Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Mkuu Pindamilia,
Asante sana kwa mchango wa mawazo yako katika hili suala.
Benjamini William Mkapa alikula kiapo cha kuilinda Tanzania, watanzania na mali zao kwa moyo wake wote, nguvu zake zote na akili zake zote. Hii ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba mali na utajiri wa nchi unakuwa chini ya wananchi, na wala si chini ya wageni ama watu wachache na ni kitu ambacho hata yeye mwenyewe Mkapa kwa sasa anakubali kwamba alifanya kosa na anajutia.
Kama Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania alipaswa kuelewa kwamba yuko pale ikulu kwa ajili ya Watanzania na si vinginevyo. Tumejionea wazi kwamba Mkapa amevunja ama amekiuka kiapo alichokula. Alipageuza ikulu kuwa ofisi za ANABEN LTD kitu ambacho hakupaswa kufanya na wala hakijawahi kutokea katika Historia yetu ya Tanzania kampuni binafsi kuandikishwa na kutumia anuani ya Ikulu. Unakumbuka Bill Clinton alipofanya tendo la ngo'no white house na Monica Lewinski nini kilimkuta?
Mkapa kwa kutumia madaraka aliyokuwa nayo alijiuzia kiwira cool mine (kwa faida yake na kundi lake) na si kwa faida ya watanzania, kitu ambacho hakupaswa kabisa kufanya hivyo. Ukweli ni kwamba Mkapa ana kesi kubwa sana ya kujibu kwa Watanzania na hakuna sababu ya kumtetea.
Matokeo ya Mkapa kuwa Ikulu ni pamoja na Watanzania kuwa wageni katika nchi yao na kundi kubwa la Wananchi ni masikini wa kupindukia, wachache ni matajiri wa kutisha mpaka wanauwezo wa kujiwekea dhamana mahakamani ya Shs bil 6 bila shaka wala hofu.
Wakati huohuo tunasafiri kwenda nchi za nje kuomba msaada wa kuchimbiwa kisima cha maji kinachogharimu shs mil 138 tu kitu ambacho tungeweza kufanya wenyewe kama utawala wa Mkapa ungekuwa makini na kuwajibika kwa wananchi ipasavyo.
Mkapa ametuacha pabaya na kamwe Watanzania hatuwezi kumsamehe kwa uchafu alioufanya.
Mkuu Kidatu,
Pamoja na maelezo yako mazuri nadhani tuiangalie hoja iliyopo mbele yetu hasa tunapochangia thread hii.
Mimi ningependa kuona kuwa unam-challenge Dk. Mvungi kwa kutuambia kitaalam zaidi kuwa wewe una hoja gani.
Tueleze kuwa sheria inayoweza kutumika ni ipi na vifungu gani na chances za kumtia hatia ziko vipi, hapo tutakuwa tunakwenda pamoja lakini hii habari yakuendelea kutuambia amefanya biashara, kiwira, ANBEN nk siyo habari mpya. Tumekwishazisikia siku nyingi sioni sababu ya kuzirudiarudia.
Pili, nilitumia neno muungwana na kukuomba uangalie kama matamko yako katika posting yako ya awali yanalingana na ukweli uliopo, nazidi kukukumbusha kwa vile umesahau kuyajibu hapo juu, tumia uungwana wako kuomba radhi kwa yale uliyoyapotosha. Kufanya hivyo kutakujengea heshima zaidi mbele ya watu wengine.