Matawi ya SAUT Songea na Bukoba Yazinduliwa: Zawadi ya TEC Miaka 50 ya Uhuru

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
520
Wakazi wa Songea hawaamini macho na masikio yao baada ya SAUT kufungua chuo kikuu katika mji huo na wa Bukoba sasa hawatafunga safari ndeeefuuu tena kufuata elimu dar na kwingineko kufuata chuo. Shukrani za pekee ziliendee Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kwa kuratibu mpango mzima na kudhihirisha kuwa madhehebu ya dini yana manufaa katika mambo ya maendeleo zaidi ya kugombania kuonekana dini gani ndo ya Mnyaazi Mungu na kukashifu wengine katika midahalo isiyo na tija na kupoteza muda!!

Last edited by a moderator:
Hongera zao kuna wale wanaopenda kusema ni mfumo kristo waambie waje watoe matamko.kuwa wanaonewa .
 
Ukombozi huu kwa WanaRuvuma.
Serikali vivu kama yetu kwanini haiigi mfano kwa makanisa?...kujenga hiyo Yudom imekuwa wimbo wa Taifa!
 
Mpango wa Kitima (Under TEC) ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo kikuu at a most affordable tuition fee.

Guys. its all about being strategic in life. Siyo kubaki katika kupiga kelele "tunaonewa SANA, 2nanyanyaswa SANA, hatutavumilia huu mfumo ......."

Be blessed my Right, Most Rev Catholic Bishops. Na uzuri mwingine ni kuwa hutakuta wanachuo wanalazimishwa "kuvaa rozary" kama wenze2 na cc!
 
Wametangaza chuo ni kwa watu wote wa dini zote na imani zote hakuna masharti na ada ni nafuu mno laki tano kwa mwaka!!!
 
Ni jambo jema kuendelea kufungua taasisi za elimu ya juu kila kona ya nchi. Cha kuzingatiwa ni utoshaji wa qualified instructors/lectures, na facilities nyingine kama library, madarasa na in general ubora wa kiwango cha elimu inayotolewa na hiyo taasisi husika
 
Wametangaza chuo ni kwa watu wote wa dini zote na imani zote hakuna masharti na ada ni nafuu mno laki tano kwa mwaka!!!

dah!kweli saut nouma,ni kozi gan ztakua znafundshwa hapo?
 
Ukombozi huu kwa WanaRuvuma.
Serikali vivu kama yetu kwanini haiigi mfano kwa makanisa?...kujenga hiyo Yudom imekuwa wimbo wa Taifa!

serikali ambayo raisi wake kutwa nzima yuko ughaibuni kuomba misaada anasababisha taifa letu ligeuke na kuwa TAIFA LA MASHOGA
 
Tunaamini kuwa hao wanachuo watakuja kuiweka sawa Historia ya wapiganaji wa vita vya majimaji na majina yao yatarudishwa kwenye kumbukumbu kama yalivyo.
 
watoto wa mama mdogo watazidi kununa maana wako buzy kule kwa uzi wa mohamed said
 
Bora Mungu atitangatili, ndava kugendagenda shida sana,
Kila siku te tavakumpepe tuu, mwe Nchimbi ni Gaudensia, komba siju vi kitakikwali, shida tuu. Kazi miziki tuu, Mipira,michezo layombo ndi kabisa awonjili tuu Uwaziri kidogoooo basi vakambii""nga.

Mungu weeeee
 
Mpango wa Kitima (Under TEC) ni kuhakikisha kila mkoa unakuwa na chuo kikuu at a most affordable tuition fee.

Guys. its all about being strategic in life. Siyo kubaki katika kupiga kelele "tunaonewa SANA, 2nanyanyaswa SANA, hatutavumilia huu mfumo ......."

Be blessed my Right, Most Rev Catholic Bishops. Na uzuri mwingine ni kuwa hutakuta wanachuo wanalazimishwa "kuvaa rozary" kama wenze2 na
cc!

Mkuu wa kaya badala ya kupanga mipango endelevu yeye yupo kwenye udini tu. Hangalia kanisa limejenga chuo kwa dini zote.
 
Bora Mungu atitangatili, ndava kugendagenda shida sana,
Kila siku te tavakumpepe tuu, mwe Nchimbi ni Gaudensia, komba siju vi kitakikwali, shida tuu. Kazi miziki tuu, Mipira,michezo layombo ndi kabisa awonjili tuu Uwaziri kidogoooo basi vakambii""nga.

Mungu weeeee

Mwe kigindaginda mivuvu vuvuku kacholi kacholi!!! Kaka umeongea lugha gani kimsumbiji au toa tafsiri bana na Nchimbi kafanyeje kwny ishu hii!!
 
Bora Mungu atitangatili, ndava kugendagenda shida sana,
Kila siku te tavakumpepe tuu, mwe Nchimbi ni Gaudensia, komba siju vi kitakikwali, shida tuu. Kazi miziki tuu, Mipira,michezo layombo ndi kabisa awonjili tuu Uwaziri kidogoooo basi vakambii""nga.

Mungu weeeee

Wenga niwona ufuna ngondo kuwaliga wayaku ndavayakiki? Kwali wa mwene! songea magono haga kuchele Mtega awaleti chuo. mumtangatilai nipiliki mwaka ujao viwanza kavili chuo cha madaktari kupera mihu.
 
Tunaamini kuwa hao wanachuo watakuja kuiweka sawa Historia ya wapiganaji wa vita vya majimaji na majina yao yatarudishwa kwenye kumbukumbu kama yalivyo.

Kwani nani aliyaondoa majina ya wapiganaji wa majimaji kwenye historia? Halafu hawa wanaosoma sasa, ni kazi yao kuiandika tena upya historia au ni kuendeleza pale ambapo wengine wamefikia? Well, kila mtu ana strategies zake. Ntafanya makosa kufikiria kama mtu mwingine. What i wish to see for this country is the progress in the right direction!!! Wenye wivu acha wajinyonge, I dont care!!!
 
Hii imetulia. Kama wataweza kuweka matawi sehemu nyingi na yakawa affordable na kutoa elimu bora, watu wengi zaidi wataweza kusoma. Itatusaidia sana kama tutakuwa na jamii kubwa ya watu waliosoma na kupanua uelewa wao katika kukabili changamoto za maisha
 
Kwa mwendo huu siku si nyingi nitabadili dini na kuwa mkristo..naona hawa wenzetu wana hekima sana
 
Back
Top Bottom