Matembezi kwenye Ufukwe wa Mabwawa ya Majitaka

IshaLubuva

JF-Expert Member
Dec 4, 2008
250
11
Kumekuwa na kawaida ya baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma siku za mwisho wa juma kufika katika mabwawa ya majitaka yaliyoko maeneo ya Swaswa (wengine wakiwa wamekodisha tax) kwa ajili ya matembezi. Mimi ni mkazi wa maeneo karibu na mabwawa hayo na mara kwa mara nimekuwa nikiona magari madogo yakifika maeneo hayo.

Picha ninayoipata ni kuwa wakazi wa Dodoma na mikoa mingine ambayo haipakani na bahari au kuwa na maziwa wanakosa kweli uhondo wa kupata fursa ya kutembelea maeneo ya ufukwe nyakati za mwisho wa juma kwa lengo la kujipumzisha au kubadili madhari, hasa kwa wale ambao hawanyanyuagi mioyo (hawanyi vileo). Hivi serikali za mikoa kama Dodoma hawawezi kuwa na mkakati wa kutengeneza mabwawa ya aina ya yale ya majitaka laakini yakawa ya majisafi ili kuwapa furs wakazi wake kujivinjari nyakati za mwisho wa juma na siku za sikukuu?
 
Back
Top Bottom