Mategemeo yetu kwa Chadema

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
tunajitahidi sana kuwasaidia Chadema wakamate dola,tunahatarisha maisha yetu na biashara zetu na familiya zetu ili waingie madarakani,lakini mategemeo yetu makubwa ni kuona mabadiliko mara watakapo chukua dola,itasikitisha sana kama Chadema watakuwa na mwelekeo wa kujineemesha kama watani zetu ccm,nasema hivyo kwa sababu tumegundua watanzania tuna mapungufu makubwa katika swala zima la uaminifu,imefika wakati tuseme ukweli tu,Chadema msituangushe kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmeharibu kila nafsi inayotarajia mabadiliko,tunajuanyie ni binadam lakini inabidi mjitoe kwa moyo wenu wote kunusuru taifa letu,naandika haya nikiwa na woga na mashaka moyoni mwangu, iwapo mabadiliko yanayoitajika ndani ya taifa letu hayatatokea itakuwa ni tatizo kubwa,watanzania ni watu wa kuvunjika moyo haraka na hawana subira,kila la kheri chadema tupo nyuma yenu kuwaweka madarakani mlete mabadiliko
 
Wala usihofu....tunachohitaji sasa hivi ni mabadilikio.

tusijidanganye wala kujifurahisha,tunahitaji mabadiliko permanent na lazima tupige hesabu nzuri ili tusikosee mbele ya safari
 
Na iwe kama ulivyonena la sivyo chadema watakiona cha mtemamoto kama si cha mtemakuni!
 
Ulichosema ni kweli kiwango cha uaminifu hasa kuheshimu makubaliano ni tete hapa TZ.

CDM wamefanya vizuri kutupa kauzoefu ka kudai haki zetu baada ya shule wanayotoa. Hiyo nI ndoana itawanasa kama watakengeuka kwenye mwelekeo huo.

Kutushirikisha kwa maana ya CDM kuwa ni chama cha wananchi/wanachama ni utaratibu komavu ambao unanipa matumaini kuwa CDM hawatajisaliti.

Mimi nawaasa waTz wenzangu hatima ya maisha yetu yako mikononi mwetu, kwa jinsi ninavyoona CCM inaondoka, ni mkakati huo huo utumke kuwawajibisha na kuwaadabisha serikali na chama tawala kutimza wajibu wake tofauti na sasa.

KWA SABABU CDM WANASEMA WAO WANAMTANGULIZA MUNGU; MUNGU YUPO KWA WATU KWA HIYO WATAKUWA NA HOFU YA MUNGU
 
tunajitahidi sana kuwasaidia Chadema wakamate dola,tunahatarisha maisha yetu na biashara zetu na familiya zetu ili waingie madarakani,lakini mategemeo yetu makubwa ni kuona mabadiliko mara watakapo chukua dola,itasikitisha sana kama Chadema watakuwa na mwelekeo wa kujineemesha kama watani zetu ccm,nasema hivyo kwa sababu tumegundua watanzania tuna mapungufu makubwa katika swala zima la uaminifu,imefika wakati tuseme ukweli tu,Chadema msituangushe kwani mkifanya hivyo mtakuwa mmeharibu kila nafsi inayotarajia mabadiliko,tunajuanyie ni binadam lakini inabidi mjitoe kwa moyo wenu wote kunusuru taifa letu,naandika haya nikiwa na woga na mashaka moyoni mwangu, iwapo mabadiliko yanayoitajika ndani ya taifa letu hayatatokea itakuwa ni tatizo kubwa,watanzania ni watu wa kuvunjika moyo haraka na hawana subira,kila la kheri chadema tupo nyuma yenu kuwaweka madarakani mlete mabadiliko

mkuu kidogo umejitahidi kufikiria. angalau wewe una imani nao kidogo, mimi haipo kabisa, kwani najua fika walionyuma ya chama cha zomea zomea ni watu walio kwenye system miaka nenda miaka rudi na huwezi kuwatenganisha na huu umasikini tulionao waTZ. na waandishi wa habari wanafanya kazi ya chama cha zomeazomea badala ya kufuata maadili ya taaluma zao.
 
Mmeweka indicators gani zilizowaongoza kujua kuwa chadema will perform better?
Why not TLP, CHAUSTA, CUF au NCCR Mageuzi?
 
Huwezi kumtegemea chizi akuvishe barabara. Chadema ni genge la wahuni ndugu yangu. Soma historia zao wote ni watu wa ajabuajabu kama waganga wa mvua. Mbowe ni form four, lema ni form two mnyika form six, slaa ni muasi wa viapo vya upadiri. Na amevunja alichofunga mungu kwa kumchukua josephine mke wa kijana wa watu. Wabebeni tu lakini mnajisumbua
 
rwanda kila m2 anaeza kwenda, hata yanga walienda na juz wamepigwa 3-0

Usipoteze mtiririko wewee, wale madiwani waCDM walitaka kutumia pesa za walipa kodi kwenda kutanua kule Kigali. Huu sio ufisadi? hapo wanatawala Halmashauri vipi CDM ikipewa keki yote pamoja na mafuta na madini? Mh!!!!!! sina imani na CDM kwani sioni hata chembe ya mabadiliko, uadilifu wala uwezo wa kuleta mabadiliko tunayoyatarajia.
 
Huwezi kumtegemea chizi akuvishe barabara. Chadema ni genge la wahuni ndugu yangu. Soma historia zao wote ni watu wa ajabuajabu kama waganga wa mvua. Mbowe ni form four, lema ni form two mnyika form six, slaa ni muasi wa viapo vya upadiri. Na amevunja alichofunga mungu kwa kumchukua josephine mke wa kijana wa watu. Wabebeni tu lakini mnajisumbua

Mkiti wenu kawaambia hamwezi kula hadi mliwe kiduchu hatuwashangai,Elimu hawa viumbe komba,lukuvi,maji matitu,kikwete mr dhaifu,ndugai,kibajaj,weye,tendwa njaa kali,lowasa,chenge mzee wa rada,napi,mkama,magufuli misifa,walema,hosea,chande,ben nk.Weka cv na nini faida na hasa kwa taifa.
 
mkuu kidogo umejitahidi kufikiria. angalau wewe una imani nao kidogo, mimi haipo kabisa, kwani najua fika walionyuma ya chama cha zomea zomea ni watu walio kwenye system miaka nenda miaka rudi na huwezi kuwatenganisha na huu umasikini tulionao waTZ. na waandishi wa habari wanafanya kazi ya chama cha zomeazomea badala ya kufuata maadili ya taaluma zao.

Tunajua kuwa hakuna chama hapa Tanzania ambacho hakina watu walio kwenye system, uzuri ni kwamba Chadema inatufundisha kukubaliana/kufuata na nguvu ya umma. Chadema ikiingia madarakani nguvu ya umma (ambayo ni Demokrasia) itailazimisha system kuusikiliza umma na kufanya kile ambacho ni maslahi ya umma.
Chadema ikiigia madarakani, ni ushindi kwa umma. Vinginevyo, ni ushindi kwa ufisadi,ubadhirifu wa mali ya umma, kulindana (huyu mwenzetu), kutokuwajibika, uhalifu wa kidola na upuuzi mwingine mwingi tu tunaouona sasa hivi.
 
Siku zote huwezi kupima ukapima kiwango cha mvua kwa kuangalia wingu.
I'm proud to be born an adventist church member.
 
Back
Top Bottom