Mateso ya 'Zain one network'

Enny

JF-Expert Member
May 26, 2009
962
130
Huduma za "zein one network " ni mbovu sana. Mimi nipo drc (congo) wiki ya pili sasa nashindwa kuingiza vocha kwenye simu. Nimejaribu kuwasiliana na watanzania wengine waliopo hapa wenye laini za tanzania pia wana matatizo hayohayo.

Mwezi wa december 09 nilikuja dar na laini ya drc nilijaribu kuweka kwenye simu yangu kulikuwa hamna network kabisa.

Naomba kama kuna wahusika waweze kuliangalia hili tatizo.
 
OOOH Enny pole sana Zain watakusaidia ..je ukipiga customer care inakuwaje ?
 
jamaa hao wamenichukulia number yangu ambayo nilikua nayo toka siku ya kwanza Celtel inazinduliwa, kisa tu nilikua sipo nje ya nchi miezi miwili.kwani wao hawana records za kujua huyu ni mteja wetu kindakindaki.
 
hata mi niliwahi kukumbwa na dhahama hii nilipofika tz nikawafata palee makao makuu yao nikawaeleza.wakanisaidia na kisha wakasema wataboresha huduma kwa wote kumbe bado?!!!
 
du kazi kweli kweli! mimi naingiza salio kama kawaida.
huyo ambaye line yake ilifutwa ni kwamba zain wana utaratibu wa kufuta namba zote ambazo hazipo active kwa kipindi cha miezi mitatu, sasa kama walikufutia kwa miezi miwili nadhani hapo kuna kitu. Mimi nipo nje ya nchi ni mwaka wa nne huu sasa na nilichokifanya ni roaming, hivyo line yangu ipo active walau kila baada ya miezi miwili naitumia hata kama ni kutuma sms mbili tatu then naifungia nikijua ipo active kadiri yao. Nadhani lengo lao ni kuondoa idadi ya wateja ambao hawapo active na hii inasaidia kuwa na takwimu za watumiaji halisi, sio mtu akinunua line basi ndio iwe milele hata kama haifanyi kazi.
 
Hongera kama wewe unaingiza salio. Sisi huku DRC imekuwa ni ngumu sana kwa kweli ni mateso. ZAIN wanatakiwa waboreshe huduma zao kwa kweli nikipiga customer care naambiwa wapo busy na wateja wengine nipige baadaye kila nikipiga naambiwa hivyo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom