakuu kuna dada yangu age 40+,amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa goita.
Ni shingon upande wa kulia japo uvimbe haujatokeza ila inaonekana kwa mbali sana,
macho huwa makubwa,kizunguzungu,kutetemeka.
Kuna vidonge alipewa akitumia anapata ahueni ila doz ikiisha anarudia dalili zilezile, sasa anawaza kuomba afanyiwe upasuaji maana hana raha kabisa! je, wakuu kuna mwenye ujuzi wa dawa nzuri ya kuponya kabisa?,hasa za kienyeji,
Mkuu Larusai Mux ulipata dawa?
 
Atengeneze juisi kwa kutumia karoti 4, majani mawili ya seleri, robo ya fungu la mchicha na robo ya fungu la giligilani anywe mara moja kila siku. Hata akinywa mwaka mzima hana hasara ilimradi apone.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom