Elections 2010 Mateja Dar wamkubali Dr Slaa

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,949
1,940
Baada ya mdahalo wa mgombea Uraisi wa chama cha CHADEMA siku ya jumamosi, niltembelembelea mitaa siku ya jumapili ili kupata maoni ya wakazi wa jiji la DSM, nikafika katika masakani ya wavuta unga(mateja) nikawauliza.

Mimi- mnajua uchaguzi mkuu wa mwaka huu unafanyika lini?
mateja- wakajibu tarehe 31-10-2010
mimi- nikawauliza je mnawajua wagombea wa uraisi
mateja- wakajibu ndio
mimi- mnaweza kunitaji
mateja- handsboy(kikwete) na bob silaa(dr slaa) na prof lipumba
mimi- nikauwaliza kati ya hao nani mnamkubali
mateja- wakajibu bob silaa
mimi- niwauliza kwa sababu gani?
mateja- wakajibu sera zake mwanagu siumesikia mwenyewe jana anasema akiingia mjengoni anashusha bei ya bati na udongo ulaya(cement) babaake bob sila
mimi- nikauliza kwanini msimchague kikwete?
mateja- wakajibu handsome ametuyayusha mwanangu amesema maisha bora lakini watu ndio tunazidi kuumia kila kukicha mambo balaa babaake safari mambo yote kwa bob silaa(dr silaa)
 
Wewe mwenyewe ni teja?
na kama siyo teja wewe na hao undugu umeanza lini?

Na tangu lini mateja wakapiga kura?
Acha uhuni hao watabadilika wenyewe na wala Dr. hawezi kuwafuata hao , maana aliyewafuga mwenyewe na kuwaletea unga (Dr. JK) hakuwatembelea
 
Huu ni uwongo mtupu kama alionana nao mbona hajaandika kuhusu kuombwa unga kidogo
Maana wanjua naye ni jamaa yao
Hala hala jirani, Slaa na kura za mateja za wakulima kazikosa?
 
we mwenyewe teja kwani umeacha lini kubwia?
Huyu jamaa bado anabwia au anauza, kwa sababu wasingempa ushirikiano wote huo, Na yeye ubunifu wa kuwakumbuka hao badala ya wengine kautoa wapi!
 
KWISHNE !Mateja mbona hawapigi kura hawa
Tena hawakujiandikisha kabisa, hawana mda. Ukichek wale watu wanawaza makubwa japo hawatayafikia kabisa.
Hawana shahada kabisa!!
Naona hatuna kura pale JK wala nani
 
hao ndugu kati ya 100 waliojiandikisha awafiki 20 sio wakutegemea saaaaanaaaa wapo vijana wengi wa kawaida wanamkubali DK
 
Wewe mwenyewe ni teja?
na kama siyo teja wewe na hao undugu umeanza lini?

Na tangu lini mateja wakapiga kura?
Acha uhuni hao watabadilika wenyewe na wala Dr. hawezi kuwafuata hao , maana aliyewafuga mwenyewe na kuwaletea unga (Dr. JK) hakuwatembelea

Kumbe ukienda kufanya research hadi uwe na uhusiano na hao watu??? ukienda kufanya research juu ya Uchangudoa lazima na wewe uwe changu??? MMh mie nauliza tu!!!
 
Hamjaelewa somo, maana ya somo ni kuwa Dr. Slaa anaeleweka hata kwa watu mnaodhani kuwa hawajui jambo linaloendelea. Hata kama mnasema mateja hawapigi kura lakini nina imani humu JF kunao ambao sio mateja lakini kutokana na ujuha wao hawakujiandikisha halafu wanaleta ushabiki maandazi.

Kaa kimya!
 
Back
Top Bottom