Mateso ya Vengu (Joseph Shamba), serikali imsaidie!

this is an inflammation of layerz covering the brain.it can be bacterial,viral or fungal. Cjapata data ana infection iliyosababishwa na nini
Meningitis
Meningitis ni uvimbe wa bongo. Kuvimba huku kunasababishwa na virusi, au bakteria au hata pia kutumia dawa fulani. Meningitis ni maradhi yanayoweza kuuwa kwa ajili ya kuwa uvimbe huu hufanyika karibu na bongo; kwa hivyo ugonjwa huu ni dharura umwone daktari.Dalili kuu za ugonjwa huu ni kuumwa na kichwa na shingo, pamoja na homa na kuchanganyikiwa kwa akili, kutapika na kutoweza kustahamili mwangaza na kelele.
Dalili


  • Kichwa kuuma sana
  • Kutokuwa na akili timamu, hii hutokea kwa takriban asilimia 44 ya wagonjwa.
  • Kutoweza kustahamili mwangaza na kelele.
  • Uvimbe juu ya kichwa hufanyika kwa watoto wa umri wa chini ya miezi sita.
  • Dalili zingine zinazopatikana kwa watoto ni kuumwa kwa miguu, kuhisi baridi kali na ngozi kugeuka rangi.
Sababu
Kwa watoto wenye umri wa chini ya miezi mitatu, ugonjwa huu husababishwa na group B streptococcus. Wengine ambao hukaa kwenye matumbo ya binadamu ni kama Escherichia coli

Virusi
Virusi vinavyosababisha Meningitis ni kama enterovirus, herpes simplex virus type 2, varicella zoster virus, herpes zoster, mumps, HIV, na Lymphocytic choriomeningitis.
Meningitis pia huweza kusababishwa na kuenea kwa saratani hadi kwenye ubongo.

Kukinga
Meningitis hukingwa kwa kutumia chanjo. Katika nchi nyingi, watoto wengi hupewa chanjo ya kuzuia Haemophilus influenzae ambayo huondoa bakteria hawa kwa miili ya watoto. Hata hivyo, chanjo hii ni ghali.
Chanjo ya Bacillus Calmette-Guérin imeonyesha kupunguza kiwango cha ugonjwa huu kuenea.
Dawa zinazotumika kuzuia ni kama rifampicin, ciprofloxacin au ceftriaxone.

I know all those stuffs, I just want to know the underlying cause of his meningitis!!
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Nenda mwaisela ndio utajua watu wanaumwa kiasi gani.. huwezi peleka watu wote india
 
mkuu wa kaya alienda kumwona na alipiga nae picha kwani hakuona umuhimu wa kumwokoa kijana?
JK ana desturi ya kuwaona wagonjwa, lakini wengi wa anawatembelea hospitali na kupiga nao picha hufa.
coincidence au tambiko!
 
kwani hawajui serikali inakutumia na kukutupa kama kondomu.acha wateseke ili wakome kutumiwa na serikali!

Sentiment za kipuuzi kama hizi mimi ndiyo huwa sizipendi. Kwani yeye si Binadamu kwa kuwa tu alikuwa anaishabikia Serikali, tuache kuwa katili namna hii kwa wenzetu.
 
Kwa kweli miaka hamsini ya uhuru inatumia gharama kubwa sana. huwezi amini kila halmashauri wamedhimisha, kila mkoa wameadhimisha, kila wizara wameadhimisha na bado wiki ya kilele..... ni kwa nini kufanya mambo makubwa wakati hali zetu ni za kuchechemea
 
Masanja anapiga porojo tu kila alahamisi,jamani jembe langu jembe langu..hawasemi wanamsaidia vipi mwezao

MASANJA: TUMUOMBEENI DUA VENGU



Na Shakoor Jongo
MCHEKESHAJI wa Kundi la Ze Komedy Original, Emmanuel Mgaya a.k.a Masanja amewaomba Watanzania kumuombea dua msanii mwenzake Joseph Shamba ‘Vengu’ anayesumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Akichonga na Za motomoto juzikati jijini Dar, Masanja alisema hali ya Vengu si nzuri na zinahitajika dua za kila Mtanzani ili Mungu amponye ugonjwa huo.
“Vengu anahitaji dua za kila Mtanzania, hali yake bado ni mbaya.

Naamini kuwa dua za watu wengi Mungu atazisikia na kumponya msanii mwenzangu ili aendelee na majukumu mengine kama kawaida,”alisema Masanja.

Masanja aliliongeza kuwa, ingawa Vengu aliyekuwa amelazwa hospitali ameruhusiwa kurudi nyumbani lakini hali yake bado haijatengemaa.



JK amjulia hali Vengu wa Ze Comedy


MSANII WA ZE ORIGINAL KOMEDY JOSEPH SHAMBA (VENGU) HALI YAKE BADO NI MBAYA, RAIS KIKWETE AMTEMBELEA HOSPITALINI.




Vengu wa kwanza kulia akiwa na wasanii wenzake wa kundi la Ze Comedy​






Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali mwigizaji wa Kundi la Ze Original Comedy, Joseph Shamba a.k.a “Vengu”, ambaye amelazwa kwa wiki kadhaa sasa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Vengu mwenye umri wa miaka 28 amejizolea umaarufu kwa kuwaigiza wanasiasa hasa Mrema na ni moja wa waasisi wa kundi la ZeOriginal Comedy.

Rais Kikweteakimfariji mama wa Vengu Hospitalini hapo.

 
Mbona kuna raia wengi tu wagonjwa miaka nenda miaka rudi hatufikirii kuwaombea waende india. Kwani kuonekana kwa tv ndio umekua muhimu?
 
ana non communicating hydrocephalus due to meningitis. Dawa anapewa ila poor response. Ni immunocompetent. Acheni kusingizia madoc! Serikali yenu ya kishkaji yenye genge la walanguzi imeshindwa kuwawezesha madoc kufanya kazi kwa ufasaha zaidi. Muulize zito kama ile operation aliyofanyiwa watanzania hawawezi? Tatizo pesa yote inaishia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya ujinga,na umaskini. Hawafikiri kuziwezesha hospital zetu.

Mkuu umemaliza kila kitu!!

Ila na si watanzania tumezidi mno kulalamika bila vitendo...sukari sasa Tsh. 2,500, mchele Tsh. 2,000 n.k. Halafu bado tunairuhusu serikali itumie mabilioni ya Tsh. katika kufanya kufuru ya sherehe; ni wakati wa sisi waTZ wenyewe kuamua kusema basi...tusitegemee chama cha siasa kutufanyia hivyo.

Hivi tunashindwa kuelewa kwamba serikali ya CCM haipo kwa ajili ya waTZ? Angalia jinsi priorities zao wanavyoziweka; kununua ndege mpya au kichwa kipya cha treni kwa ajili ya kutoa usafiri bora kwa waTZ wote wanaona hakuna pesa. Ila kununua magari mapya ya mamilioni ya shilingi kwajili ya mawaziri, wakuu wa jeshi na polisi, wakurugenzi wa wizara n.k. hawaoni shida!! Kwanini wasijinunulie wao magari used?! Ili kusave pesa angalau tununue ndege au vichwa vya treni vipya!?! Pia kwanini hizo sherehe ambazo hata misingi yake haielewiki zinaendelea kufuja pesa na kodi zetu kiasi hiki? Kwanini hizo pesa zisitumike kuongezea bajeti ya kununua ndege na vichwa vya treni vipya?!

Watanzania tunataka hadi iweje ndio tuone kwamba kwa serikali hii masilahi yetu si jambo la msingi? Kuendelea kulalamika bila matendo itaendelea kuwa kazi bure huku jamaa wakizidi kufanya maisha yetu yawe magumu.

Ni wakati wa kuunganisha nguvu pamoja na kudai taifa letu. Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu!
 
jAQ+13Zgs5XSAhSqouy7KiKIVyJVOqZKRarqQtr0jpdDYQCAbm5v8HHB4TbloparAAAAAASUVORK5CYII=

Jamaa yupo tight tumuombee kwa mwenyezimungu ampe nafuu yeye pamoja na watanzania wengine wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
 
....hakwenda Igunga huyu? Jibu likiwa YES au NO. Wafuatwe CCM,waeleze kwanini ama alienda au hakwenda. Magamba wana siri nzito,hata ukiwa unawashabikia wao bado wanaweza kukutoa kafara. Kumbukeni kafara ya kijana wa tindikali hukohuko Igunga.
 
Back
Top Bottom